Pre GE2025 Kuhusu nafasi ya Urais ndani ya CCM: Kinana amedanganya, na kwa vyovyote hana dhamira njema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Formality zitafuatwa,kwani wewe shida Yako ni nini? Mbona Kinana amesema Hawaoni shida Samia Kugombea mara ya pili au Kuna sehemu Katiba inasema successor wa kifo hatKmakiwi Kugombea?

Kama ni formality subiria mda zitafuatwa kama ilivyokuwa wakati wanamchagua kuwa Mwenyekiti wa Chama.
 
Kama kuna mtu atasema Rais Samia haruhusiwi au hatakiwi kugombea au kuendelea kuwa Rais, basi labda huyo mtu ni punguani. Jambo la muhimu apite kwenye njia iliyonyoka na safi.

Hapa watu wanalaani kauli ya kinafiki ya Kinana ya kusema eti fomu ya mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais itachapishwa moja, yaani maana yake ni kuwa hakuna mwanaCCM atakayeruhusiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM. Kwanza hilo likitokea litamtia doa Rais Samia ambaye angependa kufanya tofauti na madikteta waliotangulia kwenye upande wa demokrasia. Kama Rais Samia atakubali hilo, hata zile R zake 4 zitaonekana ni unafiki.

Ndani ya CCM, hata kama wakichapisha fomu 100, siamini kama wapo watakaomshinda mwenyekiti wao katika uteuzi wa nafasi ya mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM.

Rais Samia, binafsi naamini, kuna majitu maovu, kwa dhamira zao mbaya, wanapenda kumpitisha kwenye njia chafu ili waonekane kuwa wao ndio walimwezesha kuwa Rais, na akiwa Rais waendelee kuwa na nafasi ya pekee kiasi cha kutoguswa hata wanapoendelea na uovu wao au ili waendelee kupata upendeleo.
 
Hakupigiwa kura na wajumbe wa vikao vitatu vya juu vya CCM.

Mbona inaeleweka!??
Unashindwaje kuelewa hapo wewe Mzee Kijana !!??
 
Ndugu zitto junior hapa ndugu Bams anazungumzia mchakato ndani ya CCM.
Mh. Samia hakuwahi pitia mchakato ndani ya CCM.
 
Ndugu zitto junior hapa ndugu Bams anazungumzia mchakato ndani ya CCM.
Mh. Samia hakuwahi pitia mchakato ndani ya CCM.
Mchakato wa ndani si aligombea uenyekiti na hao hao wajumbe wakampa 100% ya kura kipi kitabadilika wamnyime urais ila wamuachie uenyekiti, is it even possible?

Udhaifu wa katiba ya chama sio kosa la Samia
 
Lakini je anayonafasi ya kuweza kufanya mabadiliko ktk kuboresha?
 
Mchakato wa ndani si aligombea uenyekiti na hao hao wajumbe wakampa 100% ya kura kipi kitabadilika wamnyime urais ila wamuachie uenyekiti, is it even possible?

Udhaifu wa katiba ya chama sio kosa la Samia
Yeye mwenyewe anazungumzia Reform. Kama kuna mambo yapo hovyo kwenye katiba yao, mazoea au kanuni, yeye ana mchango gani katika kuyarekebisha?

Hata mimi siamini kama kuna mwanaCCM wa kumshinda. Lakini kama una uhakika wa kushinda hata ukishindanishwa, una haja gani ya kupitia njia za panya kuufikia ushindi?
 
Mkuu hata akichukua fomu peke yake bado kuna kura za ndiyo na hapana, so sio kwamba hakuna mchakato ila hata huko US Biden hana mpinzani maana amesema anagombea tena.
 
Hujamwelewa mwandishi,mwandishi kasema hakuna mchujo uliompitisha samia kwenye chekecheo la kugombea kuteuliwa na ccm,kwa sababu samia yeye aliteuliwa tu na jpm.
 
Watu wengi sana mna elimu,lkn kwa nn mnaonyesha ujinga mkubwa!?.
 
Watu wengi sana mna elimu,lkn kwa nn mnaonyesha ujinga mkubwa!?.
Ujinga ni upi? Hata USA Biden hashindanishwi na mtu maana ni incumbent.

Kwa mnaodai Samia hakuchaguliwa not true maana alikuwepo kwenye ballot.

Kwa hoja ya kwamba CCM haikumpitisha , aligombea uenyekiti na alipata kura zote za NDIO, sasa legitimacy ipi hiyo ya kisiasa na kisheria asiyokuwa nayo?

Kwa hili mnamuonea bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…