Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Mawazo yako hayana tofauti na haya ya Mswekwa, nadhani hamufahamu umuhimu wa utambulisho wa mtu. Kama wazanzibari watakubali ni sawa jaribu kupeleka mswada barazani wa serekali moja. Au ni bunge tuu litapitisha serekali kama lilivyopitisha muungano mawazo ya wazanzibari hayana umuhimu.

Mfano wako pia ni Nyerere alipropose (mwanaume) ukimaanisha Karume (Zanzibar) ndio unaolewa. Sema huu mfano ni wa ndoa za wanaume wawili gay mariage. Kwa sie waislamu ni haramu mifano ya namna hii, sijuwi huko Tanganyika pengine imezoeleka kidogo 🤷‍♂️
 
Wavaa kobazi bhna.

Chamsingi kuwe na serikali moja tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yaani huyo sijui ndiyo makamo au Makamu....Ukimwangalia utaona ni kama jitu fulani lisiloelewa, ni kulalama kutwa nzima, sijui yukoje?
 
Kwani aliyetakiwa kutangaza msiba ni makamu wa Rais au katibu mkuu kiongozi?
Tanganyika ndio tumepoteza kila kitu. Just imagine now tunaongozwa na huyu bibi mkojani?!!!!
Ndio maana ilimchukua muda sana Dr. Bashiru kutangaza msiba, maana alikuwa anajiuliza huyu bibi ataweza?!!!
 
Wavaa kobazi bhna.

Chamsingi kuwe na serikali moja tu.

#MaendeleoHayanaChama
Kama nilivyoanisha awali pelekeni mswada tuu wa serekali moja. Mtazame alipo Karume wakati wa kuchanganya, halafu utafsiri vizuri ni kwanini Nyerere ndio anachanganya mchanga ? Ukijua hilo utapata tafsiri kamili ya muungano huu na utashi wa Tanganyika kutaka kuimeza Zanzibar (serekali moja).
 
Niwapeni tuu maoni yangu binafsi juu muungano, I am being honest hapa. Sitaki muungano na Tanganyika wala Kenya, napendelea Zanzibar ilio huru na mamlaka yake kamili. Sisemi hivi kwamba namchukia mtu lakini siwezi kujua faida za muungano, faida yake kubwa ninayoifahamu ni kila uchaguzi viboko ili Tanganyika ipate kueka mtu inaemtaka aongoze Zanzibar.

Jengine ni vitunguu na viazi, I really can not tell anything positive at the moment and trust me I am trying hard to think! Lakini hasara za muungano na madhila yake mkiyataka naweza jaza chapisho zima hapa!

Kama muungano una faida basi nadhani ni wazi ukimuuliza mwananchi wa kawaida kule visiwani haswa Pemba, inatakiwa mzanzibari aweze kusema haraka faida. Hata Mswekwa mwenyewe hajaweza kuorodhesha faida za muungano badala ya Nyerere alikunywa mvinyo kwa furaha ya kutimiza ndoto yake.

Obviously Mapinduzi yalipangwa na Nyerere na kuyalinda makes lots of sense.
 
Nyerere mwenyewe alikataa pendekezo hilo kwamba utaifa wa Zanzibar utapotea kwenye serikali moja, japokuwa Karume alikubali na hata kuwa tayari kuachia urais ili Nyerere aongoze. Ndiyo maana Wazanzibar wanakosea wanapomlaumu Mwl kwa muungano ambao muundo wake umebakisha utaifa wao na pia wanafaidi vingi ambavyo huenda wasingefaidi kama wangeendelea kubaki nje ya muungano. Bitter Truth.
 
Pascal Mayalla, unachanganya maneno haya mawili , makamo na makamu. Usahihi ni Makamu wa kwanza au wa pili wa Rais na siyo Makamo wa kwanza au wa pili wa Rais.
 
Huyu OMO ulianza kumkosoa toka kitambo.
 
Hili ni wazo lake kuwa walipotenza ni wazanznibar na wala sio Tanganyika. Okay suluhu ni nini? Suluhu ni kuwapa serikali yao huru. Na iwapo kuna faida yoyote ya ushirikiano uwe defined kama ule EAC. Na naona bora iwe hivyo tushirikiane tu kwenye EAC period. Na wao kwa mamia kwa maelfu Warudi kwao Zanzibar. Kwani wabara hawana cha kupeteza kwani walibaguliwa na hawakuruhusiwa kuhodhi ardhi Zanzibar.
 
Zanzibar inachangia 1% ya makusanyo yote ya TRA. Nenda kaangalie facts and figures pale Wizara ya Fedha afu uje hapa tubishane kwenye hili la kodi
 
Imepokwa sovereigninty ? Vipi kuhusu kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika ilhali kuna Rais wa Zanzibar na serikali ya SMZ kiujumla wake ?
Zanzibar ina makamu wawili wa rais ambao ni wake, jaji mkuu wake, mwanasheria mkuu wake, DPP wake, mamlaka zake za udhibiti uchumi mfano ZURA, ZIPA, Tume yake ya Ushindani wa kibiashara na kdhalika.

Unaweza kunitajia mwanasheria mkuu wa Tanganyika ni nani? Jaji mkuu wa Tanganyika ni nani ? Makamu wa rais wa Tanganyika ni nani ? DPP wa Tanganyika je ?
Na kama hivi vitu vyote Tanganyika haina, je ni nani aliyepokwa sovereignity kati ya Tanganyika na Zanzibar ?
 
Hlo jibu lake lipo wazi kwa kila mwnye akili timamu,nchi ambayo hata kiongozi wake hatambulik kmataifa c usanii huo?????
Kwa mujibu wa muungano huu, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio maana hatambuliki kimataifa.

Hebu nijibu hili swali, hivi Scotland ni nchi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…