Samiaagain2025
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 3,626
- 3,869
WanaJF,
Hongereni na usiku wa mapinduzi ya Zanzibar. Na naenda kwenye mada moja kwa moja.
Kila kundi wameongea yao; Wanasiasa, wanaharakati, wasomi wa kawaida, wanasheria, viongozi wa dini na makundi mengineyo.
Swali ambalo leo naliweka kama principal question kwa makundi hayo yanayotoa maoni ni hili;
Je, mheshimiwa rais anawatuma viongozi wapeleke au viongozi wanyewe wanaamua kwa utashi wao wapeleke Chato miondombinu hiyo?
Mimi kama Mtanzania nadhani huenda nadharia ya pili ya swali la msingi ina nguvu.
Tunajua wazi viongozi wa siku hizi walioko chini ya rais walivyo na tabia ya kujipendekeza na unafiki, ili tu waendelee kubaki kwenye nyadhifa zao, wakijua pia kuwa Kuna makosa yao fulanifulani mheshimiwa rais anayajua.
Nahitimisha kwa kuwakaribisha Watanzania wenzangu, na nyinyi muone ni nadharia ipi kati ya hizo mbili zilizopo kwenye "Principal question".