Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kusema kwako MUNGU yupo bado Hakuthibitishi uwepo wa huyo Mungu.

Thibitisha Mungu yupo na si imani na mawazo yako ya kufikirika tu.
aaa bas hayupo ila yupo unaweza akawa na kwako ila kuna vitu vya kufanya ili awepo kwa mtu
 
Wanamajumui wa Afrika wanapambanua kwamba hakuna jamii iliyowahi ishi bila kumtumaini mungu hapa duniani.Kilichosababisha jamii zetu kuacha asili zetu na kufuata miungu ya kigeni ni conversion(badili dini) na kuacha misingi yetu na kuwa wazungu weusi.Tunapata amani gani tunaposhadadia miungu ya kigeni?
 
Wengi wanaweza kukuona hauko sawa ila una logic ambayo wengi bado hajajiuliza.

Uhalisia ni kwa kwamba Muumba ni mmoja na uhalisia wake yeye ni CHANZO HALISI cha uumbaji wote unaooneka na usioonekana.

Unaposema Mungu wapo wengi japo wengi wanadhani ni mmoja sababu hiyo ni generalised term.Ndo maana ni rahisi kusikia malaya akiomba Mungu amsaidie kwenye umalaya au mwizi akiomba Mungu amsaidie kwenye wizi wake.

Unaposema Mungu(Genesis) ndie mwanzo na mwisho ila tambua kuwa Muumba (Source)hana mwanzo wala mwisho.

Haya unayoyaona ambayo ni mabaya (vita,magonjwa,vifo,umaskini,dhambi,uasi na uovu) yanayotokea ni sababu uumbaji ulikuwa kwenye uteka na Muumba alisubir majira yake aje mwenywe kurekebisha yote.

Warumi 8:21
kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.
 
Imani ya kweli na sahihi ni kuwatendea viumbe vyote yale unayotaka kutendewa na kutomtendea usiyotaka kutendewa

Hiyo ndiyo IMANI THABITI, achana na Dini na Miungu yote unayoijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…