Kuhusu Kauli ya Dr. Nchimbi (VP): Ni aidha Kuna mgogoro ndani ya serikali na CCM au mbinu ya CCM ya "jifanye uko nao, then strike hard"

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592
Hebu jaribu kidogo kufikiri hili;

KWAMBA; Ana Rais yuko madarakani na yeye ni Makamu wake, yaani kiongozi mkuu wa serikali Na. 2...

Na, chama chao ndicho kiko madarakani, kinaongoza serikali....

Na siku si nyingi amekuwa Katibu Mkuu na kada mbobezi wa chama chao karibu maisha yake yote hata kufikia hapo alipo...

Which means, wanajua watu na wananchi wanataka Katiba mpya na huyo Na. 1 wake, Rais anataka hicho hicho...

Hawa wote wawili ambao kwa vyovyote vile kabla jambo lolote kubwa ktk nchi halijafanyika au kutokea lazima wao wawili na pengine na yule Na. 3 (Waziri Mkuu) wawe wamekutana na kukubaliana na Kisha ndipo agizo linatoka juu na kushuka chini kwa utekelezaji....

Sasa sikiliza na tazama "demeanor" ya VP Dr Emmanuel Nchimbi alipokuwa akiongea...

Na msiojua, tambueni kuwa VP hawezi kwenda kwenye kusanyika hilo kama Guest of Honor bila kupata ridhaa ya boss wake pamoja na kile atakachokwenda kuongea....

Aidha, tukumbuke pia kuwa, risala za matukio kama hili alilohudhuria Dr Emmanuel Nchimbi kama mgeni rasmi zikimhusisha kiongozi fulani mkubwa toka serikalini hupelekwa kwao siku kadhaa kabla ya siku ya tukio Ili kama kuna hoja zenye maswali magumu, maswali yatafutiwe majibu kwa wakati. Lakini, what happened ktk tukio hilo..??

KWAMBA, tuamini kuwa yeye Dr Emmanuel Nchimbi na wenzake Rais na PM walikubaliana, na kumtuma mwenzao akaseme kuwa, kwa hoja ya katiba mpya nenda Waambieni "wasichoke kuipambania....?"

Tuendelee kutafakari na kujiuliza...

KWAMBA; How possible kuwa, kiongozi aongozaye kundi kwa kuwaonesha anaowaongoza njia ya kufuata ifike mahali awaambie, pambaneni kila mmoja atafute njia...?

Yaani una watu unawaongoza wewe kama namba mbili kwenye safu ya uongozi, unajua kuna njia salama ya kupita ili mtoke, badala ya kufungua mlango ili wewe na watu wako mpite, wewe unawaambia watu msiache kupambana mlango ufunguke....!!??

It doesn't make any sense, right...?

Hii Kauli ya jamaa imejaa unafiki wa mtego mbaya kwa wapambanaji wa katiba mpya. It's likely kuwa, huo mlango wanaoambiwa waupambanie ufunguke, basi mara ukifunguka, unaweza ukawa kumbe unawapeleka kutumbukia shimoni....🤔🤔🤔!!

All in all, ni kuwa kauli ya Dr Emmanuel Nchimbi inafikirisha sana kiasi kutupeleka kwenye hizi possibilities mbili;

1. Kwamba, kweli alikuwa anamaanisha kwa kuwa amewashauri wenzake ndani ya chama na serikali njia salama ya kupita na kufanikisha jambo hili, lakini hawamwelewi. Kisha uamuzi wake ukawa, mimi niko na wananchi, nitawaambia wapambane kuipata...

2. Kwamba, likely wamekubaliana huko, kuwa nenda kawafanye waendelee ku - buy time. Waambie waendelee kupambana hivyo hivyo na sisi huku tutaendelea na msimamo wetu, mwisho wa siku 2030 hiyo, na mwingine aingie labda yeye ndiye awape watakacho hawa viumbe...

♦️Inafikirisha ♦️​
 
Kwa ufupi;Nchimbi,aidha kajiweka pembeni na kuwa mtazamaji wa hayo mapambano au kajibakiza nyuma na kuwataka wanaotaka katiba waendelee mbele kujipambania kivyaovyao.Sasa huo sijui ni uongozi wa aina gani.Ni aidha anawalengesha wawe magaidi au anawasusia watajijua wenyewe.
 
Nyumbu naona mnahangaika sanaa kumbuka hata mama aliendaga kumchungulia Lissu Nairobi wakati wa JPM
 
Hawa watu wa ccm ni ngumu kuwaamini kipindi cha jpm samia alikua anajitia kama haelewi pigo za mwenzake lkn alipoingia yeye akapita mulemle hata kumzidi kwa hiyo ccm sio wazuri kwenye kupambania chama chao ni akheri afe mutu chama kibaki madarakani
 
Wewe unawaona mazafakas wa hiyo Serikali wako in lockstep? They aren’t. Moves zao nyingi hazisomani.

Nchimbi ana track record ya kuweka mguu chini pale mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo (tofauti na anavyoamini yanapaswa kufanyika). Unakumbuka kilichotokea 2015 JK alipocheza rough wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM cha kuchuja watia nia wa Urais kwa ticket ya CCM? Nchimbi alikuwa mmoja wa wajumbe watatu walioasi na kumtikisa JK vibaya. Bila Mzee Mkapa kuokoa jahazi, sijui nini kingetokea!
 
Jibu jepesi ni kwamba ndani ya ccm na serikali kwa ujumla kuna mgawanyiko mkubwa. Kuna baadhi ya makada hawafurahishwi na namna nchi inavyo endeshwa, namna uhasama baina ya wananchi, vyama, nk. unavyo ongezeka, nk.

Changamoto iliyopo hao watu hawana ujasiri wa kusimama hadharani na kukemea. Kwa sababu wanaju matokeo yake (refer ishu ya Mr. Slow slow!). Lakini kusema sijui anawachezea watu akili. Kwangu mimi siamini. Nadhani alimaanisha kile alichokisema.
 
Hawa watu wamebanwa mbavu Mkuu. Hawasiti kufanya maigizo yoyote ili kujinasua!
Kwenye kijani namwamini Mzee Warioba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…