Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

GDP per capita ni kipimo kimoja cha uchumi. Siyo kipimo pekee. Na ni kipimo ambacho benki ya dunia inakitumia. Sasa wewe na benki ya dunia ambayo ina wachumi walioshinda tuzo ya Nobel ni nani mtaalamu zaidi wa uchumi?

Kama ni serikali ya JMT ndiyo inasimamia uchumi na umasikini umezidi, nani mwingine alaumiwe? Wanzanzibari wangekuwa raia wa Oman, wangefaidi matunda ya uchumi wa Oman kama raia wengine wa Oman.

Pointi ya video ya Sheikh Barwani ni kwamba mapinduzi yalipangwa au yalichochewa na watu ambao si Wazanzibari. Wazanzibari walivyo na baadaye wajiunge na Oman badala ya kujiunga na Tanganyika, leo wasingekuwa masikini kama walivyo.
 
Mimi binafsi naona kuna tatizo mahali tunahitaji kupitia upya muungano huu kwani upande mmoja wa muungano inaona unaonewa. Hili lipo wazi, nahisi muungano ulifanyika kwa haraka bila kuangalia mambo yote vizuri, na sasa inapaswa kuupitia upya uli kuaddress mengi yaliyojitokeza na kuangangalia je tunahitaji muungano wa aina ile ile au uboreshwe kama kuna haja ya muungano kuwepo.

Wakati wa kuandaa rasimu ya kikatiba kulikuwa na dhana ya serikali tatu ili Tanganyika iwe na serikali yake na Zanzibar wawe na yao kama ilivyo sasa na juu kuwe na serikali ya shirikisho.

Au kuwe na majimbo na federal government ingawa hili laweza kuwa gumu kwa Wazanzibar. Kulifumbia macho hili haileti afya yoyote kwa upande wowote. kwa dunia hii na utandawazi huu na technolojia hii Zanzibar sio threat kwa Tanganyika kwa vyovyote vile hali kadhalika kwa Zanzibar, issue za kiusalama hazina tena mashiko tuliangalie willingness na muungano wenye win win situation.
 
Makubwa bado kuna watu wanawazo kujiunga na Oman hii ni ndoto za mchana. Kweli Zanzibar mna shida kubwa.
 
Amesema bayana kuwa alionywa kuwa Afro Shirazi walikuwa wanapanga kufanya fujo. Afro Shirazi ni chama cha watanganyika? Vurugu za 1961 zilichochewa na watanganyika? Ni nani alizisababisha? Tatizo kubwa ni kuwa hawataki kukubali kuwa wale waliokuwa wanawaona kama watwana walikuwa na genuine grievances.

Wazanzibari wengi waliokuwa wanachama wa Afro Shirazi na Umma wasingekubali kuungana na Oman kwa sababu waliwaona sehemu ya utawala dhalimu dhidi yao. Na haujiulizi kama Oman ingekubali wajiunge nao hasa ukiangalia kuwa Sultan wa Zanzibar angeweza kutaka awe sawa na binamu zake? Hamjiulizi kwa nini kama Oman waliipenda sana Zanzibar kwa nini hawakumpokea na kumpa hifadhi ndugu yao? Badala yake walimuacha aishi maisha duni Uingereza.

Maendeleo ya Zanzibar hayataletwa na nchi nyingine yeyote, Tanganyika au Oman, bali wazanzibari wenyewe. Singapore ilipokataliwa kujiunga na Malaysia Federation kutokana na umasikini wao na idadi kubwa ya raia wao wenye asili ya China, hawakujikunja na kulalamika kuwa hawapendwi. Walijipinda wakafanya kazi mpaka sasa ni tajiri kuliko Malaysia.

GDP per Capita inatumika kwa ajili ya convenience na world class economists wanajua kuwa haitoi picha kamili ya hali ya uchumi wa nchi. Bila shaka hata Stiglitz atakuambia hilo.

Amandla...
 
Adui wa Zanzibar ni machogo na vibaraka wao ,hilo halitaki kiona mbali wala microscope au darubini., hakuna cha mwarabu wala mreno ,Zanzibar imeanza kudidimia pale walipozidi kuunganisha vyama ndio ikamezwa kabisa ,imebakia mkia tu ndio wanaouchezea waTanganyika wapinga maendeleo.
 
Makubwa bado kuna watu wanawazo kujiunga na Oman hii ni ndoto za mchana. Kweli Zanzibar mna shida kubwa.

Hapa ndiyo mnapokwenda mchomo. Zanzibar kuungana hata Na Shetani ni haki Yao , mradi wanaona atawaletea maendeleo. Nyinyi Na nchi yenu Tanganyika Pia hamkatazwi kuungana Na malaika mradi ndio uamuzi wenu.
Pili pili msiyoila inawawashia nini ?
 
Jawabu ni kweli Makamo yupo sahihi.
Na nyie vidudu watu mnaosema waZanzibar wanataka kujiunga na Oman hilo ni lenu,,, letu ni kuwa tumewachoka furustop.
 
Hapa ndiyo mnapokwenda mchomo. Zanzibar kuungana hata Na Shetani ni haki Yao , mrsdi wanaona atawaletea maendeleo. Nyinyi Na nchi yenu Tanganyika Pia hamkatazwi kuungana Na malaika mradi ndio uamuzi wenu.
Pili pili msiyoila inawawashia nini ?
Sipendi kubishana na wewe kwani uchungu wenu mnaujua zaidi kuliko sisi wa Tanganyika. Endeleeni kupambana ili muirudi nchi yenu kwa Sultani. Hongera Zanzibar.
 
Sipendi kubishana na wewe kwani uchungu wenu mnaujua zaidi kuliko sisi wa Tanganyika. Endeleeni kupambana ili muirudi nchi yenu kwa Sultani. Hongera Zanzibar.
Mapambano yanaendelea , kuku wanasubiri mtama umwagwe by THE way Lukuvi alishaanza kuumwaga kule kanisani kwa upande wa wakristo
 
Kwa Leo namuuliza Pascal. Jee umeona umuhimu was kubadilisha kichwa cha habari Leo au Mods ndio wamefanya wao.

Nilitathmini busara zako kama maneno Yale " kusema uongo" unaweza kumwambia hats mbunge tu seize makamo was Rais. Tulijaribu kukustua ukaacha tu ndio tukasema punguza chuki kwa huyo Mh.
Leo kumebadilika jee ukweli umejona au ni mods tu.
 

Hana ujemedari huo wa uandishi ni bahati tu ilimkuta,ameshakosa dira alikua na chuki na zanzibar tangu miaka hiyo, ila achunguze vizuri hakuna aliefanya chuki na zanzibar akapata salama, hafi kabla ya kulipwa mabaya ya chuki zake
 

Ulisahau na Makanisa hasa hili la Kikatoliki. Tunaona wanavyogombea kujenga makanisa sehemu zisizo na mkristo hata mmoja. Mradi tu wa provoke waislamu waanzishe fujo .


Vitabu vya kanisa vinasema waziwazi

 
Soma historia utaona grievances za watu zinaweza kutumiwa na watu wengine, nchi nyingine kuleta mapinduzi.

Nilishakujibu kuwa ugomvi wa familia ya Al Said siyo ugomvi wa Wanzanzibari wote na Waomani wote. Hata mke na watoto wa Jamshid walihamia Oman mapema kuliko baba yao.

Muungano faida yake nini sasa? Ulisema kuhakikisha uchumi kitu ambacho Muungano umeshindwa na umasikini umezidi Zanzibar.

Kwa nini nimuulize Stiglitz wakati najua kusoma takwimu na documents za Benki ya dunia? GDP per capita ni kipimo kimoja cha uchumi, siyo kipimo pekee. Benki ya dunia inakitumia.
 
Sawa. Hamjachelewa bado. Vunjeni tu Muungano. Baada ya kuuvunja mtaweza kuungana na Oman ambao watawamwagia mafedha na umaskini utaisha Zanzibar.
Stiglitz ndio economist wa World Bank aliyepata Nobel Prize.

Kwangu mimi mjadala umeisha hapa. Nakutakia siku njema na mafanikio katika jitihada zenu za kuungana na Oman.

Amandla...
 
Hapo utakuwa umekasirika jee ulitaka tukwambie Na nyinyi endeleeni Tu Na uvamizi mkiupa jina la muungano huku mkituletea umasikini zaidi Na kuwabambikizia watu kesi Za gaidi Na kuwaweka magerezani?
 
Andiko maridhawa.... Kongole Pascal
 
Kama Karume ndiye aliutaka Muungano zaidi kuliko Nyerere kwanini Willium Lukuvi aliongea maneno haya miaka kadhaa iliyopita? 👇👇


Nyinyi Wadanganyika ni watu ambao mukishalishwa maneno mnakuwa wavivu hamtaki akili zenu kuzituma kutafuta kulikoni, sasa nimekutumia clip ya Mtanganyika mwenzako anatapika kila kitu kwanini Tanzania Bara inaitawala zanzibar kimabavu, nione kama utainua mdomo wako tena.
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Kwani Sasa kuna serikali ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…