Kuhusu hili jambo la mkataba wa umiliki wa bandari zote kati ya serikali ya Tanzania na kampuni DP World tumeona maoni mbalimbali kuhusu vipengele vya huo mkataba.
Mkataba huo umekosolewa kwamba haufai na watu kutoka kada tofauti kuanzia viongozi wa dini, siasa, wanasheria , taasisi za elimu, wasomi n.k
Miongoni mwa watu waliokosoa mkataba huo ni pamoja na
1. Waziri mkuu mstaafu Jaji Warioba.
2. Waziri mstaafu Professor Ana Tibaijuka
3. Mzee Butiku
4. Nguli wa sheria Professor Issa Shivji
5. Raisi mstaafu wa TLS Dr Nshana ambaye ni msomi mkubwa katika sheria kutoka chuo kikuu cha Havard kilichopo nchini Marekani.
6. Makamu Mwenyekiti wa Chadema na Mwanasheria ndugu Tundu Lisu
7. Kardinali wa Kanisa Katoliki Pengo.
8. Askofu Mwamakula
9. Mawakili na wanasheria tofauti wakiongozwa na ndugu Bonifasi Mwambukusi ambae hadi amefungua kesi Mahakama kuu kanda ya mkoa wa Mbeya.
10. Na wananchi kutoka mikoa yote ndani ya jamhuri ya Muungano wa Tanzaania
11. Mwenyekiti wa CUF Professor Lipumba
12. N.k
Serikali ya Samia imeshindwa kutoa majibu ya mapungufu ya vipengele vya huo mkataba baada yake imeanza propaganda kwa kuongopa na kualika watu mbalimbali ili wapotoshe ukweli wa mapungufu ya huo mkataba wa hovyo.
Leo tumesikia wanasheria huru wakilalamika kutishiwa maisha, miongoni mwa wanasheria hao ni raisi mstaafu TLS ndugu Dr Nshana na ndugu Bonifasi Mwabukusi kutoka Mbeya. kuhusu hili jambo endapo mtu yeyote akipata tatizo kutokana na kutetea bandari hakuna mtu atabaki salama ikiwemo ninyi familia na ndugu zenu.
Wito wangu kwa Rais Samia acha jeuri kuhusu maoni ya watanzania kuhusu ubovu wa huo mkataba, wananchi ndio wenye nchi hivyo kama hawaitaji huo mkataba usijitoe ufaham kwa kuwapuuzia.
Nchi yetu ni ya amani, hivyo hatutaki uvunjifu wa amani kwa sababu za maslahi yako binafsi Samia.
Kama wananchi hatutaki kufikia hatua ya maandamano na uvunjifu ila itakapobidi hatutakua na namna zaidi ya maandamano yasiyo na mwisho.
Bandari ni zawadi yetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu lazima tutailinda kwa namna zote iwe heri au shari