Wanatekeleza haki yao ya kimsingi, ya kikatiba, ya utu (Universal Declaration of Human Rights), ya kutimiza ibada zao kama walivyoambiwa na dini zao.
Kinachotakiwa ni kuwapanga vizuri wasilete shida kwa watu wengine, mfano, kuwawekea sehemu zao wasiingilie watu njiani, kuwawekea viwango vya kelele ambazo hawatakiwi kuzidisha, na kadhalika.
Lakini, hii ni haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kuabudu, ni haki ya utu wao na sehemu ya Universal Declaration of Human Rights, wengine wanatimiza maagizo ya dini zao, ukiwanyima nafasi hiyo unakuwa umewanyima sehemu ya maagizo ya dini zao sawasawa na kumkataza mtu kwenda kanisani, kutoa zaka, kwenda msikitini au kwenda hija.
Mimi siamini katika Mungu wala dini, ila natetea haki za watu wote kuabudu dini zao wanavyotaka bila kuingiliwa na haki hii ya kuabudu ikiingiliwa, nitawatetea wanaoamini waweze kuendelea kuwa na haki hii.
Kwangu mimi, haki hii haina tofauti na haki yangu ya kutoamini Mungu wala dini, haki hizi (za kuamini na kutoamini) ni pande mbili za shilingi moja ile ile.
Naona nikiruhusu haki ya kuabudu iingiliwe, nitakuwa nimefungua mlango wa kuruhusu haki yangu ya kutoabudu iingiliwe.
Leo mkisema hawa walokole waondolewe wasihubiri barabarani, ndiyo mwanzo wa kutupangia kwamba watu wote waende kuabudu kanisa la Roman Catholic.
Waacheni wahubiri, wafanyieni regulation tu wasilete kero kwa wapita njia na jamii kwa ujumla.