Kuhusu kuuawa Hayati Mzee Ali Kibao, Mwandishi nguli wa Habari za Uchunguzi Bollen Ngetti ameandika haya, inafikirisha!

Amendika ujinga wa hali ya juu. Sativa alitaka kuuawa, alikuwa na uhalifu gani? Haya, hata kama ni uhalifu, kwa nini wasichukuliwa hatua?
Mbona maswali yako ndio maswali ya mwandishi? Japo kwa muonekano tofauti but same mantiki.

Hujasoma mwandishi alipouliza kwanini marehemu akauwawa badala ya kupelekwa mahakamani?!

Hii yote ni kutaka sheria ifuate mkondo wake, kama utakavyo wewe unapouliza kwanini wasichukuliwe hatua!.

Halafu mwandishi kwenye andiko lake lote hajazungumzia suala la Sativa, kamzungumzia Marehemu Kibao.

Hili tatizo lenu la kuchanganya mambo ndilo linawafanya mumuone mbaya, bado hamjaweza kuhukumu kitu kulingana na kinavyokuja mbele yenu, wengine mnaishia kuhukumu historia ya mwandishi, wengine ndio mnachaganya yasiyokuwepo ilimradi tu iwe vurugu.
 
Upumbavu mtupu. Alipouawa Mwangosi mwandishi wa habari wa channel ten si ni polisi ndio walisema CDM ndio waliohusika lakini baadae zikasambaa picha kumuonesha polisi akimfyetulia kilipukizi Mwangosi.

Watanzania sio wajinga tena. Na hata sakata la mzee Kibao ni serikali imejifanya kushtuka kwa sababu wananchi wameshagundua jambo.
 
Hizo ni ‘circumstantial accusations’ tu kwenye case ushahidi wa aina hii auna merit peke yake. .

Halikadhalika mpaka sasa polisi wana strong lead kwenye hii case pakuanzia, person of interests na ushahidi mwingine (should they read careful, hata mada za JF tu).

Huko sasa ni dangerous territory ambazo sisi wa huku Bugurani kwa mnyamani atutaki kujihusu. Iła kuna loopholes nyingi sana za wahalifu kuweza ku-crack hii case.
 
Naona Bollen ameandika mambo ya msingi sana ajabu wachangiaji hapo juu wanamlaumu, kuna tatizo kubwa la upeo wa kuchambua mambo humu ndani.

Hayo maswali ya Bollen yanahitaji majibu, ajabu mnamnyooshea vidole!.

Mmegeuka watetezi wa jeshi la polisi kwa ujinga wenu, upeo wenu finyu.
Uko sahihi kachambua kitaalamu kuna humu zilikuja nyuzi zilifutwa zillandika kuhusu ugaidi uliokuwa unapangwa kuanzia kwenye zoom na Tanga huko kwa kushirikisha wasomali alshababu na wakatajwa viongozi wa Chadema kwa majina waliohudhiria hivyo vikao huko na kueleza kuwa athari zingekuwa mbaya kwa nchi

Vizuri kujadili. Mada kwa utulivu
 
Hizo ni ‘circumstantial accusations’ tu kwenye case hazina ushahidi.

Halikadhalika mpaka sasa polisi wana strong lead kwenye hii case pakuanzia, person of interests na ushahidi mwingine.

Huko sasa ni dangerous territory ambazo sisi wa huku Bugurani kwa mnyamani atutaki kujihusu. Iła kuna loopholes nyingi sana za wahalifu kuweza ku-crack hii case.
Unaandika polisi wana "strong lead" ipi hiyo?

- Polisi waliotutangazia kuna watuhumiwa lakini wakashindwa kuwakamata?

- Polisi wanaoachia vyombo vingine vitekeleze majukumu yao, sasa kwa hili tukio jukumu la jeshi la polisi ni lipi kama wanashindwa kumkamata hata mhalifu wanayemdhania asiyekuwa na silaha yoyote?

Polisi hawana mlango wa kutokea kwenye hii kesi, walitumiwa na wasiojulikana kutangaza mbinu walizoita ovu za Chadema, ili baadae waache wasiojulikana wafanye ukatili wao kwa marehemu, polisi wetu wanatumika vibaya na wahuni.
 
Nasemaje!
Mkakojoe mlale maana naona hamjamwelewa mwandishi kiundani then mkikurupuka mtaendelea kupiga domo, are we together?
 
Unaandika polisi wana "strong lead" ipi hiyo?

- Polisi waliotutangazia kuna watuhumiwa lakini wakashindwa kuwakamata?

- Polisi wanaoachia vyombo vingine vitekeleze majukumu yao, sasa kwa hili tukio jukumu la jeshi la polisi ni lipi kama wanashindwa kumkamata hata mhalifu wanayemdhania asiyekuwa na silaha yoyote?

Polisi hawana mlango wa kutokea kwenye hii kesi, walitumiwa na wasiojulikana kutangaza mbinu walizoita ovu za Chadema, ili baadae waache wasiojulikana wafanye ukatili wao kwa marehemu, polisi wetu wanatumika vibaya na wahuni.
Endelea kujiongopewa queries kadhaa kwa watu waliokuwa open minded kwenye hii case zimepata majibu kwa upande kwangu (tena kwa kupitia mada za JF tu).

Kama nilivyosema hiyo ni dangerous territory ambayo binafsi siwezi kujihusisha tena, be it baadhi ya hizo queries nilishawahi andika humu siku mwili ulipopatikana na majibu nimeyapata humu humu.

Jamaa hawapo makini kabisa (accomplices), sasa ni polisi kufanya kazi yao.

Hayo mengine ni baseless accusations żako tu.
 
C&P from Face Book.

KUTEKWA, KUTESWA, KUUAWA KWA ALLY KIBAO, TUSAIDIANE KUTAFAKARI

Na Bollen Ngetti

SOMA lakini kwa tafakuri pana labda tukajua ukweli walau kidogo si wote katika giza hili lililofunika kutekwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kikatili Mzee Ally Muhammed Kibao al-maarufu MeD.

Niharakishe kusema ukweli kwamba hakuna uhusiano mzuri baina na kati ya CCM na Chadema kimkakati, kisiasa na hata kimtazamo na kimaadili. Niharakishe pia kusema kama ilivyo kwa vyama vyote kongwe ni hayawani pekee anayeweza kutenganisha chama-tawala na dola. Kwamba dola inaishi kwa hisani ya chama-tawala na kwa mantiki hiyo dola ina wajibu mkubwa wa kukilinda chama kwa gharama yoyote.

Sasa twende. Siku za karibuni Jeshi la Polisi lilitoa taadhari kwa umma mpana kwamba lina taarifa za kijasusi zisizo na chembe ya shaka kwamba Chadema inapanga makundi ya vijana yapatayo 20 ambayo yatavamia vituo vya polisi jijini Dar es salaam kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Polisi intelijensia ilionesha kikao kilichokuja na uamuzi huo mgumu ulifanyika kupitia mtandao wa ZOOM. Hata hivyo Polisi haikusema lengo la kuvamia vituo hivyo ni nini hasa? Kuvichoma moto? Kuwapiga Polisi? Kuwafungulia huru maabusu? Kukwapua silaha? Kwenda kuvitumia wapi? Endelea kutafakari.

SASA tujiulize haya maswali ya msingi. Hakuna mtu wa kawaida mwenye uwezo wa kuvamia kituo cha polisi akijua fika ni eneo salama iliyosheheni silaha za kivita. Mtu huyo anaweza tu kama naye ana mafunzo mahsusi ya masuala hayo ama ni jambazi mzoefu. (Rejea kuvamiwa kwa kituo cha Polisi Stakishari Ukonga).

Tembea na neno "taarifa zisizo na SHAKA" kichwani.

Hii maana yake ni kwamba wavamizi watarajiwa wa vituo vya polisi kutoka Chadema wana uwezo, mafunzo, ujasiri juu ya maswala ya usalama na kwa mantiki hiyo wasingekwenda kujaribu bali kutekeleza. Swali lingine linanijia kichwani maana taarifa ya Polisi ina ukweli "usio na shaka". Kwamba vijana hawa wa Chadema wamepata mafunzo hayo wapi na lini? Maana si majambazi kwa mujibu wa Polisi.

Vyuo vya usalama nchini vinajulikana kuanzia Polisi, Magereza, TISS, JWTZ. Wao wamepata mafunzo wapi? Chadema ina chuo cha mafunzo ya silaha kiasi cha kuvamia vituo vya Polisi kulikosheheni bunduki za kila aina?

Kama hawa chuo kama hicho ndani au nje ya nchi, basi tujiulize kusumbua bongo zetu. Nani aliwapa mafunzo wakaiva na hivyo kuwa na uwezo, ujuzi na ujasiri wa kuvamia vituo vya polisi ? Kwani Red Brigade wanafunzwa kuvamia vituo vya Polisi? Usichoke kutafakari....

SASA, moja ya sifa tuliyoambiwa Marehemu Ally Kibao anayo ni kwamba ni Mwanajeshi mstaafu aliyefika katiko vyeo vya juu si kabisa. Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretariat ya Chadema lakini pia tunaambiwa kuwa ndiye alikuwa ni "strategist" wa chama na ndio hakufahamika sana majukwaani maana alikuwa "nyuma ya kamera ".

Sijui viapo vya JWTZ vinasemaje ila Kibao baada ya kustaafu alijiunga na CCM na kuwa Mwenezi Mkoa wa Tanga na baadaye kutimkia Chadema hadi alipotekwa, kuteswa., kuuawa na mwili wake kutupwa vichakani huko Ununio (Dar es salaam).

Swali fikirishi! Je, ni huyu (Kibao), strategist, JWTZ mstaafu ndiye aliwapika vijana wa kuvamia vituo vya Polisi? Je, uratibu huu ulikuwa ukiendelea na tuseme Polisi waliamua kujihami kabla ya uvamizi kwa usemi, "mpige mchungaji na kondoo wote watatawanyika"? Haya yote ni kuwaza maana ripoti ya uchunguzi juu ya waliomuua Kibao ni kina nani hasa licha ya alama zote kuonesha ni watu wenye kumiliki pingu ama wa ndani au nje ya nchi. Yote yawezekana.

Je, polisi iko katika operesheni maalum kuzuia wavamizi kabla ya kuvamiwa? Swali linalogonga vichwa ni kwamba kama taarifa za kijasusi zilionesha kuwa MeD ndiye alikuwa "chuo" cha kuwaandaa wavamizi ndiyo auawe badala ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Sina jibu....wauaji wana majibu.

Nawaacha na swali hili! Kwa tusiamini kuwa nyuma ya vitendo vya utekaji Chadema haiko nyuma yake kisiasa? Kwa nini hutaki kuamini na kwa nini uamini. Nawatakia tafakuri njema na jadidi. Alamsiki.

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Kuna vijana kadhaa wa uvccm wapo kwenye kambi kadhaa za JWTZ wakipewa mafunzo maalumu.
Tuendako ni hatari!
 
Huyu muandishi amehitimu chuo cha lumumba pale kwenye ukijani.
 
Endelea kujiongopewa queries kadhaa kwa mtu aliekuwa open minded kwenye hii case zimepata kwangu.

Kama nilivyosema hiyo ni territory ambayo binafsi kujihusisha tena, be it baadhi ya hizo queries nilishawahi andika humu siku mwili ulipopatikana.

Jamaa hawapo makini kabisa (accomplices), sasa ni polisi kufanya kazi yao.

Hayo mengine ni baseless accusations żako tu.
Una tatizo upstairs.

Polisi wanatuambia Chadema wana mpango wa kuvamia vituo vya polisi Dsm, kwanini wasiwakamate wahusika wa huo mpango kama kweli ulikuwepo ili wawapeleke mahakamani?

Badala yake polisi baada ya kututangazia uwepo wa huo mpango, wasiojulikana wanamkamata marehemu wanampiga mpaka kumuua, hivyo ndivyo sheria zetu zinavyoagiza?!

Unatumia maneno "baseless accusations" sijui hiyo sheria yako umejifunzia wapi wewe kama hata a.b.c za sheria zetu huzijui.

Hujawahi kusikia polisi wakisema "watuhumiwa/mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika" why kwa marehemu haikuwa hivyo?

Uko empty, hujui kitu.
 
CONCEPT ya kuuawa kwa MED mwandishi ameiweka wazi. CHADEMA msituharibie amai ya nchi kwa uchu wa Madaraka. Vyombo vya usalama ongezeni nguvu. Hilo liwe fundisho kwa VIONGOZI WA CHADEMA.
 
Bora mzee wako angeenda tu washroom hata na lotion ya nivea akazipunguze kisha aflash . Pengine ingesaidia sana kupunguza humanoid specie aina yako.
 
..naona kama muandishi Bollen Ngeti anajenga hoja ya kuhalalisha mauaji ya Mzee Ally Kibao.

..Huyu bwana hata kama aliwahi kuwa mwanajeshi, na alikuwa walipanga njama dhidi ya Polisi, bado hakustahili kuuwawa na kutobolewa macho.

..Na hapa sizungumzi juu juu tu. Tunaweza kurudia matukio ya ukamataji wa WAHAINI ya mwaka 1983.

..Yuko komando Captain Mussa Tamim aliuwawa wakati wa ukamataji. Tamim alikuwa askari, mtu wa Tanga, ambaye alituhumiwa kutoroka jeshini. Wengine wanadai hakutoroka alitumwa kwenda kumlinda Rais Yussuf Lule wa Uganda.

..Tamim aliuwawa na maofisa usalama waliotumwa kumkamata kwa tuhuma za kupanga njama kupindua serikali. Lakini uhalali wa kumuua ulitokana na ukweli kwamba Tamim alikataa kukamatwa, na aliwashambulia maofisa waliotumwa kumkamata.

..Tukirudi kwenye tukio la Ally Kibao, yeye hakugoma kukamatwa. Pia hakushambulia waliomkamata. Sasa imekuwaje akauwawa? Pia kwanini amwagiwe tindikali? Kwanini atobolewe macho?

..Nimewarudisha kwenye historia ili muelewe UJINGA wa baadhi ya waandishi watetezi wa CCM kama Bollen Ngeti.

Na ndicho nilichokuwa nakiwaza, kwamba Kwa madai ya polisi, walikua na taarifa za uhakika pasi shaka kuhusu uvamizi wa vituo kadhaa.
Nilitegemea hiyo iwe hatua ya muhimu na awali kabisa kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya Sheria Kwa taratibu zilizopo.

Hii inazua maswali mengi kuhusu weledi na umahiri wa jeshi letu kwenye utendaji kazi wake. Pelekezi na tuhuma mbali mbali wanazikabili kwa mwenendo wa aina hii?

Kwa namna Moja, kama ni kweli madai ya polisi walikua na hizo taarifa zisizoshaka, hii ilikua ni njia rahisi na nyepesi kabisa ya kuimaliza CDM Kwa taratibu za kisheria.
 
Usahihi na lengo la taarifa yoyote ni muhimu sana kwenye taasisi yoyote.
Bingwa wa upasuaji aweza kumpasua mgonjwa kichwa badala ya mguu kutokana na taarifa na vipimo visivyo sahihi kutoka kwa wasaidizi wasio na weledi au wanaotunga na kuandika uongo kwa malengo yao au ujinga tu.
Ukweli au usahihi huweka watu huru Ila uongo una gharama ya kuulinda au kuuhalalisha kwa muda (temporary), ambazo matokeo ni madhara na kuongeza uongo unaoharibu zaidi.
 
Nipo kila sehemu coz kichwa changu kinaniruhusu.

▪ Niliyeropoka mimi au polisi waliotuambia Chadema wana mpango wa kuvamia vituo vya polisi?

▪ Kama polisi hawakuwa na ushahidi wa hilo, kwanini wakaropoka Chadema wana mpango wa kuvamia vituo vya polisi?

Ok, waliropoka ili kuwapa wasiojulikana nafasi ya kufanya uhuni wao ķwasababu walijua hawana ushahidi wa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa.

Unatoa argument za kijinga sana kulazimisha kuwalinda polisi na uhuni wao, wakati kimsingi hawakwepi lawama kwenye kifo cha marehemu Kibao.

Sijui umesoma sheria sayari gani wewe!.
Upo kila sehemu kwa sababu kichwa chako kinaishi lala/land and you think that’s how actually the world as in your little pathetic head.

Kazi ya polisi pia ni kuzuia uhalifu kabla aujatokea. Unataka wasubiri mpaka madhara yatokee ndio wachukue hatua. Kuna wasaa kama hawajui siku wala saa ya tukio busara ni kuonya watu waache.

Sasa utakwenda kuwakamata watu bila ya strong evidence (hata kama una intelligence mipango yao). Utakwenda kuwashitaki mahakamani kwa ushahidi gani uliojitosheleza. Ndio msingi wa kukuuliza unafahamu conditions ‘actus reus na mens rea’ kwenye criminal case zote hizo lazima uthibitishe.

Sikiliza unaweza endelea ugomvi na wengine misikuingia kwenye hii mada kwa malengo ya kulumbana hasa mambo ya kijinga unayofikiria kichwani thinking that’s how actual the world works.
 
Upo kila sehemu kwa sababu kichwa chako kinaishi lala land and you think that’s how the world as in your little pathetic head.

Kazi ya polisi pia ni kuzuia uhalifu kabla aujatokea. Unataka wasubiri mpaka madhara yatokee ndio wachukue hatua. Kuna wasaa kama hawajui siku wala saa muda busara ni kuonya watu waache.

Sasa utakwenda kuwakamata watu bila ya strong evidence ya kuwashitaki mahakamani, ndio msingi wa kukuuliza unafahamu conditions ‘actus reus na mens rea’ kwenye criminal case zote hizo lazima uthibitishe.

Sikiliza unaweza endelea ugomvi na wengine misikuingia kwenye hii mada kwa malengo ya kulumbana hasa mambo ya kijinga unayofikiria kichwani thinking that’s how actual the world work.
Kama polisi hawakuwa na ushahidi kwanini wakatutangazia kwamba Chadema wana mpango wa kuvamia vituo vya polisi Dsm?!

Kwamba unaona sahihi polisi kufanya kazi ya kuhisi?!

Uhalifu waliouzuia ni upi, kumuua marehemu bila ushahidi wa kosa lake? huoni kama walimuonea? au kututangazia Chadema wabaya kisha kuwatuma wasiojulikana?

Wewe ni mjinga kama hao polisi unaowatetea, wasting my time idiot.
 
Kama polisi hawakuwa na ushahidi kwanini wakatutangazia kwamba Chadema wana mpango wa kuvamia vituo vya polisi Dsm?!

Kwamba unaona sahihi polisi kufanya kazi ya kuhisi?!

Wewe ni mjinga kama hao polisi unaowatetea, wasting my time idiot.
Walikwambia wamehisi au wanataarifa za intelligence. Kwani si kunaweza kuwa na rat kwenye hiyo mipango akapeleka umbea.

Sasa polisi wenye jukumu la kuzuia uhalifu hawana jukumu la kuonya. Kwani si hata ubalozi wa marekani uwa inatoa warning kadhaa kuna hatari ya attacks.

Polisi kusema waliyosema hawana ulazima wa kwenda kukamata watu ushahidi wao autoshelezi kukamata watu.

Wewe sasa kama kauli hiyo imekuuma sana unaweza ongea na uongozi wa CDM kwenda kuwafungulia kesi ya defamation polisi watoe ushahidi wa intelligence yao, au waombe radhi. Lakini sio kuongea hatua za kuchukuliwa watu ambazo hazina uzito.

Huna unalolijua usinichoshe tafadhali, mkishaandika ujinga wenu humu na kugongeana likes basi mnaamini mna akili kweli.

Mie nishamalizana na wewe, ain’t nobody got time to entertain your nonsense any longer.
 
C&P from Face Book.

KUTEKWA, KUTESWA, KUUAWA KWA ALLY KIBAO, TUSAIDIANE KUTAFAKARI

Na Bollen Ngetti

SOMA lakini kwa tafakuri pana labda tukajua ukweli walau kidogo si wote katika giza hili lililofunika kutekwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kikatili Mzee Ally Muhammed Kibao al-maarufu MeD.

Niharakishe kusema ukweli kwamba hakuna uhusiano mzuri baina na kati ya CCM na Chadema kimkakati, kisiasa na hata kimtazamo na kimaadili. Niharakishe pia kusema kama ilivyo kwa vyama vyote kongwe ni hayawani pekee anayeweza kutenganisha chama-tawala na dola. Kwamba dola inaishi kwa hisani ya chama-tawala na kwa mantiki hiyo dola ina wajibu mkubwa wa kukilinda chama kwa gharama yoyote.

Sasa twende. Siku za karibuni Jeshi la Polisi lilitoa taadhari kwa umma mpana kwamba lina taarifa za kijasusi zisizo na chembe ya shaka kwamba Chadema inapanga makundi ya vijana yapatayo 20 ambayo yatavamia vituo vya polisi jijini Dar es salaam kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Polisi intelijensia ilionesha kikao kilichokuja na uamuzi huo mgumu ulifanyika kupitia mtandao wa ZOOM. Hata hivyo Polisi haikusema lengo la kuvamia vituo hivyo ni nini hasa? Kuvichoma moto? Kuwapiga Polisi? Kuwafungulia huru maabusu? Kukwapua silaha? Kwenda kuvitumia wapi? Endelea kutafakari.

SASA tujiulize haya maswali ya msingi. Hakuna mtu wa kawaida mwenye uwezo wa kuvamia kituo cha polisi akijua fika ni eneo salama iliyosheheni silaha za kivita. Mtu huyo anaweza tu kama naye ana mafunzo mahsusi ya masuala hayo ama ni jambazi mzoefu. (Rejea kuvamiwa kwa kituo cha Polisi Stakishari Ukonga).

Tembea na neno "taarifa zisizo na SHAKA" kichwani.

Hii maana yake ni kwamba wavamizi watarajiwa wa vituo vya polisi kutoka Chadema wana uwezo, mafunzo, ujasiri juu ya maswala ya usalama na kwa mantiki hiyo wasingekwenda kujaribu bali kutekeleza. Swali lingine linanijia kichwani maana taarifa ya Polisi ina ukweli "usio na shaka". Kwamba vijana hawa wa Chadema wamepata mafunzo hayo wapi na lini? Maana si majambazi kwa mujibu wa Polisi.

Vyuo vya usalama nchini vinajulikana kuanzia Polisi, Magereza, TISS, JWTZ. Wao wamepata mafunzo wapi? Chadema ina chuo cha mafunzo ya silaha kiasi cha kuvamia vituo vya Polisi kulikosheheni bunduki za kila aina?

Kama hawa chuo kama hicho ndani au nje ya nchi, basi tujiulize kusumbua bongo zetu. Nani aliwapa mafunzo wakaiva na hivyo kuwa na uwezo, ujuzi na ujasiri wa kuvamia vituo vya polisi ? Kwani Red Brigade wanafunzwa kuvamia vituo vya Polisi? Usichoke kutafakari....

SASA, moja ya sifa tuliyoambiwa Marehemu Ally Kibao anayo ni kwamba ni Mwanajeshi mstaafu aliyefika katiko vyeo vya juu si kabisa. Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretariat ya Chadema lakini pia tunaambiwa kuwa ndiye alikuwa ni "strategist" wa chama na ndio hakufahamika sana majukwaani maana alikuwa "nyuma ya kamera ".

Sijui viapo vya JWTZ vinasemaje ila Kibao baada ya kustaafu alijiunga na CCM na kuwa Mwenezi Mkoa wa Tanga na baadaye kutimkia Chadema hadi alipotekwa, kuteswa., kuuawa na mwili wake kutupwa vichakani huko Ununio (Dar es salaam).

Swali fikirishi! Je, ni huyu (Kibao), strategist, JWTZ mstaafu ndiye aliwapika vijana wa kuvamia vituo vya Polisi? Je, uratibu huu ulikuwa ukiendelea na tuseme Polisi waliamua kujihami kabla ya uvamizi kwa usemi, "mpige mchungaji na kondoo wote watatawanyika"? Haya yote ni kuwaza maana ripoti ya uchunguzi juu ya waliomuua Kibao ni kina nani hasa licha ya alama zote kuonesha ni watu wenye kumiliki pingu ama wa ndani au nje ya nchi. Yote yawezekana.

Je, polisi iko katika operesheni maalum kuzuia wavamizi kabla ya kuvamiwa? Swali linalogonga vichwa ni kwamba kama taarifa za kijasusi zilionesha kuwa MeD ndiye alikuwa "chuo" cha kuwaandaa wavamizi ndiyo auawe badala ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Sina jibu....wauaji wana majibu.

Nawaacha na swali hili! Kwa tusiamini kuwa nyuma ya vitendo vya utekaji Chadema haiko nyuma yake kisiasa? Kwa nini hutaki kuamini na kwa nini uamini. Nawatakia tafakuri njema na jadidi. Alamsiki.

PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Waandishi kama wewe ndiyo tunawahitaji hapa JF. Siyo kina Lucas na watoa mitusi na wapingaji.
 
Ndo Tanzania ya CCM hiyo
 
Back
Top Bottom