Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Mtu amejua ulimwengu umekuwepo kabla ya yeye kuwepo baada ya yeye kuwepo.

Maana yake ni kwamba mtu hakuwa anajua kama ulimwengu upo au hata umekuwepo kabla ya yeye kuanza kuwepo. Uzoefu huo ameupata baada ya kuanza kuwepo duniani.

Kwa maneno mengine ni kuwa, kabla mtu hajaanza kuwepo duniani hakuwa anajua kama ulimwengu upo na kwamba umekuwepo kabla ya yeye kuwepo.

Hii inaonyesha kwamba kama mtu au watu hawatakuwepo, uzoefu kwamba ulimwengu upo au ulikuwepo na utakuwepo hautakuwepo na hivyo ulimwengu pia hautakuwepo.
This logical fallacy is called logical non sequitur.

Ukweli kwamba wewe hunioni, haumaanishi kwamba mimi sipo.
 
This logical fallacy is called logical non sequitur.

Ukweli kwamba wewe hunioni, haumaanishi kwamba mimi sipo
This isn't a logical fallacy. Otherwise you're that logical fallacy.

Kutokuwepo na kutoonekana ni mambo mawili tofauti. Hoja sio kutoonekana. Hoja ni kutokuwepo.
 
Usipokiona kitu, je, hilo linamaanisha hakipo?

Kabla hujazaliwa, ulikuwa huuoni ulimwengu, je, hilo linamaanisha ulimwengu ulikuwa haupo?
 
Mtu ambaye hajazaliwa - mtu ambaye hayupo, huo uzoefu kwamba ulimwengu ulikuwepo anaupata wapi? Kwa sababu uzoefu kwamba ulimwengu upo au umekuwepo kabla, mtu au watu wameupata baada ya kuwepo duniani.

Labda kama kuna taarifa zinazoonyesha mtu amewahi kuwepo katika sayari nyingine kabla ya kuwepo duniani.

Unapouliza "Kabla hujazaliwa, ulikuwa huuoni ulimwengu, je, hilo linamaanisha ulimwengu ulikuwa haupo?" Hili swali lako linaonyesha uzoefu. Ni swali ulilolipa baada ya kuwepo - baada ya kuwa na uzoefu. Kabla ya kuwepo, mimi au mtu mwingine yeyote hakuwa na huo uzoefu.

Hii hoja yako ingeweza kuwa na maana kiimani lakini sio kiyakinifu (materialism).

It is like to say there is no possibility of God in our earth but there are forms of intelligent out there. What interesting!
 
Kwa hivyo, ili kitu kiwepo, ni lazima ukione?

Vyote ambavyo hujaviona havipo?
 
Mkuu samahani nna swali hivi tangu uzaliwe hukuwahi kuamini ata kidogo uwepo wa MUNGU🤔 ? umekulia katka familia ya wapagani au ya dini?
 
Nimekulia katika familia ya Ukristo tena kwetu pande zote ni kanisani. Upande wa baba ni watu wa kanisani na upande wa mama ni watu wa kanisani yani nikirudi nyumbani kwenye makaburi ya familia pande zote ni kanisani na babu yangu upande mmoja alikuwa mchungaji, upande mwingine baba yake bibi yangu mchungaji.

Baba yake bibi yangu mzaa mama kajenga kanisa la Azania Front hapo Dar, wamemaliza kujenga na Wajerumani mwaka 1903. Kwetu wachungaji wapo mpaka leo, si historia tu.

Ila, neno "wapagani" linatumika vibaya.Wapagani si watu wasioamini Mungu, wapagani ni watu wanaoamini miungi tofauti na miungu ya dominant cultures kama Ukristo na Uislamu.

Hivyo, wazungu walivyokuja Afrika na kukuta watu wanaabudu miungu yao, mizimu, wakawaita wapagani.

Pia, katika dunia ya wasomi wa leo inayokubali kwamba habari za Mungu ni tamaduni tu, na kila utamaduni una Mungu wake, neno "wapagani" linaonekana si neno zuri, ni neno la wakoloni kunyanyapaa watu wa tamaduni tofauti.
 
Okay. Ulianza lini kuamini kuwa hakuna MUNGU?
 
Nilianza kuwa na maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu tangu nikivyokuwa mdogo.

Nikiwa darasa la sita (miaka 11) nilisoma nadharia za Laplace kuhusu dunia ilivyoanza, na zilikuwa tofauti sana na habari za dunia kuumbwa na Mungu zilizomo katika Biblia. Nikaona tatizo habari za Biblia na sayansi kuwa tofauti, nikaona hapa lazima kuna upande unakosea, vyote viwili haviwezi kuwa sawa wakati vinatupa habari tofauti.

Niliendelea kuwa na maswali mengi, na kusoma sana, falsafa tofauti, dini tofauti, polepole nikizidi kuondoa imani ya Mungu.

Kufikia umri wa miaka 19 nikasoma kitabu kinaitwa "Philosophy of Religion: An Anthology". Kitabu hiki kilikuwa na maelezo mengi sana kuhusu falsafa za dini tofauti (anthology). Lakini sehemu m9ja ilinivutia na kunifumbua macho zaidi, inaelezea kitu kinaitwa "the problem of evil" kama ilivyoulizwa na Epicurus. Hiyo chapter ndiyo iliyonifungua macho kujua bila shaka kuwa huyu Mungu tunayemuamini (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) hayupo, ni wa hadithi ya kutungwa na watu tu. Kisayansi na kimantiki kabisa.

Kusema Mungu huyo yupo ni sawasawa na kusema kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara katika Euclidean geometry.
 
Kwa hivyo, ili kitu kiwepo, ni lazima ukione?

Vyote ambavyo hujaviona havipo?
Naomba kusistiza kwamba, katika mtazamo wa kiyakinifu kabla watu kuwepo na watu wasipo kuwepo huo uzoefu haupo.

Juu ya hili swali lako, angalia namba 254
 
Kutokuwapo kwa uzoefu wa kitu ni kutokuwapo kwa kitu?
 
Hiki hapa
Asante sana mkuu.

Nilipoteza hiki kitabu. Ni kizuri sana. Kinafanya utazame mambo kwa makini. Kinaleta hali kuuliza zaidi badala ya kukubali mambo tu bila ushahidi wao wa ndani, bila kujua.
 
Naam.

Kumbe ulikuwa nacho awali pia?
 
Back
Top Bottom