mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kulikuwa na kisa kimoja kuwa mama mmoja alikuwa na watoto watatu. Kati ya hao wawili ni watoto wa kambo na mmoja ni WA kwake. Huyu mama alinunua machungwa mawili huku akitaka mtoto wake apate chungwa Zima lakini wale wa kambo wagawane chungwa moja nusu kwa nusu!!
Ili kuwadanganya Hawa watoto wa kambo aliwagawia Kila mmoja chungwa moja na yule wa kwake akakosa!! Halafu akawaambia Hawa wa kambo kuwa Kila mmoja amgawie "kidogo' huyu aliyekosa!! Hawa watoto wakafurahi kuwa wao wamepata chungwa Zima halafu wanamgawia huyu mwenzao "kidogo" tu kwa hiyo wakakubali!!
Yule mama akawaambia niwasaidie kumkatia huyu mwenzenu kidogo na wakakubali. Mama akakata nusu ya Kila chungwa na kumgawia mtoto wake!!
Mwisho wa siku mtoto wake alipata chungwa Zima na hawa watoto wa kambo wakafurahi kuwa wao walipewa chungwa Zima na wakamgawia mwenzao "kidogo" tu maana hawajui kuwa nusu Mara mbili ni chungwa Zima!!
Hicho ndicho alichokifanya Putin, iko hivi:
Urusi aliwekewa vikwazo na mabeberu, moja ya kikwazo ni kwamba haruhusiwi kufanya miamala yoyote kwa kutumia Dola au Euro!!
Kwa maneno mengine ni kuwa Dola na Euro alizokuwa nazo zilikosa kabisa thamani maana Hana jinsi ya kuzitumia. Ndio maana Putin alisema kuuza gesi yake kwa Dola ni sawa na kuuza bure maana hiyo Dola Haina faida kwake.
Putin akasema kuanzia tarehe 31/03/2022 atauza gesi na mafuta kwa Rouble!! Na akasema hakuna gesi na mafuta ya bure! Ukitaka mafuta na gesi ya Urusi tafuta Rouble! Mabeberu wakagoma kabisa kununua kwa Rouble!!
Ilipofika tarehe 30/03/2022 yaani siku moja kabla ya utekelezaji kansela wa Ujerumani akaamua kuongea moja kwa moja na Putin kuhusu jambo Hilo. Hapo ndipo Putin alipomchezea mchezo wa kitoto!! Akamwambia hivi, kwa Sasa hatukubali kuuza mafuta na gesi kwa Dola au Euro!
Nenda ukanunue Rouble halafu Uje ulipie!! Ukiona kwako ni shida kwenda kununua Rouble, tupe sisi hiyo Dola halafu TUTAITUMIA HIYO DOLA KUNUNUA ROUBLE, KWA HIYO WEWE UTAONA UMENUNUA KWA DOLA! KWA MANENO MENGINE MTURUHUSU SISI KUTUMIA HIYO DOLA KUNUNULIA ROUBLE!! (Kumbuka kwa mujibu wa vikwazo Urusi hairuhusiwi kufanya miamala kwa Dola au Euro, kwa hiyo ukikubali pendekezo la Putin ni kwamba unafuta kikwazo Cha awali Ili upate gesi na mafuta). Kwa maneno mengine Kuna vitu viwili Putin amevipataa kwa pamoja:
1. Amewalazimisha mabeberu wakubali Urusi kufanya miamala kwa kutumia Dola kununua Rouble! Kwa hiyo kikwazo Cha kufanya miamala kwa Dola kinakuwa kimekufa kifo Cha Mende asubuhi na mapema
2. Urusi imetimiza lengo lake la kuuza gesi na mafuta kwa Rouble maana Mara beberu anaponunua kwa Dola au Euro, Urusi inaibalilisha hiyo Dola kuwa Rouble!!
Hivyo Urusi kufanikiwa kuhifadhi utajiri wake kwa fedha ya ndani ambayo hakuna mwingine mwenye mamlaka nayo!!
Mwisho wa siku ni kwamba Mabeberu wamenunua kwa Rouble kwa njia ya mzunguko Kama ambavyo yule mama alivyompa mtoto wake chungwa Zima kwa njia ya mzunguko!
Vinginevyo wangesema hatukubali kununua kwa Rouble, tutaendelea kununua kwa Dola, na wewe huruhusiwi kufanya miamala kwa Dola!!
Kwa hiyo hizo Dola tunazokulipa huwezi kuzitumia kwenye miamala yoyote! Lakini mjerumani alinywea akasema SAWA!!