Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

 

Pascal si wende ukamshitaki mahakamani ??? Hujachelewa nenda mahakamani ukamdhibiti usimwage povu hapa JF la kutafutia upewe tonge ya ugali

 
Huyu nae makamu asituchanganye,basi Kama anakosa usngz na hiyo soveregnity yao ,si aitafute iikopotelea!!asituchanganye hapa na harakati za kusaka uongoz wa juu wa zbr,
 
Kuna Mquebec aliwahi kuuwawa , kunajisiwa kuchukuliwa mali yake , kujeruhiwa kwa risasi na Mcanada yeyote ??

Nadhani nyinyi watanganyika mjifunze kuwa huu si muungano ni uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar.
Hebu tuambie waunguja na wapemba wangapi wamenajisiwa, kuchukuliwa mali zao, na kuuawa kwa risasi na watanganyika? Halafu niambie wangapi walifanyiwa yote hayo wakati wa Mapinduzi na chini ya utawala wa Hayati Karume? Aidha, niambie wakati hao watanganyika wanafanya huo unyama nani alikuwa Rais wa Zanzibar? Mwisho niambie mtanganyika yupi alifuta matokeo ya uchaguzi wenu mwaka 2015, na aliyeharibu uchaguzi wenu wa hivi karibuni.
Hampendani lakini kwa unafik wenu mnataka kutulaumu machogo kwa chuki zenu.

Amandla...
 
Huu ni uchochezi wa kwango cha SGR.

Unapo mtaja makamu wa rais wa zanzibar pekee kuwa ni muongo wakati ndani ya ccm ndiyo kiwanda cha waongo.
 
Ni haki yake kuzungumza atakacho. Lakini kwa nini asubiri mpaka mtanganyika amvue koti badala ya kulivua mwenyewe wakati linambana kwa miaka 57? Mmo kwenye serikali ya Muungano ambayo mnasema imeumbwa kuidhibiti Zanzibar lakini mnaishia kuwaomba watanganyika wawape talaka? Mnadai mmepigwa, mmeuawa, mmedhulumiwa katika uchaguzi uliopita lakini hamkusita kujiunga na serikali iliyotokana na uchaguzi huo? Leo Chadema inapambana kudai Katiba Mpya ambayo itazungumzia hayo mnayolalamikia lakini mmekaa pembeni mnawaangalia!

Quebec, Scotland na Catalonia walipoona wanaonewa katika mfumo uliokuwepo waliweka wazi agenda ya kujitoa katika Muungano wao na wakapigania. Nyinyi mnashindwa nini? Hasa kwa sababu mnajua Muungano wenyewe hauna uhalali kwa sababu hamjau ratify? Acheni kupambana na machogo. Washikeni wanasiasa wenu ili waanze juhudi za kuvunja muungano ambao hauna faida kabisa kwenu.

Amandla...
 
GDP per Capita ni kipimo cha uchumi na ni kipimo kinachotumiwa hata na Benki ya dunia. Uchumi ambao unasema ni moja la jukumu la serikali ya JMT kusimamia halafu imeshindwa kutokana na umasikini uliopo.

Sababu za mapinduzi ziko nyingi, nyingine hizi hapa

 
Naona mazuzu mnapongezana
Ni vigumu kutambua idadi ya watu wenye mafaili kule hospitali ya Milembe waliopo hapa jukwaani. Lakini kwa kuwa visa vingi vya wangojwa hulipuka katika kipindi cha miezi ya Septemba na Octoba, sioni ajabu kwa mgonjwa wa kwanza kujitokeza hadharani na maoni kama haya.

Ugua pole mkuu, "wishing you quick recovery"
 
Hiyo habari za mirembe anazijua Ndugaye maana alishajitangaza kuwa anafaili.
 
Hiyo habari za mirembe anazijua Ndugaye maana alishajitangaza kuwa anafaili.
Mkuu kunywa maji mengi, na unahitaji muda mwingi wa kupumzika na kutuliza akili. Ni hivyo tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
NB: Kuna mambo ya muungano.

Tanganyika na Zanzibar tuliungana katika mambo hayo tu. Mengine yote nje ya mambo hayo, Zanzibar ni nchi na inajitegemea. Ila Tanganyika (kwa yale yasio ya Muungano) inategemea JMT.

To be honest, muungano wetu ni wa kulazimishana tu. Muundo wake ni wa hovyo (kwa maoni yangu).
 
Tumekusikia ,Sasa jibu swali
Kuna MQuebec yupi aliwahi kuuliwa, kunajisiwa ,kuibiwa Na mKanada yeyote?
 
Tumekusikia ,Sasa jibu swali
Kuna MQuebec yupi aliwahi kuuliwa, kunajisiwa ,kuibiwa Na mKanada yeyote?
Mwaka 2019 waquebec 77 waliuawa. Idadi za walio najisiwa hazijulikani maana watu wengi wana ficha. Au unadhani Canada watu hawauawi, kunajisiwa au kuibiwa? Kuwa hayo yanatokea kwenu tu?

Amandla...
 
Confusing vs Mixing. Hata hivo Asante kwa andiko murua
 
Inakubalika kote kuwa GDP siyo kipimo kamilifu cha hali ya uchumi wa nchi. Kwa mfano mapato yanayotokana na dhahabu yetu yatahesabiwa katika GDP yetu wakati ukweli ni kuwa sehemu kubwa inahamishwa na kupelekwa katika nchi ambako Barrick wana makao yao makuu. Kwa upande mwingine, sehemu kubwa sana ya biashara katika nchi zinazoelendelea sio formal kwa hiyo haziwi reflected katika GDP yake. Kingine ni kuwa remittances ambazo zinaingia nchini kutoka kwa raia wake wanaoishi humo ni nadra kuonekana katika hesabu za GDP. Ndio maana wakaja na GNP ( Gross National Product) kama kipimo sahihi zaidi ya hali ya uchumi wa cnhi. Lakini pamoja na haya, wachumi wakasema takwimu hizi hazireflect ubora wa maisha ya wananchi wanaoishi humo kwa sababu haionyeshi tofauti ya kipato baina ya wakati. K.m. Equatorial Guinea ni zaidi ya dola 34,000.00 lakini sehemu kubwa ya GDP imehodhiwa na watu wachache na sehemu kubwa ya raia wake wana hali duni sana. Mfano kama huo unaonekana Gabon ( Usd 19,266). Raia wa Equatorial Guinea wengi hawana access ya maji safi wakati Rais na ndugu zake wana majumba ya kifahari Marekani na kwengine. GDP per capita imekosolewa kwa kuto reflect thamani ya pesa nchini. Kwa mfano, sarafu inayotumika ni dola lakini kuna tofauti kubwa baina ya nchi ya thamani ya dola moja (vitu na huduma zinazoweza kununuliwa na dola moja) ndio maana kipimo kinachotumika sasa ni GDP PPP ( Purchasing Power Parity). Kwa sababu hiyo dhana ya kusema GDP per Capita ndio kipimo sahihi cha hali ya uchumi katika nchi haikubaliki tena. Inatumika tuu kwa sababu ya urahisi wake na mazoea.

Mimi sikatai kuwa JMT ni masikini. Ninachokipinga ni pale mnapoilaumu JMT kwa umasikini wa pemba na Unguja.

Anachozungumza Bharwani ni kuwa waliopindua ni Afro Shirazi dhidi ya waarabu wa chama cha Hizbu. Hajaeleza kwa nini Afro Shirazi walikuwa na chuki na Hizbu. Anawalaumu Waingereza kwa kuto kutoa ulinzi kwa serikali yao. Hizi ndio chuki ninazozizungumzia. Waarabu mpaka leo hawajawasamehe Afro Shirazi na Afro Shirazi wanahofia makaburi kufufuliwa.. Zanzibar wanatakiwa kuwa na Truth and Reconciliation Commission kuzungumzia historia yao na kuombana msamaha wa dhati badala ya kushinda kuwalalamikia machogo. Bharwani anasema wafuasi wa Afro Shirazi walitumia mishale kuteka arsenal ambayo ilikuwa na silaha. Ninachojiuliza ni kuwa kama walikuwa na silaha kutoka Algeria zilizopitia Dar, kwa nini walitumia mishale?

Amandla...
 

Mwaka 2019 waquebec 77 waliuawa. Idadi za walio najisiwa hazijulikani maana watu wengi wana ficha. Au unadhani Canada watu hawauawi, kunajisiwa au kuibiwa? Kuwa hayo yanatokea kwenu tu?

Amandla...
Tuwekee ushahidi kuwa wa Quebec hao waliuliwa kwa kudai uhuru wao ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…