Sehemu sahihi zaidi ya kufanya biashara ni mji wa Masasi.
Kwa sababu zifuatazo:-
1. Mji upo katikati ya Newala na Tandahimba upande wa kusini, Nachingwea na Liwale upande wa kaskazini, Lindi vijijini, Ruangwa na Lindi Manispaa au Mtwara Manispaa upande wa mashariki; wilaya ya Nanyumbu (Mangaka), Tunduru na Songea (mkoa wa Ruvuma) kwa upande wa magharibi.
2. Mwingiliano wa makabila mbalimbali.
Ukiwa Masasi utakuta watu toka sehemu au mikoa mbalimbali wanafanya biashara mji wa Masasi.
Hivyo basi ukiachana na kilimo shughuli nyingine za kiuchumi ni biashara kubwa na ndogo ndogo katika mitaa ya Mkuti, Kaumu, Tandale, Wabiso, nk. Kwa hiyo hukosi pesa kama utajikita kutoa huduma bora kwa jamii.
NB:
Changamoto za biashara hazikosi unapokuwa ugenini ila sio za kuziogopa.