Pre GE2025 Kuhusu nafasi ya Urais ndani ya CCM: Kinana amedanganya, na kwa vyovyote hana dhamira njema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Apitoe mchujo au usanii?
 
Mama Samia Suluhu Hasan, huwa anapita humu. Bila shaka atazingatia ushauri wako bora kabisa, huku akiwapuuza chawa wanaotaka aminye demokrasia ndani ya chama. Na kama mimi kumshauri pia kwa kulinda heshima yake na kulinda uislamu wake ningemshauri aache kugombea 2025 alichopewa na Mungu bila kukitaabikia kinamtosha. Isipokuwa akina Lucas Mwashambwa.
 
Apitoe mchujo au usanii?
Usanii, sawa kabisa, kama tu usanii wa Uchaguzi wa kura ya Urais ilhali inajulikana akitangazwa hakuna Rufaa popote.

Huo usanii ufanyike.

HOFU ya nini ilhali anajua atapita?
 
Umeongea vyema sana mkuu, kuna kipindi waziri mkuu wa Uingereza mama Susan May aliitisha uchaguzi wa mapema kutafuta kuungwa mkono zaidi, na hata waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwahi fanya..........sasa unajiuliza hawa viongozi wa wadanganyika wanahofia nini kuingia kwenye mchakato wa kutafuta kuungwa mkono? ngozi nyeusi tuna matatizo ya kiasili, si bure....

Na ukumbuke bi hadija hakuwahi kupitishwa na mchakato wa uchaguzi ndani ya chama chake kuwania nafasi ya urais.​
 
Hongera kwa andiko elimishi na la ukweli mtupu. Kwa andiko hili umenipa matumaini kwamba bado kuna wa -Tanzania wenye busara!!!!!
 
Kwenye karatasi ya kura alikuwepo JPM na Samia sio kwamba alikuwepo JPM pekee so kusema alichaguliwa JPM sio samia inakuwa sio sawa.

Pili huwezi sema umemteua makamu eti kuziba pengo kwa muda tu ilihali katiba ipo wazi ukisafiri, ukiugua, au kufariki basi Makamu ndio anakua Rais!! Huwezi risk kiasi hiko.

Nachoweza kusema, next time mtakua makini kwenye kuchagua wagombea wenza na hili ni mpaka chadema walimuweka yule Said Issa kama makamu mwenyekiti. At some point Lissu alikua abroad na Mbowe alikua jela, yule jamaa akawa mwenyekiti kwa almost mwezi mzima na ilihali hamna anachoweza!!
 
Na huo ndio ukweli mchungu !
🙏🙏
 

Samia hakupigiwa kura hata 1 kwaajili ya kuwa Rais. Kila aloyempigia kura Magufuli, alipiga kura ya Magufuli kuwa Rais na Samia kuwa Makamu wa Rais. Nikisema kuwa wewe unafaa kuwa meneja wangu, na Mwashambwa kuwa makamu wako, haimaanishi Mwashambwa anafaa kuwa meneja, ila ina maana ninaona kuwa anafaa kufanya kazi kwa maelekezo yako. Au katika hali ya dharula ana uwezo wa kuishikilia hiyo nafasi wakati natafuta replacement yako.
 
Acha Ujinga, Magu ilikuwa Awamu yake ya pili,alipitia mchujo na kushinda.

Sa100 hajawahi pigiwa kura popote kabla, jambo Hilo ni LAZIMA lifanyike nw!!
Jamaa yenu si aliprint fomu moja tu? Hatutaki arudie mtu Kama yule na Mungu asaidie
 
Hoja namba mbili izingatiwe ,japo wao katiba inaruhusu kupingana ila hifanya mazoea

Kimsingi ni patashika apumzika kwa amani ,kakayangu BERNARD membe
 
Hivi kweli Samia ambebe Magufuli! Hata mtandaoni tu Samia watu hawamkubali Ukiingia mtandaoni X utaona kabisa people are not ready kwa huyu Mama!
 
Hauna akili.
 
Rais ni Samia na formality zitafuatwa kama kawaida.

Na Kwa kutumia huo utaratibu inaweza kumpa Samia miaka 15 ya kuwa Rais unless yeye atumie busara maana anaweza sema awamu hii ni ya dharura hivyo haiko rasmi.

Je mko tayari? Usiempenda kaja.
 
Rais ni Samia na formality zitafuatwa kama kawaida.

Na Kwa kutumia huo utaratibu inaweza kumpa Samia miaka 15 ya kuwa Rais unless yeye atumie busara maana anaweza sema awamu hii ni ya dharura hivyo haiko rasmi.

Je mko tayari? Usiempenda kaja.

Siyo suala la mtu kukubali au kukataa bali ni suala la katiba.

Katiba iliishatamka kuwa ikitokea Makamu wa Rais amekuwa Rais kutokana na dharula iliyotokea, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Urais, na akichaguliwa kuwa Rais, hataruhusiwa kushikilia zaidi ya vipindi viwili, ile ya Urais wa dharula, nayo ikihesabiwa kama kipindi kimoja. Hivyo Samia katiba inamruhusu kugombea nafasi ya Urais, na akichaguliwa, hicho ndicho kipindi chake cha mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…