Magufuli hahusiki na graduates kuwa mitaani. Na mwaka wa tano tangu atwaliwe na bado hao graduates wapo mitaani. Shida ingekuwa yeye huyu aliyepo angeshawaajiri wote.
Tatizo ni uwenda wazimu wa Watanzania wote wakiongozwa na wanasiasa wao na wasmoni. Kuliwa na haja gani kuua vyuo vya kati na kila Chuo kutoa elimu ya Shahada wakati nchi ina sekta zinazozalisha ajira na kodi.
Kulikuwa na ulazima gani hadi SUA na Mzumbe kutoa hadi kozi za ualimu? Kwa nini hivyo vyuo visingebaki na taaluma zao za asili ya vyo vyao?
Kuna sababu gani vyuo vya ajabu ajabu kutoa elimu ya biashara na uhasibu badala ya taaluma hizo kuachwa kwa UDSM. Mzumbe, IFM, AIA, TIA na CBE?
Ngoja tuendelee kuisoma namba maana sisi ni vichwa vya wenda wazimu.