DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 84
- 118
Binafsi nimefanya utafiti nimejiridhisha pasi na shaka kuwa kile kinachodaiwa kwamba ulikuwa ni mgogoro kati ya Wafanyabiashara wa Wilaya ya Handeni na TRA, hususani Manager wa TRA Handeni mpaka kufikia hatua ya baadhi ya Wafanyabiashara kufunga maduka, ni mpango ulioratibiwa na baadhi ya Wafanyabiashara waliozoea kukwepa na kufanya biashara isivyo halali bila kufata taratibu za ulipaji kodi katika Wilaya hiyo ya Handeni.
Kuna mtandao wa baadhi ya wafanyabiashara unatumia mbinu na udhaifu wa baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuhalalisha ukwepaji kodi kama sehemu ya mazoea kwa baadhi ya wafanyabiashara kiasi kwamba kila Manager anayekuja Wilaya ya Handeni kundi hilo la Wafanyabiashara linatamani Manager huyo awe chini ya mamlaka yao ili waendeleze kusudio la ukwepaji kodi na hatimaye Wilaya ya Handeni na Tanzania kiujumla kupoteza mapato.
Mbaya zaidi usipokuwa sehemu ya kundi hilo lililotengeneza mtandao mpana lazima kundi hilo litafute namna ya kukuchafua kama wanavyofanya sasa kwa Manager mpya; "Mfano kuna wafanyabiashara mahodari wakutokutumia mashine za EFD kama tunavyopewa elimu ya mlipa kodi kila siku, lakini pia kuna baadhi ya wafanyabiashara hawataki kulipa kodi kwa wakati na baadhi kukacha kulipa kodi kwa njia halali zilizowekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na hatimaye kuikosesha Serikali mapato, hao hawataki kuguswa, wakiguswa wanazua mgomo."
Hapa Handeni kuna baadhi ya vishoka ambao wanawadanganya baadhi ya wafanyabiashara kuwa wakienda TRA watatozwa kodi kubwa hivyo kuwatia hofu na uoga baadhi ya wafanyabishara huku wao kama vishoka wakikusanya hela za walipa kodi kwa njia ya udanganyifu.
Manager wa sasa kawabana kiasi kwamba hawatambuliki kisheria, kama wewe ni mwakilishi wa mtu basi unaambiwa aje mhusika mwenyewe, Pia hao vishoka Wilayani Handeni walitengeneza genge la ukwepaji kodi na kukacha kulipa kodi halali ya Serikali katika biashara huku wakiwaaminisha wafanyabiashara wadogo na watanzania kwamba Manager wa TRA Handeni ndiye tatizo kumbe sivyo.
Achana na hao wafanyabiashara wadogo waliotumika kuandaa migomo na kusababisha baadhi ya maduka kufungwa bila kujua kwamba wanatumika na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, kundi hilo la wafanyabishara wakubwa liliandaa pia baadhi ya waandishi wa habari ili kumchafua Manager wa TRA Handeni, lengo na kusudio lao ni moja tu kutoa msukumo ili Manager huyo wa TRA ahamishwe kituo cha kazi ili Wafanyabiashara hao wapate uhalali wakuendeleza ukwepaji kodi.
Kwasasa pale Handeni kuna baadhi ya watumishi wa TRA wanakerwa na usimamizi bora na mzuri wa Manager huyu wa sasa katika utendaji kazi, Manager huyu anafuatalia sana ufanisi na utendaji kazi haswa wafanyakazi wanapohudumia wananchi, "Mfano baadhi ya wafanyakazi walizoea kufanya kazi kwa mazoea bila usimamizi, Manager huyu wa sasa anawasimamia ipasavyo ule mtindo wa kufanyakazi huku mtu ana chati hakuna kabisa.
Mfano mzuri nilishuhudia mwezi wa tatu akiwaeleza maofisa wake watu wote wanaokuja kulipa wawe kwenye foleni na akaenda mbali zaidi kuwambia kuwa wazee na wale waliokuja na watoto wadogo wahudumiwe kwanza waondoke, sasa hapo kweli utasema Manager huyo mbaya?
Lakini pia wafanyabiashara tujifunze kitu, "Unaposema una biashara Dar na Handeni, hiyo biashara ya Dar kama TIN ni moja na biashara ya Handeni unalipia kodi wapi! au badae ikigundulika hulipi kodi Handeni utakuja kusema unaonewa na Manager?
Tujifunze kupata elimu ya mlipa kodi kabla ya kukimbilia kutoa shutuma na kusababisha taharuki.
Binafsi nikiwa kama mlipa kodi wa Wilaya ya Handeni, nampongeza Manager mpya wa TRA Handeni kwakazi nzuri na bora. 90% ya wafanyabiashara tumeelewa dhamira njema ya Manager, ukiondoa hao wafanyabiasha wachache wanaotumika bila kujitambua kwamaslahi ya wafanyabiashara wakubwa waliotengeneza genge la ukwepaji kodi wilayani Handeni.