Kuhani Musa: Aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu

Kuhani Musa: Aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Kuhani Musa Richard Mwacha anasema aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu aliyemuweka pale, ili atamtereshia maarifa na ufahamu wa kuyafanya mambo mazuri yatakayokufanya ufurahie. Sasa wewe huna maombi.......

Alikuwepo Magufuli pale lakini Mungu alimchukua kama alivyokuwa anasema mwenyewe; akamwacha huyu mama, sasa ulitaka ukae wewe!?

Tujifunze kuwaombea viongozi wetu, tuwasupport! Hakuna mtu anayekusudia kufanya mabaya na hakuna mtu ambaye anataka amalize vibaya aache historia mbaya popote pale



Tumsupport Rais na tumuombee sana
 
Nyie pigeni keleleee kuleni sadaka za Mama lakini mkataba wa DP World lazima ufanyiwe marekebisho makubwa kwa maslahi ya Nchi

Hawa watu wanaojiita manabii, mitume,kuhani nk ni nonsense na waongo wakubwa.

Huyu niliona interview yake clouds TV akisema eti alikuwa anafanya kazi Bank huko Arusha wakati aliacha shule std 4
 
Ina maana kuhani hajui kuwa shetani naye ni Mungu?

Ingefaa pia huyo jamaa akiweka wazi ni nani aliyempa ukuhani maana anadhani anatumika kama mtiwa mafuta kumbe ni mtia mafuta wa mchongo.
Yaani kitu chochote kinaweza kuwa mungu wa watu husika.

Kuna watu wanaabudu teknolojia.
 
Huyo naye ni CHAWA tu, kama walivyo CHAWA wengine.

Kusema ukweli ni uchawa eeeh
Kwani imani yako inakufundishaje kuhusu watawala na viongozi😎

Warumi 13:1-2
Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.


Quran Tukufu Sura ya 4 (An-nisaai) Aya ya 59: “Enyi Waumini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu.’’
 
Kwani kina Haruni walipewa na nani 🤣🤣🤣

Ukimjua aliyewapa basi umemjua Yule aliyempa Kuhani Musa Richard Mwacha
Nijuavyo mie Yesu Kristo alihitimisha kila kitu pale kalvari, mambo ya kina Harun na Musa kuwa makuhani yalikomeshwa.

Sasa huyu anayejiita kuhani yametumwa na nani kufufua huduma zilizokomeshwa na Yesu ?
 
Back
Top Bottom