Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Bandari, viwanja vya ndege, electric power supply plants, reli na barabara ni maeneo mhimu sana kiuchumi na kiusalama wa taifa lo lote duniani. Hili halina ubishi. Hivyo umiliki na mamlaka ya uendeshaji yanapaswa kuwa ya taifa lenyewe kwa asilimia 100%. Mamlaka haya hayapaswi kuporwa na mtu, kampuni au taifa lingine lo lote lile. They are national assets kwa mjibu wa katiba yetu.
Miradi katika maeneo haya inapaswa kuwa ya kimkakati ya kuleta maendeleo kwa wananchi. Miradi hii hufanywa na serikali kwa pesa yake au ya mikopo kama ambavyo ilivyofanyika kwenye bwawa la Nyerere na SGR ambako serikali ilitoa kandrasi za ujezi kwa kampuni za Misiri, Uturuki na Uchina kwa utaratibu tuliojiwekea wa competitive international tendering. Hakukuwa na IGA (Intergovernmental Agreement) wala HGA (Host Government Agreement).
Tutatumia zaidi ya TSh trillion 30 kwa miradi hii mikubwa miwili ya SGR na JNHPP. Pesa hizo ni zetu wenyewe zikiwemo nyingi tulizochukua mikopo nafuu ya kimataifa ambayo sisi hadi wajukuu wetu tutazilipa kidogo kidogo bila maumivu yo yote.
Kwa bahati nzuri hiyo IGA na huo mkataba ambao kesho kutwa unaenda kupitishwa (ratify) bungeni, vyote vimewekwa mtandaoni. Wananchi karibu wote walioweza kuusoma wanashindwa kuelewa huu mradi mkubwa wa bandari zetu zote unaotarajiwa kupewa kampuni moja ya Dubai, uko kundi lipi kati ya hayo niliyoyataja kwenye kichwa cha habari cha uzi huu?:
1. Wapo wanaosema serikali inataka kuziuzwa bandari zetu zote kwa kampuni moja ya kiarabu inayomilikiwa na nchi ya Muungano wa falme za Kiarabu (UAE = United Arab Emirates). Ni sawa serikali ina mamlaka ya kuuza baadhi ya mali zake lakini upo utaratibu wake wa kunadi mali hizo. Huwa inatangazwa na watu kushindana kwenye mnada. Sasa hii kampuni imeuziwa bandari zetu kwa bei gani? Mbona hili haliko wazi kifedha kwenye huo mkataba. Serikali itapata manufaa kiasi gani ya kifedha kwa mwaka kutoka kwa kampuni hiyo?
2. Serikali kupitia mtendaji mkuu wa mamlaka ya bandari na msemaji mkuu wa serikali (Musigwa) wanasema hiyo kampuni ya falme za kiarabu imepewa kandrasi ya kujenga/ kupanua bandari zetu na kuziendesha. Kwa maneno mengine to design, construct and operate. Ni kweli ipo aina hiyo ya miradi lakini lazima ijulikane awali mkandrasi huyo anaenda kujenga gani, ramani ya atakachojenga, bill of quantities zake. Lazima ikubalike hiko atakachojenga na ubora wake ndicho tunachotaka. Gharama yake lazima ikubalike kwani mwisho wa yote gharama hiyo lazima itabebwa na wananchi kwani lengo la mkandrasi ni kupata faida to the maximum. La sivyo tutajengewa mavitu substandard na kuletewa mitumba ya mitambo.
Hawajatuambia ata operate hadi lini. Hakuna kipengere cha transfer kama ambacho kimo kwenye ule mradi wa Kigamboni bridge ambao ulikuwa wa design, construct, operate and transfer to government after a certain period.
Musigwa anasema kupanua gati 2 pale bandari ya DSM serikali ilitumia TSH trillion moja, hizo gati zilizobaki serikali ingalitumia trillion 4 na kwa sababu serikali haina hizo trillion 4 ndipo ikaamua kuipa hiyo kampuni iipanue kwa gharama zake. Mkataba hausemi hivyo na kwa hiyo kampuni itafanya inavyotaka na kuweka gharama inayotaka. CEO wa bandari anasema mkataba ni wa mwaka mmoja. Sasa huo upanuzi wa ghati zote hizo na bandari zote hizo zinaweza kufanyika kweli kwa mwaka mmoja?
3. Ubinafishaji kama uliofanyika kwa kiwango kikubwa cha viwanda vyetu enzi za Mkapa, nao unataratibu zake. Waliobinafishiwa walilipa gharama fulani na walishindanishwa. Walipewa sharti la kuwa wakishindwa kuviendeleza kwa ufanisi vitarudishwa serikalini na hawatarudishiwa pesa yao. Inasemekana hii kampuni imetoa dolla million mia tatu (Tsh billion 7). Hivyo inaweza ikawa bandari zetu zote zimebinafishwa kwa kiasi hicho cha pesa ambazo wako watanzania wengi tu wangaliweza kuzitoa hata zaidi ya hapo.
4. Uwekezaji: Utaratibu wake ni kuwa mwekezaji anauziwa ardhi ya kufanya uwekezaji wake husani kujenga kiwanda cha tiles. Baada ya hapo anajenga kwa gharama yake na kuanza uzalishaji. Bidhaa anaziuza mahali po pote kwa bei anayotaka yeye. Serikali hutoza VAT kwenye ya bidhaa zake na humpa masharti ya wafanyakazi atakaoajiri wengi wao wawe ni watanzania na awalipe mishahara isiyopungua kima cha chini kilichowekwa na serikali. Kama kampuni hii ya kiarabu imekuja kwa mgongo huu wa uwekezaji, mbona imekuja kwa mtindo wa mabavu sana. Yenyewe ndiyo inaipa masharti lukuki na magumu serikali yetu, na kuonekana inatunyang'anya bandari zetu zote. Hatutakuwa tena na mamlaka kamili juu ya bandari zetu, kitu ambacho kinaweza kuleta changamoto kwa ulinzi na usalama wa nchi yetu.
5. Public Private Partnership: Hili nalo lina utaratibu wake. Hususani ule ujenzi wa barabara ya express way ya kutoka kibaha hadi Morogoro, mtu au kampuni binafsi itaijenga kwa gharama zake halafu watu watakuwa wanalipia kupita barabara hiyo. Au SGR inayojengwa na serikali, watu au kampuni binafsi watakaoweza kumiliki mabehewa na vichwa vyake wataruhusiwa kufanya biashara ya usafirishaji kwenye reli hiyo.
6. Kukodisha au kupangisha: Mtu ukimukodisha au kumpangisha anakuwa anakulipa fedha kila mwezi au kila mwaka. Na anabidi afuate masharti yako na si yeye aje na masharti yake.
7. Kutapeliwa: Hii kampuni kuna viashiria vingi vya kutaka kututapeli bandari zetu. Ni vyema hii miradi mikubwa tukaifanya kwa pesa yetu wenyewe hata kama ni ya mkopo. Tunaweza kuajiri technical consultants wa kutushauri jinsi ya kufanya bora zaidi. Tunaweza kuajiri wakandrasi wa nje au ndani kufanya hizo kazi za kushusha na kupakia mizigo kutoka kwenye hizo meli kama alivyokuwa anafanya TICC. Tunaweza kuajiri au kukodi kampuni za kuzitangaza bandari zetu duniani ili kupata wateja zaidi. Tusitake kujidharirisha kwa taifa lingine lo lote kwamba sisi hatuwezi kufanya mambo haya.
Tuwaombe wabunge wetu wapitie kwa makini hiyo IGA na huo mkataba utakaofikishwa bungeni kesho kutwa.