Kuhusu sakata la G55 CHADEMA, Mbowe anahusika kwa asilimia 100

Sumbaye

Member
Joined
Apr 26, 2025
Posts
59
Reaction score
77
Wataalamu wa historia wanasema historia hutuambia kwa nini tupo hapa. Nimelazimika kutafakari na kurejea matukio mbali mbali yanayomhusu Mwenyekiti Mbowe kabla ya kupumzishwa na wanachama kwenye nafasi ya wenyekiti wake. Nimerejea matukio mbali mbali hususani baada ya mwenyekiti Mbowe kutoka Gerezani na kuibukia Ikulu, mwenendo wa vikao vya maridhiano, mwenyekiti Mbowe kuanza kuwashughulikia wajumbe wa kamati kuu waliopinga mwenendo wa maridhiano kama Mch Msigwa, Lema, Lissu na Heche kwenye kamati kuu na kwenye chaguzi za Chama. Nimelazimika kurejea hotuba yake aliyotoa akiwa mwanza vile vile. Nikiwa naendelea na tafakuri nikakumbuka namna alivyopambana kuhakikisha Lissu hagombei uenyekiti wa Chama baada ya kumwekea kivuli chake kwenye nafasi ya umakamu, mpaka alipowaita maaskofu wakae vikao vya upatanishi. Muda huo mwenyekiti Mbowe alikuwa hajatagaza kugombea uenyekiti. Baada ya jitihada zote za kumzuia Lissu kugombea kugonga mwamba, hatimaye alishawishiwa na wanachama kama kawaida yake kutangaza nia ya kugombea. Alitangaza nia akiwa anavuja jasho kubwa sana. Baada ya tukio la kutangaza nia, tulishuhudia pia matukio mengi yanayomhusu yeye mwenyewe kumshambulia Lissu au wafuasi wake. Nimerejea interviews kadhaa zake yeye mwenyewe na za wafuasi wake kama Kina Yericko Nyerere, Daniel Naftal nk.

Tumeshuhudia pia nguvu kubwa ya rushwa siku ya uchaguzi ikiwa ni mwendelezo wa njia za kuhakikisha anashinda na hivyo aliamini anashinda kwa asilimia zote. Siku ya uchaguzi tukashuhudia uchaguzi bora sana wa huru na haki uliomstaafisha na akatoa hotuba ya kishujaa sana tukadhani ni mzee ambae amekubali Chama kiongozwe na vijana aliowalea.

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, baada ya uchaguzi tukaanza kuona vituko vya Mchome ambaye ni kijana wa mbowe na sakata lake la akidi, na baadae likaibuka kundi la G55 ambao zaidi ya asilimia 70 walikuwa wafuasi wa Mbowe kwenye uchaguzi mkuu wa Chama. Nirudia pia kisoma waraka wao juu ya No reform, No election, nikasikiliza pia hotuba ya Mwenyekiti Mbowe juu ya No reform, No election.

Kuna mambo mengi sana ambayo ukiwa unatumia milango yote ya fahamu, ukirejea matukio yote, huwezi kumuondoa Mbowe kwenye sakata la G55 labda tu Ukiziba milango ya fahamu unaweza kudhani Mbowe amepumzika. Nalazimika tusema Mbowe bado yupo kazini. Kama tukimjengea nia njema, kama Mbowe Angelikuwa na uchungu na Chama alichokijenga kwa miaka zaidi ya 20, kama mzee wa chama na mjumbe wa kudumu wa kamati kuu alikuwa na anayonafasi ya kuwazuia G55 kuendelea na mipango yao kwa simu moja tu na wangeacha mara moja kwa sababu wanachafua na kuharibu legacy yake aliyojenga miaka mingi. Kama mzee wa chama na mtu mwenye uchungu na Chama tunatamani angefanya hivyo ila bahati mbaya hajafanya hivyo mpaka leo.

Hivyo kwa kurejea matukio yote hayo, nalazimika kusema Mbowe anahusika kwenye sakata la G55 na matukio haya yanatuambia kwa nini Hali ilivyo sasa chadema juu ya viongozi wakuu na harakati za kundi la G55.

Wasalaaam
 
Mbowe ni tapeli. amewalaghai watz kwa zaidi ya miaka 20. Yeye na genge lake wameshafeli sana! Mungu Yuko upande wa haki. Haki itatamalaki. This year
 
Kitendo Cha mbowe kukaa kimya na kukaa pembeni inaonyesha hakuipenda chadema kwa dhati..
 
Mbowe ni tapeli. amewalaghai watz kwa zaidi ya miaka 20. Yeye na genge lake wameshafeli sana! Mungu Yuko upande wa haki. Haki itatamalaki. This year
G55 wanachafua legacy ya Mbowe. Kwa nini anawaacha wafuasi wake waendelee kuhujumu chama, ikiwa bado anakipenda chama chake?
Kitendo Cha mbowe kukaa kimya na kukaa pembeni inaonyesha hakuipenda chadema kwa dhati..
Ni kweli.
 
Yan Chadema mtanyosheana vidole Hadi siku mtoboane macho kudadeki ....
😂😂😂
 
Yeyote mwenye akili timamu analijua hilo.
 
Kwahiyo, way forward unayoishauri kwa Chadema ni ipi? Kama hauna, mimi nakupa ushauri mzuri tu; MFUKUZENI MBOWE CHADEMA! Ahahahahaha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…