Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

Unasema Yondani ana nidhamu ya khali ya juu! Dah
We unaonaje kwani, kama hana nidhamu si angepigwa red, zile ni mbinu za kuwatuliza washambuliaji au maadui wasumbufu, sawa na Marekani anavowawekea vikwazo vya kiuchumi Maadui wasumbufu, Unadhani hiyo ni adabu ya uchumi au hataki usumbufu??
 
Nakumbuka Alan Shealer aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya new Castle na timu ya Taifa uingereza.
Alikuwa ni mchezaji mwenye nidhamu sana.

Kuna siku alichezewa rafu alipoanguka akampiga teke la mdomo yule beki aliyemchezea rafu.
Hakuna aliyetarajia kitendo kile kingefanywa na Shealer.

Haya mambo katika soka hutokea
 
Kheri lawama kuliko fedhea

Safi sana Yondani tena ungemzaba kibao kabisa
Umekifikiria ulichokiandika lakini? ndio mana FIFA wanatoa ujumbe kuwa 'FOOTBALL is FAIR PLAY GAME'.
Kilichofanywa na Yondani kinastahili kupingwa na Wanamichezo wote kwa pamoja licha ya Usimba au Uyanga wetu. Unafikiri wachezaji 'wachanga' wanaomuona Yondani ni 'Role model' wao wanajifunza kitu gani?
Anachafua taswira yetu Kitaifa na Kimataifa kwa matukio yake ya 'Kipumbavu' kama lile la jana. Na of course sio mara yake ya kwanza kufanya hivi, Inabidi adhabu kali itolewe iwe fundisho kwake na kwa wengine.
Nawasilisha.
 
angekuwepo boban unafikiri angemfanyia kitendo hicho hawa wachezaji inabidi wapimwe kabla ya mechi ndio maana ni wa hapahapa timu gani inaweza kumchukua mchezaji kama yule
hata kadi nyekundu aliyopata kesy ni ya kijinga lakini utaona bado kuna watu wanamtetea
 
Nakumbuka Alan Shealer aliyewahi kuwa nahodha wa timu ya new Castle na timu ya Taifa uingereza.
Alikuwa ni mchezaji mwenye nidhamu sana.

Kuna siku alichezewa rafu alipoanguka akampiga teke la mdomo yule beki aliyemchezea rafu.
Hakuna aliyetarajia kitendo kile kingefanywa na Shealer.

Haya mambo katika soka hutokea
Nakubaliana na wewe, lakini kumbuka ushasema 'alikuwa mchezaji mwenye nidhamu sana', sasa turudi kwa huyu mchezaji wetu, je na yeye tusimuhukumu kwakuwa ana 'nidhamu' sana? La hasha, Kelvin ni kati ya wachezaji wenye nidhamu mbovu kupindukia na pasipo na shaka alifanya vile kwa makusudi na sio kwamba alishindwa kuzuia hasira zake.
Lakini je, kuna kitu gani kikubwa kilichopelekea afanye vile? Kwa marudio ya picha mnato wala hakukuwa na 'kujibizana' baina yao.
 
Kwanza mimi sio jamaa, ni mama.

Pili, baloteli kazaliwa ulaya unadhani atachezea wapi? Wachezaji wa kiafrika ndoto yao kubwa ni kuchezea ulaya, ndiyo maana nakuambia usifananishe ulaya na tanzania wenzetu wapo mbali sana.

Huko Ulaya ambako hata Yondani anatamani apate team achezee asitegemee kufika kwa nidhamu mbovu kiasi hicho.

Tafadhali ukinijibu tena nijibu na pointi.
Hana ubavu huo wa kukujibu kwa points
 
Hana tofauti na Nyosso..

Kamati ya maadili ya TFF ikae na kulitolea maelezo hili suala...
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Moja ya mchezo wenye changamoto nyingi sana hasa katika mchezo wa Soka ni mchezo wa "WATANI WA JADI" yaani Simba Vs Yanga.
Ni mchezo ambao unabeba hisia nyingi sana kwa wanamichezo kuanzia washabiki,wachezaji,makocha na wadau wote wa timu husika na timu mbalimbali shiriki.
Katika mchezo kuna matukio mengi sana ambayo machache yanaweza yakaonwa na mwamuzi na kuchukuliwa hatua na mengine mengi sana mwamuzi anaweza asiyaone na yakaonwa na watazamaji wengine hasa wa kwenye TV,hii ni kutokana na picha za marudio (Reply) zinazooneshwa.
Katika mchezo wa leo wa tarehe 29/04/2018 (Jumapili) ambapo timu ya Simba SC imeibuka na ushindi kuna matendo mengi sana yaliyotokea.
Moja ya kile kilichotokea ambacho kimenishawishi niandike haya ni mchezo/kitendo ambacho sio cha kiungwana kabisa (sio cha kimichezo) kilichofanywa na beki wa Yanga Kelvin Yondani kwa kumtemea mate mchezaji wa timu ya Simba.
Kiukweli ni moja ya kitu ambacho sio cha kiungwana kabisa kufanywa na mchezaji huyu hasa ukizingatia sifa ambayo Yondani amejijengea katika soka la Tanzania na hata nje ya nchi.
Ni kitendo ambacho labda mwamuzi hakukiona kabisa labda maana attention ya mpira ilikuwa ipo sehemu tofauti na kitendo hicho kilipotokea.
Ni wakati sasa wachezaji wazingatie michezo iliyo sahihi ili kufanya soka uwe mchezo wa kuburudisha kwa watazamaji wake.
Sheria ichukue mkondo wake dhidi ya vitendo kama hivi ambavyo si vya kiungwana vinavyotokea michezoni,TFF,inapaswa ichukue hatua kali sana ili iwe funzo kwa Yondani na wengine wote wenye tabia za aina hii.


Mwana_michezo
Kelvin ana Usela-mavi,
Niliona moja alitishia kama anataka kumkanyaga Kotei nadhani,
Mpira wa Mguuni kwa Kelvin umeisha umebaki mpira wa kihuni huni ambao huwezi kuuona Professional Leagues.
Ni mpira waliokua wakicheza miaka ile Ashant na Boom lakini sio kwa sasa,

Inawezekana ni technique aliitumia ili Jamaa apanic na kupewa red card lakini hii kitu hufanywa kama kuna timu ngeni kutoka mbali labda nchi za nje. Unamtemea mate mtu ambae baadae mnakutana mitaani mtaangalianaje sasa?
 
Kwanza mimi sio jamaa, ni mama.

Pili, baloteli kazaliwa ulaya unadhani atachezea wapi? Wachezaji wa kiafrika ndoto yao kubwa ni kuchezea ulaya, ndiyo maana nakuambia usifananishe ulaya na tanzania wenzetu wapo mbali sana.

Huko Ulaya ambako hata Yondani anatamani apate team achezee asitegemee kufika kwa nidhamu mbovu kiasi hicho.

Tafadhali ukinijibu tena nijibu na pointi.
kumbe shida yako upewe mifano ya walio zaliwa afrika na kuwa na tabia za utukutu na wakafika ulaya aya diofu na middle

kiwango ndo kitu cha muhimu, kumtemea mate mtu haiondoi nidhamu ya yondani aliyo kuwa nayo toka mwanzo.
 
aliumwa chelini sikio na suarez itakuwa kutemewa mate. ya nyoso mmeyasahau
 
Yondan ana utapiamlo wa akili! Jana alifikiria chini ya kiwango mpaka kufikia uamuzi wa hovyo kama ule! Kwa kuzingatia suala la nidhamu mchezoni na diplomasia nzuri iliyopo kati ya Tanzania na Ghana, tangu kuasisiwa mataifa haya mawili nafikiri yondan anakidhi vigezo vya kufungiwa angalau miezi sita na kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Kumtemea mate mwenzake na huo ubora vinahusiana vipi! Hakuna anayepinga ubora wake lakini kitendo alichofanya si cha kiungwana na kinapaswa kulaaniwa na wapenda michezo wote
Hana ubora. Alikuwa bora wakati anachezea simba ikiifunga yanga tano bila.
 
1.Yeye ndiye mtu mzee sana kupita wote katika mchezo wa leo na yawezekana kwa wachezaji wote Tanzania

2.Alitakiwa awe ndio kiongozi wa busara na kwarekebisha wadogo zake wanapofanya kosa

3. Najua kwa nidhamu ile mbovu hatarajii chochote kwenye maendeleo yake ya kisoka ukijumlisha na umri wake

4. Amefanja jambo ambalo sii baya tu kwa clabu yake lakini hata kidiplomasia sii zuri kwa dharai ile aliyoionyesha kwa mchezaji wa TAIFA la kigeni ambaye hakumkosea chochote na hata baada ya kitendo kile yule mchezaji hakumjibu kwa ubaya zaidi alikwenda kumstaki kwa refa.

5. Haya mambo ni ya kizamani sana ambapo sikutarajia nilichokiona leo kwa karnr hii ambayo soka limeshaa toka kwenye uhasama na kubaki ni taaluma inayoongozwa na " FAIR PLAY" concept

6. Huyu mchezaji afutwe kabisa kwenye suala la uchezaji akafanye kazi nyingine hata za kusukuma toroli maana kwa kitendo kile anaonekana hana proffession nyingine zaidi ya mpira ambao sasa unaisha kutokana na umri ndio maana anafanya vitu vya ajabu

Wewe sijui umetokea wapi, Kelvin sio wa kwanza kufanya hivyo na uwanjani huwa kuna matukio mengi ya ajabu zaidi ya hilo.

Shida yenu mumejaa umbea mno.
 
angekuwepo boban unafikiri angemfanyia kitendo hicho hawa wachezaji inabidi wapimwe kabla ya mechi ndio maana ni wa hapahapa timu gani inaweza kumchukua mchezaji kama yule
hata kadi nyekundu aliyopata kesy ni ya kijinga lakini utaona bado kuna watu wanamtetea

Kadi nyekundu zisizo za kijinga huwa zinakuwaje ?
 
We nae mpira ulicheza wapi? Hukuona huyo kwasi alichomfanyia Yondani mpaka kureact vile? Acheni viherehere kudandia mambo msiyo yajua...wengine nyie ni wajuzi wa kulala chali and nothing else.
Ukinikashifu kuwa mimi ni mjuzi wa kulala chali sababu tu ni mwanamke...jua hata mama yako ni mwanamke ninachokifanya na yeye anakifanya so kabla ya kumkashifu mtu jifikirie kwanza.

Anyway sitokujibu kwa kashfa kama ulivyofanya.
 
mi hilo tukio nilienda Mechi ikiwa iko mbali sana, Yondani hakoseagi ndio maana katoka hana kadi hata moja. Hii inadhihirisha Ana nidhamu ya hali ya juu sana.

Yanga wakimuuza au kumtema wasitegemee kupata mwingine maana Hamna beki tena wa kiwango kile

Yule alikuwa anatafuta namna ya kutolewa aidha kwa kadi nyekundu au kujifanya kaumia. Angalia kuna wakati alianguka anaomba atolewe.
Kelvin ni mchezaji/beki mzuri kwa talent lakini apparently ana shida kwenye mindset. Akiwa challenged mara mbili tatu anapoteza mwelekeo. Yuko juu kwa talent kuliko kanavaro, lakini mind set ya Kanavaro ni ya juu kuliko yeye. Yanga wamemlea vizuri amedumu kiasi cha kupata unahodha, ajitahidi asijiharibie kabla ya kustaafu kwa heshima.
 
Back
Top Bottom