Kuhusu miundombinu Chato, Rais anawaagiza au viongozi wenyewe wanaamua tu kuipeleka huko?


Wakati wa kampeni alisema yeye ndiye anaamua maendeleo yaende wapinakuwahawezi kupeleka maendeleo kwa wanaochagua wapinzani.Kwa hiyo ikowazi nani anayeamua
 
Hata Chato ni Tanzania Ila kwanini kila mradi ni huko Chato? Tanzania ni kubwa sana kuna Mtwara, Kigoma na Mikoa mingine ambayo nayo ilistahili kupata miradi ya mikakati ya maendeleo. Kinachotokea hivi kinaweza kuleta madhara uongozi utakapobadilika. Upo uwezekano kila Rais akafanya upendeleo Kwa kanda atakayotoka. Tuchukue tahadhari Kwa kumshauri Rais wetu.
 
Na mbaya zaidi,miradi inaenda huko kwa mfululizo! Is it a simple probability or?
 
Rejea kauli zao youtube wakati wa kampeni,ikirudiwa na mtoto wa dada pia kwamba wao ndio uamua wapi maendeleo yaende wapi yasiende.
Rejea kauli ya Mwalimu ikulu ni sehemu takatifu sio KILA mtu ni lzm aende.
 
Kama ni viongozi wanajipendekeza kwa nini Rais akae kimya?Kwa nini Rais asikemee?
Rais alikwisha kemea pale Dodoma mbele ya TAKUKURU. Ila maendeleo haya ni kwa wote iwe chato, iwe Manyoni,iwe Manyara nk.
 
Hii miaka 4 iliyobaki tungependekeza miradi yote iende Chato Ili akastaafu salama na apewe nchi ya Chato atawale milele atuachie nchi yetu tumpe mwingine atakae tumia vizuri Kodi zetu.
 
Toeni ushauri na siyo kukata tamaa.Hakuna mwenye hii nchi,ni yetu sote.
Hii miaka 4 iliyobaki tungependekeza miradi yote iende Chato Ili akastaafu salama na apewe nchi ya Chato atawale milele atuachie nchi yetu tumpe mwingine atakae tumia vizuri Kodi zetu.
 
Anapenda mwenyewe....wangekuwa wamepeleka miundombinu miwili ningesema wanajipendekeza kwake sasa wanapeleka kila kitu unategemea nini?

Anawaambia mwenyewe nataka Chato muweke hiki na hiki.
 

Dr Chalz KIMEI alitatua ilo swali lako kipindi anazindua CRDB ,KIMEI alisema MAGUFULI ndio aliyefanya utafiti na ndio wakaamua wajenge CRDB CHATTLE.

Conclusion: JIWE ndio anatoa maelekezo ya mambo yanayofanyika CHATTLE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…