Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?



Watanganyika na sisi tunataka Rais wa serikali yetu na muondo wenye hazi sawa na huu SMZ hivyo tu. Khalafu huyu Rais wa JMT aendelee na majukumu yake ya JMT.
 
Kuna hatari siku watu watachoka kuvumiliana kwenye mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar. Unakuta kiongozi mkubwa makamu wa kwanza wakati wote ana maoni ya kuudhi au kama huyo masudi saa zote anapinga muungano na anafanya mambo tofauti na sheria na taratibu. Amekua anaingilia mara kwa mara shughuli ya serikali ya muungano mambo ya nje kwa kutuma salamu kama zanzibar kwa viongozi wa dola za nje.
 
Tanganyika ipo na imevaa au kujivalisha ngozi ya kondoo.

Inakuwaje Almasi na Dhanabu hazipo katika mahesabu ya Muungano.......ila mafuta yaliopo kizani ni ya Muungano. Wahafidhina mnaofaidika na upigaji katika Muungano ,leteni jawabu inakuwaje Almasi ni huko huko tu ?
Hakuna Muungano kuna kizungunkuti.
Wajinga walikuwepo Zamani- Mzanzibari mkaazi hivi yupo Mtanzania Mkaazi Huko ??
 
WaZanzibari wapo pamoja isipokuwa vibaraka ,sijui vibaraka maana yake nini ? Ila one day Yes the Voice of Zanzibarians will be heard everywhere.
 

Mafuta mliambiwa Zanzibar mfanye tafiti na mchimbe mafuta yenu. Sijui kwa nini hamtoi mrejesho mmefikia wapi? Msigwa wa habari maelezo aliahidi kuleta mtaalamu wa kero za muungano. Atakapo mleta na amini atatolea ufafanuzi huu wa hii hazina ya raslimsli ya mafuta yenu Wazanzibari.
 
Mkuu Shocker , sijui mwenzetu unaishi kwenye karne ya ngapi, gesi na mafuta viliishatolewa kwenye mambo ya muungano, hivyo Zanzibar iko huru kuchimba hayo mafuta yake ya kwenye kinibu, ila mafuta ya kwenye bahari ni mali ya muungano. Kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya Tanzania hakuna mpaka wa nchi nyingine yoyote iitwayo Zanzibar, bali Zanzibar ni sehemu ya JMT.
P
 
MPE walau heshima take ya Umakamu was Rais.

Ficha chuki zako binafsi. Hebu pitia tena hayo maandishi yako, yahakiki vizuri wewe in mwandishi Mkongwe uone ulivyotumia maneno ya kubeza.

Nadhani umenielewa
Sawia mkuu. Huyu anaheshima yake halafu ni mwanasheria mbobezi sasa Pascal anamkejeli!!!!!!!!! Huwa nashaka na uelewa wa Pascal vilevile.
 
Sawa kabisa uliyosema. Kuanzia jina, bado kuna nchi inayoitwa Zanzibar yenye Rais, mawaziri, bendera na wimbo wa taifa, na kila kitu kinachoashiria serikali, kama vile bunge. Lakini thubutu kutaja 'Tanganyika' kwa maana ya nchi ya zamani iliyokuwa ikiitwa hivyo, utachukuliwa kuwa una yako ambayo si mazuri kwa nchi. Tanzania imekuwa na marais wawili kutoka Zanzibar: Mwinyi na Samia. Mawaziri kibao na kwa wafanyakazi wa kawaida hao ndio usiseme. Huku bara mtu anaweza kukuuliza unatoka wapi ukasema Zanzibar na hiyo itachukuliwa sawa na yule anayejibu anatoka Kigoma au Songea. Hakuna cha kushangaa kwa kuwa hakuna nchi 'Tanganyika'. Lakini jee mtu wa Bara anaweza kuwa Rais, au waziri, au mbunge wa Zanzibar? Hiyo haiwezekani kabisa. Mfanyakazi wa kawaida tu wa serikali anasumbuliwa sana kufanya kazi Zanzibar. Nawafahamu wenzagu wawili waliowahi kufanya Zanzibar. Wanasema walikuwa wakihojiwa sawa na Mkenya au mtu wa taifa jingine. Kwa hiyo ukweli ni kwamba Tanganyika ndiyo ilikufa lakini Zanzibar ilibakia.
 
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya Muungano. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.
Mkuu Pascal, kwa nia ya kujifunza naomba unielekeze;

Umesema Z'bar ni sehemu ya JMT, nakubali, hata Shinyanga ni sehemu ya JMT, kadhalika Gairo na kwingineko. Kila sehemu ya JMT inatambuliwa kwa jina la mfumo kiutawala, haiitwi tu sehemu ya JMT. Kuna mikoa, wilaya n.k

Z'bar kwa kuwa si nchi na ni sehemu ya JMT, naomba utambulisho wake kiutawala.
 
Makamu wa rais ZNZ inaonekana hafurahishwi na muungano
Pamoja na kutofurahishwa, hakuna lolote analoweza kufanya. Akae atulie atuachie Tanzania yetu.
Nashangaa sana, tukienda Zanzibar ni kama tunaenda nchi nyingine tiofauti. Huku bara hakuna hata mmoja anayehangaika na ndugu zetu hawa. Nini hasa shida yao? Kwanini hatupendani?
 
Serikali ya SMZ siyo jambo la Muungano.
Katiba yako ya JMT ilicheza ngoma isiyo yake kuweka muundo wa SMZ ndani yake, Ndiyo maana Wazenji hawakujali kuwa katiba ya JMT inatambua muundo wa zamani wa SMZ wa uwepo wa waziri kiongozi huko Zenji wao wakaweka makamu wawili wa rais instead.

Ndiyo maana tunataka katiba mpya ambayo inaondoa dicrepancies hizi otherwise ni kichekesho katiba mama itambue muundo wa SMZ ambao haupo, ushabadilishwa tayari na wazanzibar wenyewe.
 
Kama ulinisoma vyema kule mwanzo, nimesema muungano wetu ni very unique, ni muungano wa union kwa upande mmoja wa kimataifa na ni muungano wa federation kwa upande wa pili ndani ya muungano.

Hivyo japo Zanzibar sio nchi, haina sovereignity yake, haina dola, haina sarafu, haina mipaka ya kimataifa, haina Jeshi, haina polisi lakini ina autonomy yake kwa mambo yake ya ndani yasiyo ya muungano.

P
 
Kasema Uongo wapii na ukweli hamtaki wabara ,wewe na OMO ww ndio msomi zaidi kushinda OMO ebu wacha kuwashwa washwa Paskali.
 
Sawia mkuu. Huyu anaheshima yake halafu ni mwanasheria mbobezi sasa Pascal anamkejeli!!!!!!!!! Huwa nashaka na uelewa wa Pascal vilevile.
Sijamkejeli nimesema amesema uongo. Kwanini kiongozi Mkuu wa nchi kati ya wale Viongozi wetu wakuu 6 wa kitaifa waseme uongo ?. Ukiishakuwa ndani ya serikali, unafungwa na kifungo cha a Collective responsibiliy clause. Huwezi kuuzungumza uongo mkubwa hivi Wazalendo tukanyamaza. Mkuu huyu anahitaji semina elekezi.
P
 
Kasema Uongo wapii na ukweli hamtaki wabara ,wewe na OMO ww ndio msomi zaidi kushinda OMO ebu wacha kuwashwa washwa Paskali.
Mkuu mfufuka, Resurrection , hapa hatuzungumzii usomi wa mtu, zungumzia hoja iliyopo mezani usilete mipasho. Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda Tanzania, nchi zote mbili zilipoteza sovereignity zake. Sii kweli iliyopoteza ni nchi moja tuu ya Zanzibar.

Mtu unaweza usiwe msomi na ukawa na hoja mujarab kuliko Wasomi.

P
 
Brother hebu achana na mambo yaliyoko kwenye makaratasi fikiria hili swala la muungano kwakutumia fikra na utashi wako alafu jiulize je yanayofanyika nakutendwa kwa pande zote mbili ndivyo ilivyo na inavyopaswa kua au kuna walakini unaolindwa kwa nguvu ya dola na wanasiasa wanufaika?.
 
Dawa ya jambo hili ni maamuzi magumu yafuatayo: Kutoa notisi ya siku 90 wazanzibara wote walioko ZANZIBAR warudi Tanzania bara, na Wazanzibari wote walioko Tanzania bara warudi wZanzibar!!. Kila sehemu ya Jamhuri ya Muungano ione itawahifadhi vipi watu wao. Baada ya siku hizo 90, itolewe notisi ya siku 90 ya kutafakari, siku hizi zikiisha iitishwe kura ya maoni Tanzania bara na kule Zanzibar watu waamue aidha kuuvunja muungano au kuuimarisha kwa kuwa na nchi moja ya Tanzania yenye serikali moja tu! Hakuna cha serikali ya Zanzibar kama ilivyo hakuna serikali ya Tanganyika!! Matokeo ya kura hiyo yaheshimiwe!! Tanzania visiwani iwe mikoa miwili tu ya Tanzania!!
Hawa wazenji wametuchosha!! Wapemba wamejaa kila kona ya Tanzania bara lakini hawaridniki !! Waondoke warudi kwao!!!
 
Na alimasi na dhahabu ni ya kinanani,mbona mnaibania ndio muungano huo,eti kwenye bahari ni ya Muungano , Sasa niwaulize mnaogopa nini kuwa na Tanganyika yenu ?
Sijawahi kusikia jibu mlikurupuka miaka ya Baba haambiliki kisha mkaufyata,mnaona aibu kuwa na Tanganyika ? Au mnaogopa KuCongoana au KuSudaniana.

Kigoma kwake Mtwara kwake ndivyo mnavyowadanganya watu ili muzidi kuchomeka mirija,maana ukiangalia Tz kama hakuna wanaomaliza vyuo,kuna watu tokea tupate Uhuru wanazeekea ndani ya serikali na kurithishana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…