Kuhusu sakata la G55 CHADEMA, Mbowe anahusika kwa asilimia 100

Kuhusu sakata la G55 CHADEMA, Mbowe anahusika kwa asilimia 100

Kwani Lisu alipokuwa anamtukana Mbowe na kuongea na taifa wakati hajawa mwenyekiti alifuata utaratibu upi.Aliyeanzisha utomvu wa nidhamu ni Lisu,anavuna alichopanda.Alimtukana sana Mbowe na kusema hata biashara zake hazina TIN vumilieni tu mjenge chama maneno ni biashara ya wanasiasa.
Lissu hajawahi kumtukana Mbowe. Lissu alileta hoja kuhusu mwenendo wa chama, mwenendo wa maridhiano, mabdiliko ya msimamo wa mwenyekiti baada ya kutoka gerezani nk. Hayo yote hayakuwa matusi. Kama ambavyo mwenendo wake ulikiuka falsafa ya chama, tumewaona marafiki zake CCM wakimpigia kampeni awe mwenyekiti kwa awamu nyingine. Ni lini mpinzani wako anakupigia kampeni ya kuwa mwenyekiti?

Haya yote yanathibitishwa na matukio yote ya wafuasi wake baada ya uchaguzi. Haihitaji hadubini kujua Mbowe ametutapeli muda mrefu.
 
Ni kweli. Ametudanganya muda mrefu sana. Wanachama walichelewa kushtukia.
Muda wao umeisha kama unaweza kutafakali kidogo tu tafakali siku ile mdude anakamatwa mbele yake mtizame kwamakini je kunakitu aliongea au kufanya? Wenda mda wa vyama pinzani kuwa pinzani umefika kwasababu watu wamedanganywa sana
 
Tunafukuza aliowatanguliza, kama tulivyomshughulikia kwenye uchaguzi pamoja na mapesa yake kutoka kwa Samia
Mtaondoaje sumu kama hamumshughulikii anayeisambaza? Liambieni tu tawi lake limfukuze. Kama mnaogopa hata hilo bali limpe suspension. Na kama hiyo nayo mnaogopa, Katibu Mkuu atoe press release kuwa Mbowe ndio yuko nyuma ya G55 na ni msaliti wa CDM. Au Kamati yenu ya Maadili imuite ili akajieleza kuhusu hizi shutuma. Ukweli ni kuwa nyinyi kama bullies wote, ni cowards. Mnaweza kuwashughulikia vidagaa kama wakina Sigrada na Mrema lakini mnagwaya kulishughulikia papa.

Unless kama nyinyi ni mawakala wa CCM na nia yenu ni kuibomoa CDM.

Amandla...
 
Lissu hajawahi kumtukana Mbowe. Lissu alileta hoja kuhusu mwenendo wa chama, mwenendo wa maridhiano, mabdiliko ya msimamo wa mwenyekiti baada ya kutoka gerezani nk. Hayo yote hayakuwa matusi. Kama ambavyo mwenendo wake ulikiuka falsafa ya chama, tumewaona marafiki zake CCM wakimpigia kampeni awe mwenyekiti kwa awamu nyingine. Ni lini mpinzani wako anakupigia kampeni ya kuwa mwenyekiti?

Haya yote yanathibitishwa na matukio yote ya wafuasi wake baada ya uchaguzi. Haihitaji hadubini kujua Mbowe ametutapeli muda mrefu.
Spinning na doctrine ya alternative facts in full swing. Na bado.

Amandla...
 
Mtaondoaje sumu kama hamumshughulikii anayeisambaza? Liambieni tu tawi lake limfukuze. Kama mnaogopa hata hilo bali limpe suspension. Na kama hiyo nayo mnaogopa, Katibu Mkuu atoe press release kuwa Mbowe ndio yuko nyuma ya G55 na ni msaliti wa CDM. Au Kamati yenu ya Maadili imuite ili akajieleza kuhusu hizi shutuma. Ukweli ni kuwa nyinyi kama bullies wote, ni cowards. Mnaweza kuwashughulikia vidagaa kama wakina Sigrada na Mrema lakini mnagwaya kulishughulikia papa.

Unless kama nyinyi ni mawakala wa CCM na nia yenu ni kuibomoa CDM.

Amandla...
Mbinu aliyoitumia kuwashughulikia kina lissu , Lema, Heche nk ndio hiyo hiyo anayoitumia sasa kwa kuwatanguliza chawa wake. Ni vigumu kushughulika nae moja kwa moja
 
Mbinu aliyoitumia kuwashughulikia kina lissu , Lema, Heche nk ndio hiyo hiyo anayoitumia sasa kwa kuwatanguliza chawa wake. Ni vigumu kushughulika nae moja kwa moja
Kumbe ndio maana mlimshughulikia kinafik? Kwa kujificha mitandaoni. Angalau Mrema anasema anayosema hadharani bila kujificha.

Nyie ni watu wabaya sana. Mnaishi kwa fitna na ulaghai.

Amandla...
 
Uzuri wanachama wanaelewa kinachoendelea. Ndio maana walimstaafisha. Sasa hivi kwa namna yoyote akatavyokuja watamshughulikia. Wamechoka kuuzwa.
Spinning na doctrine ya alternative facts in full swing. Na bado.

Amandla...
 
Kelele za Akina mrema ni za kukatiwa Mirija. Kwa namna yoyote ile ilikuwa lazima watoe milio.
Kumbe ndio maana mlimshughulikia kinafik? Kwa kujificha mitandaoni. Angalau Mrema anasema anayosema hadharani bila kujificha.

Nyie ni watu wabaya sana. Mnaishi kwa fitna na ulaghai.

Amandla...
 
Mbowe ni tapeli. amewalaghai watz kwa zaidi ya miaka 20. Yeye na genge lake wameshafeli sana! Mungu Yuko upande wa haki. Haki itatamalaki. This year
Jichunguzeni mlivyo wabinafsi, mnamshambulia mtu ambaye kwa muda wa miaka 20 alikuwa shujaa aliyeongoza chadema goigoi mpaka kuwa chama kikuu cha upinzani! Mnamvua nguo mtu ambaye angetaka huyo Lissu hata fomu yake ya ugombea isingerudi na hivyo kukosa sifa. Mlimsifu kwa usitahamilivu kutokana na madhila aliyoyapata yeye binafsi kwa sababu ya chadema. Iliharibiwa miradi yake, alipigwa akawekwa jela na hamkuweza kumsaidia kwa lolote. Akafanya maridhiano na serikali mkarejeshewa tena haki ya kufanya siasa, Kwasababu hakutaka uchafuzi wa amani ili kuwalindeni mnamuita Tapeli. Mkaungana na kichaa LISU kwenye uhaini wa 'no reform no election' na sasa yupo jela. Angalia mlivyo wanafiki, mbona hamuendi kuungana naye huko jela? Kamanda mmemuachia msala. Mlitaka mbowe aingie kwenye hilo chaka?
 
Mbowe amewaachia chama muongoze, yeye anaendelea na maisha yake. Ila kutwa kumfatafata.
Amewaachia ama ameachia kwa fedheha na kwa kulazimishwa?

Alitaka aendeleze ulaghai wake wakamshtukia wakamkataa mchana kweupe licha ya mfumo wote kuwa upande wake.
 
Uzuri wanachama wanaelewa kinachoendelea. Ndio maana walimstaafisha. Sasa hivi kwa namna yoyote akatavyokuja watamshughulikia. Wamechoka kuuzwa.
Hawana huo ubavu. Hawa wanaogopa wakiona mgambo wanafanya usafi barabarani hawawezi kumshughulikia.
Swali langu ni lile lile. Kama Mbowe ni tapeli, mfujaji wa mali za chama, msaliti n.k. mnashindwaje kumfukuza wakati chama mmekishika na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Chama wakati wake bado yupo? Lazima kuna paper trail ya uchafu wake. Iwekeni wazi ili akose hata pa kukimbilia. Kama hamuwezi, nyamazeni na m focus kwenye chama chenu na NRNE.

Amandla...
 
Watu wengi wameumizwa. Wapo waliokufa kwa sababu ya Chadema. Shida ilianzia pale alipotoka gerezani. Alitoka akiwa ametuuza kwa CCM. Akaamua yeye mwenyewe kukanyaga legacy yake aliyojenga kwa miaka mingi.
Jichunguzeni mlivyo wabinafsi, mnamshambulia mtu ambaye kwa muda wa miaka 20 alikuwa shujaa aliyeongoza chadema goigoi mpaka kuwa chama kikuu cha upinzani! Mnamvua nguo mtu ambaye angetaka huyo Lissu hata fomu yake ya ugombea isingerudi na hivyo kukosa sifa. Mlimsifu kwa usitahamilivu kutokana na madhila aliyoyapata yeye binafsi kwa sababu ya chadema. Iliharibiwa miradi yake, alipigwa akawekwa jela na hamkuweza kumsaidia kwa lolote. Akafanya maridhiano na serikali mkarejeshewa tena haki ya kufanya siasa, Kwasababu hakutaka uchafuzi wa amani ili kuwalindeni mnamuita Tapeli. Mkaungana na kichaa LISU kwenye uhaini wa 'no reform no election' na sasa yupo jela. Angalia mlivyo wanafiki, mbona hamuendi kuungana naye huko jela? Kamanda mmemuachia msala. Mlitaka mbowe aingie kwenye hilo chaka?
 
Mbowe kanyang'anywa supermarket yake ikageuzwa kuwa chama cha kweli cha upinzani. Mbowe alikuwa anapata pesa toka CCM kila mwaka wa uchaguzi
 
Wanachama wameshughulika nae kupitia uchaguzi. Hata sasa watashughulika nae kwa namna yoyote atakavyokuja.
Hawana huo ubavu. Hawa wanaogopa wakiona mgambo wanafanya usafi barabarani hawawezi kumshughulikia.
Swali langu ni lile lile. Kama Mbowe ni tapeli, mfujaji wa mali za chama, msaliti n.k. mnashindwaje kumfukuza wakati chama mmekishika na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Chama wakati wake bado yupo? Lazima kuna paper trail ya uchafu wake. Iwekeni wazi ili akose hata pa kukimbilia. Kama hamuwezi, nyamazeni na m focus kwenye chama chenu na NRNE.

Amandla...
 
Kama ni hivyo, mpelekeni mahakamani. Sio kila mtu yuko kama wewe.

Amandla...
Mahakama gani mzee anatakiwa kuacha uhuni, kuna suala la kupeleka mahakamani hapo. Kwa nini aruhusu waliokuwa wanamuunga mkono wakanyage legacy yake kwa kuhujumu chama. Yeye ndio mzee pekee wa chama. Kwa heshima yake, alihitaji Simu moja tu kuzima huo uhuni. Tunawezaje kumuondoa kwenye huo uhuni.
 
Vipi mnaona hao G55 wanaweza kuua chama,au wanaleta hofu juu ya kiti cha mwnyekiti na makamu wake?.
Muwaache vijana wakagombee
 
Nyie ngombe, mmeachiwa chama kimewashinda?
 
Mbo
Wataalamu wa historia wanasema historia hutuambia kwa nini tupo hapa. Nimelazimika kutafakari na kurejea matukio mbali mbali yanayomhusu Mwenyekiti Mbowe kabla ya kupumzishwa na wanachama kwenye nafasi ya wenyekiti wake. Nimerejea matukio mbali mbali hususani baada ya mwenyekiti Mbowe kutoka Gerezani na kuibukia Ikulu, mwenendo wa vikao vya maridhiano, mwenyekiti Mbowe kuanza kuwashughulikia wajumbe wa kamati kuu waliopinga mwenendo wa maridhiano kama Mch Msigwa, Lema, Lissu na Heche kwenye kamati kuu na kwenye chaguzi za Chama. Nimelazimika kurejea hotuba yake aliyotoa akiwa mwanza vile vile. Nikiwa naendelea na tafakuri nikakumbuka namna alivyopambana kuhakikisha Lissu hagombei uenyekiti wa Chama baada ya kumwekea kivuli chake kwenye nafasi ya umakamu, mpaka alipowaita maaskofu wakae vikao vya upatanishi. Muda huo mwenyekiti Mbowe alikuwa hajatagaza kugombea uenyekiti. Baada ya jitihada zote za kumzuia Lissu kugombea kugonga mwamba, hatimaye alishawishiwa na wanachama kama kawaida yake kutangaza nia ya kugombea. Alitangaza nia akiwa anavuja jasho kubwa sana. Baada ya tukio la kutangaza nia, tulishuhudia pia matukio mengi yanayomhusu yeye mwenyewe kumshambulia Lissu au wafuasi wake. Nimerejea interviews kadhaa zake yeye mwenyewe na za wafuasi wake kama Kina Yericko Nyerere, Daniel Naftal nk.

Tumeshuhudia pia nguvu kubwa ya rushwa siku ya uchaguzi ikiwa ni mwendelezo wa njia za kuhakikisha anashinda na hivyo aliamini anashinda kwa asilimia zote. Siku ya uchaguzi tukashuhudia uchaguzi bora sana wa huru na haki uliomstaafisha na akatoa hotuba ya kishujaa sana tukadhani ni mzee ambae amekubali Chama kiongozwe na vijana aliowalea.

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, baada ya uchaguzi tukaanza kuona vituko vya Mchome ambaye ni kijana wa mbowe na sakata lake la akidi, na baadae likaibuka kundi la G55 ambao zaidi ya asilimia 70 walikuwa wafuasi wa Mbowe kwenye uchaguzi mkuu wa Chama. Nirudia pia kisoma waraka wao juu ya No reform, No election, nikasikiliza pia hotuba ya Mwenyekiti Mbowe juu ya No reform, No election.

Kuna mambo mengi sana ambayo ukiwa unatumia milango yote ya fahamu, ukirejea matukio yote, huwezi kumuondoa Mbowe kwenye sakata la G55 labda tu Ukiziba milango ya fahamu unaweza kudhani Mbowe amepumzika. Nalazimika tusema Mbowe bado yupo kazini. Kama tukimjengea nia njema, kama Mbowe Angelikuwa na uchungu na Chama alichokijenga kwa miaka zaidi ya 20, kama mzee wa chama na mjumbe wa kudumu wa kamati kuu alikuwa na anayonafasi ya kuwazuia G55 kuendelea na mipango yao kwa simu moja tu na wangeacha mara moja kwa sababu wanachafua na kuharibu legacy yake aliyojenga miaka mingi. Kama mzee wa chama na mtu mwenye uchungu na Chama tunatamani angefanya hivyo ila bahati mbaya hajafanya hivyo mpaka leo.

Hivyo kwa kurejea matukio yote hayo, nalazimika kusema Mbowe anahusika kwenye sakata la G55 na matukio haya yanatuambia kwa nini Hali ilivyo sasa chadema juu ya viongozi wakuu na harakati za kundi la G55.

Wasalaaam
Mbona Bon Yai hayumo?
 
Viongozi wa chadema wanatakiwa kukiflash chama yani kuna watu kama 400 waondelewe chadema la sivyo samia na genge lake kapata mkono wa mauaji ndani ya chadema
 
Back
Top Bottom