Pre GE2025 Kuhusu nafasi ya Urais ndani ya CCM: Kinana amedanganya, na kwa vyovyote hana dhamira njema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kinana amesema uwongo kuwa eti CCM imekuwa na utaratibu wa kutoruhusu kuwepo na ushindani ndani ya CCM wa kumpata mgombea wa chama kwenye kiti cha Urais pale ambapo Rais aliyepo madarakani hajamaliza vipindi viwili vya Urais wake. Amesema hayo akimlenga Rais wa Sasa.

Uwongo wa Kinana upo katika ukweli ufuatao:

1. Huko nyuna hakujawahi kuwa na Rais wa kiolpindi cha dharula. Hivyo hakujawahi kuwa na desturi ya kumpitisha Rais wa Dharula bila ya kura za wajumbe wa vikao vikuu vitatu vya CCM. Kifo cha Rais Magufuli ndiyo ilikuwa dharula ya kwanza kwa Taifa.

2. Rais wa sasa hakuwahi kupigiwa kura na wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu kuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha Urais. Utamaduni anaousema ni kwa Rais aliyepo madarkani ambaye kipindi chake cha kwanza cha Urais alichaguliwa na vikao vilivyotajwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM. Lakini siyo kwa mtu ambaye hajawahi kupigiwa kura hata moja na wajumbe wa vikao hivyo kwa nafasi ya Urais.

3. Rais wa sasa ni Rais wa dharula. Katiba, kwa kuzingatia ukweli kuwa nchi isiingie kwenye mkanganyiko pale inapotokea dharula ya kifo cha Rais akiwa madarkani, ndiyo inayotamka ni nani awe Rais wa dharula katika kipindi hicho cha dharula. Huyu anakuwa Rais wa dharula mpaka wakati ule ambapo chama kitampata mtu ambaye vikao vya chama vitamchagua mtu ambaye wanataka awe ngombea wa Urais kupitia chama chao. Kulazimisha Rais wa dharula, ambaye hakuna uhakika kama chama kinaridhika awe mgombea wao kwa nafasi ya Urais, ni kukiuka misingi mikuu ya demokrasia.

Kwenye nchi zenye watu wenye akili timamu, ambako viongozi nao wana akili timamu, siku zote viongozi hutafuta uhakika wa kutaka kujua kama watu wanaotaka wawaongoze wanataka waongozwe na viongozi husika. Watawala wanapojua kuwa wananchi wao wanawataka wawaongoze, inawapa nguvu viongozi katika utendaji wao wa kazi kwa sababu wanatambua kuwa nyuma yao kuna umma mkubwa wa watu unaowataka wao viongozi wawe mbele yao katika utendaji wao wa kuyaongoza mataifa yao. Huku kwetu, sijui ni ujinga, upunguani au ushetani, watawala wanaogopa wananchi kuwadhihirishia viongozi kama wanawataka wawe viongozi wao au la. Ndiyo maana akina Kinana wanatamka wazi kuwa ndani ya CCM hakutakuwa na nafasi kwa wanaCCM kuthibitisha kama wanataka aliyekuwa Rais wa dharula, sasa awe Rais wa kuchaguliwa au apumzike na kupewa heshima yake ya kuiongoza nchi katika kipindi cha dharula.
Ngoja tuone !
Ila inafikirisha sana !
Pia Kinana ametumia neno “ sio dhambi “ kama atapitishwa !
Hiyo ina maana lipo fukuto Chamani au labda ni mawazo yake tu !
Ngoja tuone !!
 
Hapo Namba 2 si sawa. Magufuli na Samia walipitia mchakato mmoja hadi Magufuli akawa Rais. Kura alizopata Magufuli kwenye Urais kwenye ile karatasi alikuwepo pia Samia. Kuna watu walimchagua Magufuli kwa sababu tu ya uwepo wa Samia. Si sawa kusema eti hakupigiwa kura.
 
Rais wa sasa ni Rais wa dharula. Katiba, kwa kuzingatia ukweli kuwa nchi isiingie kwenye mkanganyiko pale inapotokea dharula ya kifo cha Rais akiwa madarkani,
Ni mgombea mwenza hata 2020 aligombea kwa tiketi moja na JPM na walikua wote kwenye ballot paper. So sio Rais wa dharura bali Makamu wa Rais ambaye alipigiwa kura na wananchi.

Sasa kama aliaminiwa awe number mbili, yule top akifariki kivipi asiaminiwe? Kama wao walimchagua kwa huruma za muungano au gender balance its up to them ila katiba lazima iheshimiwe.

Ni hivi, Samia ndio mgombea wa Ccm 2025 kwa sababu ya precedence ya 2020 na 2010, kama JPM anger uhuru Membe achukue fomu hata leo wangepata confidence ya kupambana dhidi ya samia.

Sasa kama vile wao walivyokataza asichukue mtu fomu 2020 basi ndio wembe ule ule atautumia samia kufukuza wote wenye kutaka fomu ya Urais.
 
Hiyo ina maana lipo fukuto Chamani
Fukuto gani, si walimchagua kuwa mwenyekiti wao kwa kura zote za ndio, sasa nani wa kumchallenge Mwenyekiti? Ana uwezo wa kufukuza kamati kuu nzima na hamna pa kumpeleka. Ndugai huyo hapo alipojaribu kumpinga alipata nini? Na leo keshasahaulika kabisa.
 
Hapo Namba 2 si sawa. Magufuli na Samia walipitia mchakato mmoja hadi Magufuli akawa Rais. Kura alizopata Magufuli kwenye Urais kwenye ile karatasi alikuwepo pia Samia. Kuna watu walimchagua Magufuli kwa sababu tu ya uwepo wa Samia. Si sawa kusema eti hakupigiwa kura.
Usipotoshe.

Mchakato ndani ya vyama kila mwanachama anachukua fomu mwenyewe hachukui na mgombea mwenza.

Akishapitishwa na chama anatakiwa sasa achague mgombea mwenza kuendana na matakwa ya tume ya uchaguzi ya Taifa na ndio kilichofanyika.

Kilichombeba Magufuli ni historia yake ya kiutendaji kama waziri katika wizara mbali mbali.

Rekodi ya Magufuli pekee ilitosha kumbeba bila kujali nani alikua mgombea mwenza.

Kama alivyowahi kusema mwenyewe kuwa yeye alipenda Mwinyi awe mgombea mwenza ila Chama kwa sababu zao wenyewe wakampendekeza Samia.

Hivyo swala la Samia kumbeba Magufuli hapo liondoe bali itambulike kuwa Magufuli ndie alimbeba Samia.

Hata akikataa ila ukweli ndio huo.
 
Ni mgombea mwenza hata 2020 aligombea kwa tiketi moja na JPM na walikua wote kwenye ballot paper. So sio Rais wa dharura bali Makamu wa Rais ambaye alipigiwa kura na wananchi.

Sasa kama aliaminiwa awe number mbili, yule top akifariki kivipi asiaminiwe? Kama wao walimchagua kwa huruma za muungano au gender balance its up to them ila katiba lazima iheshimiwe.

Ni hivi, Samia ndio mgombea wa Ccm 2025 kwa sababu ya precedence ya 2020 na 2010, kama JPM anger uhuru Membe achukue fomu hata leo wangepata confidence ya kupambana dhidi ya samia.

Sasa kama vile wao walivyokataza asichukue mtu fomu 2020 basi ndio wembe ule ule atautumia samia kufukuza wote wenye kutaka fomu ya Urais.
Acha Ujinga, Magu ilikuwa Awamu yake ya pili,alipitia mchujo na kushinda.

Sa100 hajawahi pigiwa kura popote kabla, jambo Hilo ni LAZIMA lifanyike nw!!
 
Zilongwa mbali Zitendwa mbali 🐼
1000006218.jpg
 
Ndio ameishatuchagulia rais hivyo 2025,kwa katiba iliyopo hta CCM wakaweka njiwe bado litapita kwa kura nyingi zaidi ya asilimia 80%,
Sio litapita, sema watatangazwa kwa kura zaidi ya 80%. Kuna tofauti ya kupata na kutangazwa.
 
Acha Ujinga, Magu ilikuwa Awamu yake ya pili,alipitia mchujo na kushinda.

Sa100 hajawahi pigiwa kura popote kabla, jambo Hilo ni LAZIMA lifanyike nw!!
Hata zikipigwa kura ni kiini macho tu, atatangazwa kwa idadi ya kura azitakazo. Dhalimu magu ndio aliharibu heshima ya uchaguzi ndani ya chama chake na nchi hii.
 
Ndo Sa100 pia apitie mchujo, hakuna anaeungana na Magu katika wizi wa uchaguzi.

Hilo liko wazi binafsi nilipinga uchaguzi huo.

Magu tulimuunga mkono Kwa Uzalendo na uthubutu na uchapakazi.

Lazima wanachama waruhusiwe kuchukua fomu na mchujo ufanyike.
 
Ni mgombea mwenza hata 2020 aligombea kwa tiketi moja na JPM na walikua wote kwenye ballot paper. So sio Rais wa dharura bali Makamu wa Rais ambaye alipigiwa kura na wananchi.

Sasa kama aliaminiwa awe number mbili, yule top akifariki kivipi asiaminiwe? Kama wao walimchagua kwa huruma za muungano au gender balance its up to them ila katiba lazima iheshimiwe.

Ni hivi, Samia ndio mgombea wa Ccm 2025 kwa sababu ya precedence ya 2020 na 2010, kama JPM anger uhuru Membe achukue fomu hata leo wangepata confidence ya kupambana dhidi ya samia.

Sasa kama vile wao walivyokataza asichukue mtu fomu 2020 basi ndio wembe ule ule atautumia samia kufukuza wote wenye kutaka fomu ya Urais.
Nikikuteua wewe kuwa manager, na mwingine kama msaidizi wako, haimaanishi huyo msaidizi wako anafaa kuwa meneji bali ana uwezo wa kuziba pengo endapo katika hali ya dharula wewe huwezi kufanya mambo fulani au akatimiza majukumu yako wewe kama meneja kwa muda fulani tu kwa sababu wewe hupo.

Kimantiki ni kwamba wale waliomchagua Magufuli walikubali Magufuli kuwa Rais na Samia kuwa msaidizi wake, hawakumchagua Magufuli na Samia, wote kwa pamoja kuwa Marais. Msaidizi ni mtu anayepokea maagizo au maelekezo na siye anayefanya maamuzi ya mwisho.
 
Back
Top Bottom