Kuhani Musa Richard Mwacha anasema aliyemuweka Rais Samia kwenye kiti cha urais ni Mungu, kama mnaona kuna mambo ambayo anapaswa kuyafanya ili kuwafurahisha muombeni Mungu aliyemuweka pale, ili atamtereshia maarifa na ufahamu wa kuyafanya mambo mazuri yatakayokufanya ufurahie. Sasa wewe huna maombi.......
Alikuwepo Magufuli pale lakini Mungu alimchukua kama alivyokuwa anasema mwenyewe; akamwacha huyu mama, sasa ulitaka ukae wewe!?
Tujifunze kuwaombea viongozi wetu, tuwasupport! Hakuna mtu anayekusudia kufanya mabaya na hakuna mtu ambaye anataka amalize vibaya aache historia mbaya popote pale
Hawa ndio wanaotumika kuendelea kuwafanya waafrika na waTZ kuwa mazezeta...nakuhakikishia kuna wahubiri waliwaambia waKongo Mobutu alikuwa mpango wa Mungu..
Kusema ukweli ni uchawa eeeh
Kwani imani yako inakufundishaje kuhusu watawala na viongozi😎
Warumi 13:1-2
Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
Quran Tukufu Sura ya 4 (An-nisaai) Aya ya 59: “Enyi Waumini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka miongoni mwenu.’’