Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Kwahiyo ni Mkongo toka DRC??Huyu anayejiita Kuhani kuna mambo ya kujiuliza sana toka nilipomfahamu akiwa msaidizi wa Mulilege Mukombo au Mzee wa Yesu aliyekuwa na huduma pale Boko magengeni.
Ilikuwa ukifika kwa mzee wa yesu naye alikuwa na style ya Maombi,uponyaji na maombezi kama Mussa Mwacha , baba yake wa kiroho na ndio aliyempokea Kutoka Congo DRC na kumlea kiimani na hatimaye kumuozesha mwanae wa kike kama mtumishi wa kanisa lake akikuombea kwa mbwembwe nyingi za kufunga macho anakupatia mtumishi mussa uende naye kwako nyumbani au Ofisini akakufanyie maombi ni lazima atatoa vibuyu, hirizi na uchawi aina nyingine.
Style hii ya maombi ya kutoa uchawi wanayo wachungaji wengi wanaotokea Congo DRC hapa Tanzania yupo kijana mmoja mchungaji alikuwa pale Kunduchi baada tuu ya Shule ya Bahari ile njia ya kwenda Rungwe Oceanic naye ana upako aina hii lakini ni wa kisanii. Anakuwa anaficha hirizi halafu akija nyumbani mnaomba mmefumba macho anazitupia kwenye mito makochi hata vyungu vya maua.
Mussa amepitia na kukua toka kwa Mzee wa yesu ambaye haieleweki baadae walitofautiana sana mpaka ndoa yake na mtoto wa.mzee wa yesu ikafika mwisho.
Maoni yangu inawezekana ni mtumishi wa mungu lakini sababu ya kuwajua wacongo watumishi wengi wanaongeza nguvu za mitishamba na fahamu kwamba Congo kuna.msitu mkubwa.sana hivyo kuna.mitishamba ya hatari sana. Nguvu za miujiza, nguvu za kuvuta watu au wateja. Unaweza kumfatilia pia mchungaji tajiri Johanessburg Alpha Lukau ambaye kanisa lake lina Bank clerks ukitaka kutoa sadaka unaenda kwa bank clerks una chanja tuu.
Huduma yake ina angalia zaidi nani anatoa hela kiasi gani. Nadhani ukitaka kumuona sio chini ya laki 3 akisisitiza anajenga kanisa hivyo michango ni lazima. Huwa waumini wapo wanaosaidiwa na kinachowaponya ni imani yao na utayari kwa yesu na si nguvu ya mchungaji.
Hilo jina Mwacha asili yake ni huko??