Kuhusu kununua gesi na mafuta kwa Rouble: Putin awafanya mabeberu Kama watoto wadogo

Kuhusu kununua gesi na mafuta kwa Rouble: Putin awafanya mabeberu Kama watoto wadogo

Nakushukuru Sana kwa kulifafanua jambo hili kwa maelezo ya kueleweka Sana!! Mwisho wa siku mauzo ya gesi na mafuta yataingiza Rouble kwenye akiba ya Urusi na Siyo Dola!

Mbona umekomaa na dola na sio Euro.
Ongelea euro ndo inahisika hapa.
 
Wote wataipata, urussi mapato yake makubwa yanatokana na gesi na mafuta na mteja wake Mkubwa ni ulaya

Na ulaya atapata shida lakin huwezi mtuhumu ulaya ata loose huku ukimsifia urussi huo ni ushabiki na sio uhalisia

We kua na duka alafu wateja wasije alafu jidandanye unawakomoa wateja baada ya mda hata wewe utakuja gundua unapata hasara

Usiponunua utaishije? Usafiri/gari inahitaji mafuta/gesi, kupikwa vyakula vinahitaji gesi. Sasa nani anajikomoa hapo!! Na hapo hapo india atanunua kwake, na india ina population kubwa kuizidi ulaya yote.
 
Unaelewa unachoelezwa lakini? Hakuna sehemu urusi amekataa kuuza gesi. Ameweka masharti ya jinsi ya kununua gesi yake kua ni rouble, Ulaya wamekataa kununua kwa rouble wamesema mkataba hausemi hivyo, na wala hawajui sehemu ya kuipata hizo roubles.
Sasa urusi kawaambia sawa, nunueni kwa euro au dollar kisha mimi nitazibadilisha kua rubles. Yaani anaenda benki kulipia gesi kwa euro pale benk wanazigeuza kwa Russian ruble. Ni sawa na kufanya kitu kile kile.

Na ulaya wameanza kukubali hilo jambo na jana chancellor wa Germany ameongea na Putin.
Hizo habari mnazitoa wapi mbona RT news hii habari haipo?

Soma habari kutoka katk website yao hamna hiyo habari.
 
Hizo habari mnazitoa wapi mbona RT news hii habari haipo?

Soma habari kutoka katk website yao hamna hiyo habari.
hivi umesoma taarifa ya maongezi ya kansela wa ujerumani na rais Putin yaliyofanyika jana tarehe 30/03/2022, yaani siku moja kabla ya deadline iliyowekwa na urusi? Itafute taarifa hiyo halafu urudi hapa. Inaelekea uko nyuma sana ya wakati!
 
hivi umesoma taarifa ya maongezi ya kansela wa ujerumani na rais Putin yaliyofanyika jana tarehe 30/03/2022, yaani siku moja kabla ya deadline iliyowekwa na urusi? Itafute taarifa hiyo halafu urudi hapa. Inaelekea uko nyuma sana ya wakati!
RT pamoja na kufungiwa na nchi za Magharibi, ila ndio source ya uhakika kwa habari za russia,nimeingia kwenye website yao hamna hiyo habari.
 
Marekani keshabwaga manyanga tayari asubuhi na mapema baada ya kuona baadhi ya vikwazo ilivyoiwekea urusi vinawaumiza wamarekani zaidi. Amua kuviondoa hivyo vikiwemo ununuzi wa mbolea, vyakula nk kutoka Urusi!!
Nashangaa nchi za ulaya hazishtuki tu, wanamwona marekani akiachana na vikwazo vinavyoiumiza huku ikizishinikiza nchi za ulaya ziachane na gesi rahisi ya urusi halafu ziumie na gesi ya bei kubwa toka marekani!! Wazungu wa ulaya inabidi wapimwe akili! Ona marekani ilivyoachana na vikwazo kwa Urusi vinavyoiumiza yenyewe zaidi!

US exempts critical Russian commodity from sanctions​

Washington aims to protect farmers from fertilizer shortages
US exempts critical Russian commodity from sanctions

© Getty Images / Westend61
Washington has eased sanctions on Russian agricultural products, including fertilizers, placed on Moscow over the crisis in Ukraine. The move aims to protect US farmers from a shortage of chemical products as food prices in the country continue to soar.
The Office of Foreign Assets Control (OFAC) of the US Treasury recently published a new general license dated March 24, which effectively removed restrictions on the import of Russian fertilizers.
The document authorized transactions relating to the exportation and re-exportation of agricultural commodities, banned last month by Washington’s ‘Russian Harmful Foreign Activities Sanctions Regulations’.
The list of agro-related products now exempt from sanctions includes food for humans, live animals, vitamins and minerals, food additives and supplements, seeds for food crops, fertilizers, and reproductive materials.
Exemptions also cover medicine, medical devices, software updates, and replacement parts for medical devices and Covid-19-related medical components. Analysts say the EU may soon mirror the measure.

Kwa kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, japo wengine wna upaa!
 
Kwani gesi na mafuta urussi anawapa bure ulaya anawauzia kwa hiyo ulaya kugoma kunamfanya urussi naye ku-loose sababu mapato asilimia 30 ya Russia yanatokana na kuuza gesi na mafuta, kwa hiyo ni hasara kwa pande zote
5% tu ya GDP ya Russia ndio inategemea Export ya Mafuta na Gas.
Wakati, Nchi za Ulaya zinategemea 40% ya Gas na Mafuta ya Russia.

Pia kuna mataifa Mengi ya Asia, ambayo kwa sasa, ndio Economic zone ya Dunia, wapo willing kupata Gas na Mafuta ya Russia itakapo patikana nafasi.

So unaona big loser ni nani hapa,Ulaya.


Kutaka Mafuta,Mbolea na Gas yake zinunuliwe na pesa yake, ni kuwataka Ulaya ku pandisha thamani ya pesa wanayo fanya juu chini kuishusha
 
Kulikuwa na kisa kimoja kuwa mama mmoja alikuwa na watoto watatu. Kati ya hao wawili ni watoto wa kambo na mmoja ni WA kwake. Huyu mama alinunua machungwa mawili huku akitaka mtoto wake apate chungwa Zima lakini wale wa kambo wagawane chungwa moja nusu kwa nusu!!

Ili kuwadanganya Hawa watoto wa kambo aliwagawia Kila mmoja chungwa moja na yule wa kwake akakosa!! Halafu akawaambia Hawa wa kambo kuwa Kila mmoja amgawie "kidogo' huyu aliyekosa!! Hawa watoto wakafurahi kuwa wao wamepata chungwa Zima halafu wanamgawia huyu mwenzao "kidogo" tu kwa hiyo wakakubali!!

Yule mama akawaambia niwasaidie kumkatia huyu mwenzenu kidogo na wakakubali. Mama akakata nusu ya Kila chungwa na kumgawia mtoto wake!!

Mwisho wa siku mtoto wake alipata chungwa Zima na hawa watoto wa kambo wakafurahi kuwa wao walipewa chungwa Zima na wakamgawia mwenzao "kidogo" tu maana hawajui kuwa nusu Mara mbili ni chungwa Zima!!

Hicho ndicho alichokifanya Putin, iko hivi:

Urusi aliwekewa vikwazo na mabeberu, moja ya kikwazo ni kwamba haruhusiwi kufanya miamala yoyote kwa kutumia Dola au Euro!!

Kwa maneno mengine ni kuwa Dola na Euro alizokuwa nazo zilikosa kabisa thamani maana Hana jinsi ya kuzitumia. Ndio maana Putin alisema kuuza gesi yake kwa Dola ni sawa na kuuza bure maana hiyo Dola Haina faida kwake.

Putin akasema kuanzia tarehe 31/03/2022 atauza gesi na mafuta kwa Rouble!! Na akasema hakuna gesi na mafuta ya bure! Ukitaka mafuta na gesi ya Urusi tafuta Rouble! Mabeberu wakagoma kabisa kununua kwa Rouble!!

Ilipofika tarehe 30/03/2022 yaani siku moja kabla ya utekelezaji kansela wa Ujerumani akaamua kuongea moja kwa moja na Putin kuhusu jambo Hilo. Hapo ndipo Putin alipomchezea mchezo wa kitoto!! Akamwambia hivi, kwa Sasa hatukubali kuuza mafuta na gesi kwa Dola au Euro!

Nenda ukanunue Rouble halafu Uje ulipie!! Ukiona kwako ni shida kwenda kununua Rouble, tupe sisi hiyo Dola halafu TUTAITUMIA HIYO DOLA KUNUNUA ROUBLE, KWA HIYO WEWE UTAONA UMENUNUA KWA DOLA! KWA MANENO MENGINE MTURUHUSU SISI KUTUMIA HIYO DOLA KUNUNULIA ROUBLE!! (Kumbuka kwa mujibu wa vikwazo Urusi hairuhusiwi kufanya miamala kwa Dola au Euro, kwa hiyo ukikubali pendekezo la Putin ni kwamba unafuta kikwazo Cha awali Ili upate gesi na mafuta). Kwa maneno mengine Kuna vitu viwili Putin amevipataa kwa pamoja:

1. Amewalazimisha mabeberu wakubali Urusi kufanya miamala kwa kutumia Dola kununua Rouble! Kwa hiyo kikwazo Cha kufanya miamala kwa Dola kinakuwa kimekufa kifo Cha Mende asubuhi na mapema

2. Urusi imetimiza lengo lake la kuuza gesi na mafuta kwa Rouble maana Mara beberu anaponunua kwa Dola au Euro, Urusi inaibalilisha hiyo Dola kuwa Rouble!!

Hivyo Urusi kufanikiwa kuhifadhi utajiri wake kwa fedha ya ndani ambayo hakuna mwingine mwenye mamlaka nayo!!
Mwisho wa siku ni kwamba Mabeberu wamenunua kwa Rouble kwa njia ya mzunguko Kama ambavyo yule mama alivyompa mtoto wake chungwa Zima kwa njia ya mzunguko!

Vinginevyo wangesema hatukubali kununua kwa Rouble, tutaendelea kununua kwa Dola, na wewe huruhusiwi kufanya miamala kwa Dola!!

Kwa hiyo hizo Dola tunazokulipa huwezi kuzitumia kwenye miamala yoyote! Lakini mjerumani alinywea akasema SAWA!!
Kinachofuata atawaambia waziachie Mali zote Russia wanazozishikilia otherwise hauzi mafuta
 
Wote wataipata, urussi mapato yake makubwa yanatokana na gesi na mafuta na mteja wake Mkubwa ni ulaya

Na ulaya atapata shida lakin huwezi mtuhumu ulaya ata loose huku ukimsifia urussi huo ni ushabiki na sio uhalisia

We kua na duka alafu wateja wasije alafu jidandanye unawakomoa wateja baada ya mda hata wewe utakuja gundua unapata hasara
Ni HALALI 100% kumsifia URUSI na tafadhali usione wivu wala chuki! Wao walitaka wamuue Urusi kifo cha mende! Walitaka atoke 3-0!!! hata kama kalazimisha 0-0 kama unavyodai wewe huoni kama ameshinda? Malengo yao katika hilo yameshindwa, kwa kifupi wameshindwa!
 
Mikataba inasema ulaya atamlipa urussi kwa dollar au euro ikinunua gesi na mafuta hizo narrative Zako unazitolea wapi
Kwamba wajerumani hawajui mikataba inasemaje?
Au kwenye hiyo mikataba kuna kipengele cha kufanya biashara kwa dola halafu upande mmoja uwe na uwezo wa kumuwekea muuzaji vikwazo kwenye matumizi ya dola!?
Kubali tu kuwa,wamagharibi hapa walichemka. Walifikiri kwakutumia masaburi

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
tofauti urusi atabaki na mafuta na gesi yake huku wengine wakifunga viwanda, kupunguza wafanyakazi na kuongeza mfumuko wa bei
Kwahiyo Russia hatakuwa na cha kupoteza kwa kukosa mapato ya gas? Yeye maisha yake yataendelea kuwa vilevile?
 
Back
Top Bottom