The introvert
JF-Expert Member
- Sep 15, 2023
- 1,508
- 3,136
Anaandika Malisa GJ
Kuna wakati niliwahi kuandika hapa kuwa real estate ya bongo ni pasua kichwa, nikacompare bei ya nyumba Atlanta GA, zikazidiwa bei na baadhi ya nyumba za Dar. Yani ni Futuhi. Nyumba ya Philadelphia inazidiwaje bei na nyumba ya Kimara Temboni? Kweli bongo nyoso.
Anyway, hii video nimeirepost kutoka kwa @mbowejames akicompare bei ya nyumba Dar na Nairobi, Kenya. Nyumba ya kwanza ipo Nairobi, Ruiru mita 100 tu kutoka barabara kuu ya lami ya Thika. Angalia muundo wa nyumba, angalia touch za finishing, angalia facility zilizopo na executive neighbourhood. Nyumba hiyo inauzwa kwa KES 24M sawa na TZS 480M. Halafu video ya pili ni jumba la kifahari lililopo Goba linalouzwa kwa TZS 680M 😂.
Yani ukiuza nyumba ya Goba unaenda kununua hiyo nyumba ya Nairobi na unabaki na chenchi ya 200M. Najua hii post itawapandisha madalali sukari, lakini ukweli ni kwamba tunahitaji regulatory body kwenye real estate ya bongo. Uholela umekua mwingi sana.
Naposema real estate namaanisha kuanzia bei ya ardhi (mashamba & viwanja), bei nyumba na gharama za nyumba za kupangisha. Tunahitaji regulations kwenye hili, maana huko duniani tunaonekana kituko. Nyumba ya Tegeta kwa Ndevu inazidi bei nyumba ya Calgary Canada? Futuhi.!
View: https://www.facebook.com/share/v/1EKfCKaumQ/