Kwa hivi sasa nchini hakuna mwanasiasa anayekubalika, kueleweka na kupendwa kama Lissu.
Hii ni kwa sababu Lissu ni mkweli, anamaanisha mabadiliko, hana uchu wala tamaa ya vyeo na mali bali ana uchungu wa kweli wa Taifa hili.
Katika blunders kubwa ambazo rais Samia alizifanya punde tu baada ya kuwa rais ni kumkamata Mbowe, hiki kitu kilimshusha sana Samia kisiasa.
Soma Pia: Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma
Sasa kwa sasa Lissu ana mtaji mkubwa wa kisiasa, Iwapo Samia ataamua kutumia ubabe kwa Lissu itamharibia sana taswira yake, kuaminika kwake mbele ya umma na hata akishinda uchaguzi wa mwaka 2025 (Kitu ambacho ni obvious kutokana na sheria mbovu na tume isiyo huru) atapata shida ya imani ya wananchi.
Cha msingi hapa akubali tu kuzitekeleza zile 4R zake, ambapo R moja wapo kati ya hizo ni REFORMS. Kitu ambacho Lissu anakipigania.
Kilichotokea leo huko Mbinga cha Polisi kuwapiga mabomu wananchi ndo kwanza kinawathibitishia wananchi kuwa anachosema Lissu kuhusu mifumo yetu ya haki za kisiasa ni kweli, na inathibisha kuwa NO REFORMS NO ELECTION ni ajenda yenye mashiko makubwa sana.