DOKEZO Kuhani Musa Richard Mwacha ashitakiwe kwa kuwadhalilisha watoto wadogo

DOKEZO Kuhani Musa Richard Mwacha ashitakiwe kwa kuwadhalilisha watoto wadogo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari,

Huyu jamaa Kuhani Musa Richard Mwacha wa Kimara temboni ni muhuni na hafai kuwa kiongozi wa dini.

Kwanini nasema hivi? Kila siku ya leo ana ibada ambayo huenda mpaka saa nne hivi ya usiku.

Na majira ya usiku katikati ya ibada kinawekwa kipindi cha shuhuda. Ukifuatilia kwa undani utaona ni kama anawapanga watoto wadogo wakajisalimishe kwake yaani wanakwenda kwa Kuhani kukiri kuwa ni wachawi na walikuwa wanakula nyama za watu.

Ni kama wamemezeshwa maneno, kila kitoto cha kike kinasema yeye ni malkia na anakwenda makaburini kula nyama za watu. Huu ni uhuni wa wazi kabisa.

Hebu wenye mamlaka msiishie kutoa vibali vya makanisa tu. Fuatilieni na yanayotendeka huko makanisani. Hili jambo linafanyika kila siku. Fuatilieni kupitia TV yake au classic FM radio.

Shuhuda za fulani kataka kumuua fulani zimejaa na washirika wake wanazipenda sana.
 
Ni shuhuda za uchonganishi na mafarakano na huo sio msingi wa Kikristo. Watu wengi hamjui na mnaulaumu sana Ukristo kwa ajili ya uhuni wa wazi wachache. Uhuni wa watu wachache ni wao wenyewe na hauhusiani na Ukristo. Hii ni sawa na Shehe kubaka, hakuhusiani na Uislamu bali ni mtu mwenyewe.

Msingi wa Ukristo ni imara na umejengwa juu ya Kristo mwenyewe ambaye ndiye jiwe la msingi. Mi ninatumika kanisani huku kwetu na wapo watumishi wenye weledi na maadili mazuri ya kiroho na sio hao wahuni wasiojitambua wala kujua nini wanafanya. Maadili ya Kikristo hayaruhusu shuhuda za namna hiyo wala kuuliza mapepo wala kuwa na visaidizi kama Mafuta, maji, chumvi, udongo, leso, keki n.k.

Sisi tumeachiwa Jina la Yesu. Hilo ndilo liponyalo, liokoalo, litakasalo, lifungualo vifungo, linalotushindia kwa maana hapana wokovu katika mwingine zaidi ya Jina la Yesu. Na katika Jina hilo kila Goti litapigwa likiwepo goti la Kuhani Mussa na la Mkureshi Muddy(56) mme wa Bi. Aisha(9)🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😜😆
 
ni kweli, mfano mlokole akijenga nyumba anaamini kwa imani tu Mungu anamlinda, lakini dini zingine lazima wafukie vitu kujua kuwa kweli kuna ulinzi...
Biblia inasema hekima ya mwanadamu ni upuuzi mbele za Mungu (1 Wakorintho 3:19).Mtu anayemtegemea mwanadamu huyo amelaaniwa.

Huko kufikia vitu kwa ufupi ni kujisalimisha na kuweka nyumba yako yote chini ya mamlaka za giza. Mungu yupo, na tunalindwa na nguvu zake kwa njia ya imani maana maisha ni imani kama alivyosema wenye haki wake wataishi kwa IMANI.
 
Back
Top Bottom