Watu wanachotakiwa kuelewa ni kwamba unapoona pale ibadani huyo kuhani/ mtume au nabii amemtabiria kumponya mtu, hiyo ni kama kupromote ujuzi au vipawa vyake ili watu wengine waone na waamini. Kumbuka kanisa lina waumini wengi na kila mmoja amekwenda pale anashida zake, kwahiyo ile kumsimamisha mtu mmoja au watu kadhaa na kauwafanyia miujiza ni sehemu tu ya kuwajenga watu wazidi kumuamini zaidi. Sasa kwa nyinyi mliobaki anajua tu kuwa lazima mtataka kumuona private. Sasa hapo ndio kiwango cha fedha mnapangiwa. Na kwakuwa alishafanya kwa baadhi yenu kanisani (kama sample) hivyo lazima uamini kua ukionana nae tatizo lako limekwesha.
Mfano mdogo kwa wavuta sigara au wauza karanga. Kunakuwaga na za kuonjesha kwanza ukipenda unalipia.
Kuhusu uwezo walionao sitaki kuongelea sana nisije nikakosea
Ila naamini kuwa kila binadamu ana uwezo, karama na vipawa tofauti tofauti alivyojaaliwa na Mungu, kwakuwa tuna nguvu ya uungu ndani yetu, ni wachache sana wanaoijuwa siri hii. Sema viongozi wetu wadini (baadhi yao) wa wanazitumia kama fimbo ya kukamatia waumini, wanatenda miujiza na kurushia mpira kwa Yesu ndo kafanya muujiza siri inabaki kuwa yake ( wanatuficha hawataki tuujue ukweli).
Kasomeni Uzi wa
Pascal Mayalla Psychic power.
Pia pitieni google na website mbalimbali kusoma kuhusu Third Eye au pineal gland.
Third Eye ni Jicho lisiloonekana lenye uwezo wa kuona mambo ya rohoni na kutenda mambo mengi ambayo hayawezekani kiakili ya kawaida, sisi huku ndo tunaita miujiza.
View attachment 2131640View attachment 2131641