Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Ndio maana tuna wazanzibari katika bunge la Tanganyika? Ndio maana tuna mawaziri wazanzibari katika wizara za Tanganyika? Mnafik ni wewe. Na uliyejaa chuki dhidi ya kile unachokiita Tanganyika ni wewe. Ni haki gani ambayo mzanzibari ananyimwa katika serikali ya Tanganyika? Wakati huo huo kuna haki kibao mtanganyika hanazo huko Zanzibar lakini bado unalia na kumuita mtanganyika mbaguzi na mwenye chuki dhidi yenu! Hivi mnatuita machogo kwa sababu mnatupenda sana?

Wewe ni mnafik mkubwa uliyejaa chuki. Ubaya ni kuwa kuna watanganyika wana entertain chuki na unafik wenu kiasi kwamba hamtaki kuambiwa ukweli.

Amandla....
 
Makamu wa Rais yuko sahihi. Zanzibar ilikoma kuwa soverign state. Ikapoteza baadhi ya vyombo muhimu (fedha, majeshi na uraia) kwa Tanganyika. Wakapewa kuwa autonomous state (mambo ambayo nchi nyingine huita provinces - SA, au states huko USA. Zina magavana, mabunge, na hata mahakama zao. Zanzibar iliingizwa kwenye mambo 9 ya muungano ili Tanganyika iyadhibiti. Ndicho anachomaanisha Makamu wa Rais.

Kubadilisha jina la nchi na kuiita Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuwa ni kuzaliwa kwa taifa jipya - ilikuwa ni kuichukua Zanzibar!! Burma ilitwa Myanmar, Swaziland imeitwa Eswatini na hata Afghanistan imeitwa Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan.

Je, Tanganyika ilipoteza nini katika muungano??
 
Huu Muungano una kasoro nyingi za kimuundo ndio maana unakuwa na changamoto nyingi sana. Kibaya zaidi ni kuwa imekosekana nia ya dhati katika kutatua changamoto hizo ndio maana imebaki kuwa kama ndoa ya wanandoa waliochokana lakini wanaogopa talaka.
 
Ukifikiri kwa mawazo huru bila kukariri;

1. Zanzibar haina uwezo wa kuamua lolote kama Tanzania haikubali (Tanzania ni kubwa kuliko Tanganyika au Zanzibar na ni Tanganyika ukiongeza mambo ya Muungano kihalisia).
2. Serikali ya Tanzania inashughulikia mambo yote yaliyokuwa ya Tanganyika pamoja na yale yaliyokubaliwa kwenye muungano.
Tanzania ukitoa mambo ya Muungano unapata Tanganyika.
 
Lini Zanzibar walipoteza?? Wao bado wanasomeka Zanzibar!
Ili kuwa dola kamili/ state, panatakiwa pawepo watu, Serikali, ardhi, na sovereignty/uhuru wa ndani na nje.

Zanzibar ina watu, Serikali, na ardhi ila haina uhuru wa kitaifa na kimataifa, kwa sababu kitaifa mfanya maamuzi mkuu ni Serikali na Bunge la JMT, wakati kimataifa Tanzania ndiyo yenye utambulisho. Pia ulinzi na Usalama ni jukumu la Tanzania.

Kwa hiyo Zanzibar siyo huru wala siyo dola kamili
 
Camalad paskali ndiyo maana tunataka muungano uvunjike why usitambue viongozi wetu wa kitaifa Zanzibar?.

Au hujui pasipo SUK nchi inachafuka?.
Wewe hauwatambui ila Rais wako anawatambua ndiyo maana week hii makamu wa pili wa rais wa Zanzibar alikuwa mkoani Tanga kwa ziara ya kichama na serikali akiweka jiwe la msingi kwenye miradi ya maendeleo pia kuimarisha chama.
 
Hilo liko wazi na halina mjadala, kwanza wana kauli yao eti ardhi ni ndogo, wakiruhusu wageni ardhi itajaa haraka although wageni wanaruhusiwa kununua apartment zilizo tayari ila si kununua ardhi.

Sheria za visiwani zinambana sana raia kutoka Tanganyika kuliko anayetoka ughaibuni, tena akiwa raia asiye na uwezo kimapato.

Huwa nasema wanaopiga kelele muungano uvunjike ni watu hohehae ila, wenye akili hawawezi ruhusu hilo, sababu mojawapo ni ule uwekezaji walioufanya Tanganyika, yaani Wapemba na waunguja wengi sana wamewekeza bara so, nani ataruhusu arudi kwao Pemba kuacha assets kibao kule chuchubani au mvuti?.
 
Wazanzibari wengi wanajuta kumfukuza Sultan na kuungana na Tanganyika. Tena wanaona yale mapinduzi ni kama yalipangwa na watu ambao si Wazanzibari. Sultan wa Oman angekuwa bado anatawala Zanzibar ingekuwa kama Muscat siku hizi. Utajiri wote wa mafuta ya Oman, Wazanzibari wameukosa. Wamebaki na umasikini na kuburuzwa na serikali ya JMT.
 
Wewe unaijua Zanzibar kuliko Masoud Othman ?? Be serious man .... Wasukuma na Zanzibar wapi na wapi !!

Masoud Othman kaongea ukweli ambao ninyi wengi wenu mmedanganywa na wengine hawataki kuusikia.
 
Kwa nini vibali vya maendeleo ya zanzibar vinatoka Tanganyika., mfano mduchu juzi kuhusu babara ya wete mkoani, kwann nje hakuna balozi yoyote kutoka zanzibar? Othman alimaanisha yote hayo
 
Waziri wa Ujenzi wa hiyo unayoiita Tanganyika ni Mpemba. Wabunge kutoka Zanzibar wana uwezo wa kuchangia jambo lolote katika Bunge la Tanganyika. Niambie kuna mawaziri wangapi watanganyika katika SMZ? Au katika BMZ? Wazanzibari hawafiki milioni tatu lakini kwenye hilo bunge la Tanganyika yenye zaidi ya watu milioni 58 wanapewa haki sawa na watanganyika bila kubaguliwa!

Amandla...
 
Kwa nini vibali vya maendeleo ya zanzibar vinatoka Tanganyika., mfano mduchu juzi kuhusu babara ya wete mkoani, kwann nje hakuna balozi yoyote kutoka zanzibar? Othman alimaanisha yote hayo
Umewahi sikia mahali kuna ubalozi wa Scotland, Wales, Northern Ireland, Catalonia, California, Texas, Kerala n.k.? Tangu lini umesikia barabara za Zanzibar zimeingia kwenye bajeti ya Tanganyika? Kama mnataka kuwa na balozi zenu vunjeni Muungano. Badala ya kuzunguka mbuyu mwambieni Rais wa JMT kuwa hamtaki Muungano, sio kujificha kwenye kile mnachoita kero. Pitisheni muswaada kwenye Baraza lenu la kusema kuwa hamtaki Muungano. Chama chake cha ACT Wazalendo kiweke kwenye ilani yake kuwa hakitaki Muungano. Shida kwani iko wapi? Fanyeni hivyo halafu muuone watanganyika wangapi watawabembeleza. Na mnaweza kukuta ndugu zenu wenyewe watawageuka.

Amandla...
 
Mkuu kipengele cha kwanza sio sahihi hata kidogo... Znz ina jiamulia mambo yake yote ambayo sio ya muungano na mengine kadhaa mfano mdogo swala la ardhi wameamua kuwa sideline wa tanganyika, znz walijiamukia kuwa na serikali ya maridhiano, znz walijiamulia kuwa na vitambulisho vya mkaazi ambavyo ww mbara huwezi pewa ng'oooo lkn huku bara vya NIDA ndivyo ivyo ivyo tuna gawana nawo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…