Kuhusu DP World: Rais Samia acha kushupaza shingo, epusha Taifa na machafuko

Kuhusu DP World: Rais Samia acha kushupaza shingo, epusha Taifa na machafuko

CONSISTENCY

Senior Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
135
Reaction score
309
Kuhusu hili jambo la mkataba wa umiliki wa bandari zote kati ya serikali ya Tanzania na kampuni DP World tumeona maoni mbalimbali kuhusu vipengele vya huo mkataba.

Mkataba huo umekosolewa kwa mapana yake kwa kila kipengele kwamba haufai na watu waliokosoa hawajafanya kwa political interest ila wamekosoa kwa uzalendo wao watu hao wametoka kada tofauti kuanzia viongozi wa dini, siasa, wanasheria , taasisi za elimu, wasomi n.k

Miongoni mwa watu waliokosoa mkataba huo ni pamoja na

1. Waziri mkuu mstaafu Jaji Warioba.
2. Waziri mstaafu Professor Ana Tibaijuka
3. Mzee Butiku
4. Nguli wa sheria Professor Issa Shivji
5. Raisi mstaafu wa TLS Dr Nshala ambaye ni msomi mkubwa katika sheria kutoka chuo kikuu cha Havard kilichopo nchini Marekani.
6. Makamu Mwenyekiti wa Chadema na Mwanasheria ndugu Tundu Lisu
7. Kardinali wa Kanisa Katoliki Pengo.
8. Askofu Mwamakula
9. Mawakili na wanasheria tofauti wakiongozwa na ndugu Bonifasi Mwabukusi ambae hadi amefungua kesi Mahakama kuu kanda ya mkoa wa Mbeya.
10. Wananchi kutoka Tanzania na nje ya Tanzania - Diaspora
11. Mwenyekiti wa CUF Professor Lipumba
12. Mwenyekiti wa Chadema ndugu Mbowe
13. Chama cha sheria na haki za binadami ( LHRC)
14. Balozi mstaafu Dr Slaa
15. Kitima
16. N.k

Serikali yako Samia imeshindwa kutoa majibu ya mapungufu ya vipengele vya huo mkataba baada yake imeanza propaganda kwa kuongopa na kualika watu mbalimbali akiwemo msemaji wa serikali msigwa, waziri mkuu majaliwa, wasanii na watangazaji n.k ili wapotoshe ukweli wa mapungufu ya huo mkataba wa hovyo.

Leo tumesikia wanasheria huru wakilalamika kutishiwa maisha, miongoni mwa wanasheria hao ni raisi mstaafu wa TLS Dr Nshala na ndugu Bonifasi Mwabukusi kutoka Mbeya. kuhusu hili jambo endapo mtu yeyote akipata tatizo kutokana na kutetea bandari hakuna mtu atabaki salama miongoni mwenu ikiwemo ninyi viongozi, familia pamoja na ndugu zenu popote walipo.

Wito wangu kwa Rais Samia acha jeuri kuhusu maoni ya watanzania kuhusu ubovu wa huo mkataba, wananchi ndio wenye nchi hivyo kama hawaitaji huo mkataba usijitoe ufaham kwa kuwapuuzia.

Nchi yetu ni ya amani, hivyo hatutaki uvunjifu wa amani kwa sababu za maslahi yako binafsi Samia.

Kama wananchi hatutaki kufikia hatua ya maandamano na uvunjifu wa amani ila itakapobidi hatutakua na namna zaidi ya maandamano yasiyo na mwisho.

Bandari ni zawadi yetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu lazima tutailinda kwa namna zote iwe heri au shari
 
Huu mkataba wakilazimisha kutekeleza mkataba huu huko mbele kutakuwa na shida kati ya serikali na raia
Upo sahihi kabisa, shida itakayokuwepo sio ndogo.
Samia uwezo wa akili ni mdogo sana ila analazimisha mambo asiokua na uwezo nayo.
Samia anatakiwa ajue kwamba huo uongozi ni jambo la mda mfupi tu ila Tanzania itabaki milele na milele
 
Kaanzisha songombingo nyingine ya Mwekezaji awe pia na haki ya kumiliki ardhi...Huyu bi Mkubwa haya mambo mbona Zanzibar hayapeleki?
 
Kaanzisha songombingo nyingine ya Mwekezaji awe pia na haki ya kumiliki ardhi...Huyu bi Mkubwa haya mambo mbona Zanzibar hayapeleki?
Ni jambo la mda tu, hili jambo la mkataba wa bandari haliwezi kupita hivi hivi.
Samia asipotengua huo mkataba lazima alipie gharama
 
Ni jambo la mda tu, hili jambo la mkataba wa bandari haliwezi kupita hivi hivi.
Samia asipotengua huo mkataba lazima alipie gharama
Kwakuwa wawakilishi wa wananchi (bunge) wameridhia; kwakuwa serikali imetoa ufafanuzi wa jinsi gani hawa wanasheria walionunuliwa na hawa 'great thinkers' fake 20 wa humu jf wanavyopotosha na kwakuwa wananchi huku uraiani wameshaelewa muda tu na nyie wanakuoneni kama mabonto tu a.k.a vikatuni, basi hayo machafuko labda yatatokea katika familia yenu katika kugombea urithi. Tanzania itaendelea kubaki salama chini ya Jemedari Jasiri Mama Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania!!!!!!
 
Kuhusu hili jambo la mkataba wa umiliki wa bandari zote kati ya serikali ya Tanzania na kampuni DP World tumeona maoni mbalimbali kuhusu vipengele vya huo mkataba.

Mkataba huo umekosolewa kwamba haufai na watu kutoka kada tofauti kuanzia viongozi wa dini, siasa, wanasheria , taasisi za elimu, wasomi n.k
a usijitoe ufaham kwa kuwapuuzia.

Nchi yetu ni ya amani, hivyo hatutaki uvunjifu wa amani kwa sababu za maslahi yako binafsi Samia.

Kama wananchi hatutaki kufikia hatua ya maandamano na uvunjifu ila itakapobidi hatutakua na namna zaidi ya maandamano yasiyo na mwisho.

Bandari ni zawadi yetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu lazima tutailinda kwa namna zote iwe heri au shari
KILA ZAMA NA KITABU CHAKE, ACHENI KUMTISHIA RAIS WETU, NA HAKUNA WA KUTHUBUTU KUFANYA FUJO / MACHAFUKO WALA CHOCHOTE, RAIS WETU SONGA MBELE!
 
Upo sahihi kabisa, shida itakayokuwepo sio ndogo.
Samia uwezo wa akili ni mdogo sana ila analazimisha mambo asiokua na uwezo nayo.
Samia anatakiwa ajue kwamba huo uongozi ni jambo la mda mfupi tu ila Tanzania itabaki milele na milele
Kumuelewa Samia inabidi uwe umeshiba kichwani, tena ushibe sana! Tofauti na hapo utageuka kituko kwa wenye akili kutokana na uharo utakaokuwa unaumwaga kutoka kinywani. Mama si levo zenu ndo maana jpm kwa misimu miwili alishindwa kabisa kuwa mbali nae. Pumbaaaaav senu!!!!
 
Back
Top Bottom