Kuna vitu kama viwili au vitatu vinachanganywa ndani ya huu uzi, na vimechochewa na mleta uzi kuanza kuchanganya.
Mosi, kuna issue ya uwingi au uchache (namba) wa Watanzania kulinganisha na rasilimali tulizonazo. Je, idadi yetu na ukuaji wake vinarandana na rasilimali tulizonazo? Je, tunapaswa kuongezeka? Je tunapaswa kupanga uzazi? Je tuongezeke tu kwa sababu serikali inaweza saidia kutusomeshea hizi level za chini? Vipi kuhusu mahitaji mengine kama chakula, malazi, afya, nk, je nayo utapewa na serikali? Na vipi akija rais mwingine akafuta sera ya ada bure,? Je, ukiangalia uchumi wa familia yako, vipi unaweza kwenda na watoto wangapi ukiwapatia mahitaji yao ya msingi bila shida mpaka wakafikia kujitegemea? Na tunaposema mahitaji ya msingi, mfano chakula, haimaanishi mtoto apewe chakula kitachomfanya tu asife, bali chakula kinachokidhi mahitaji ya ukuaji wake wa afya ya akili na mwili?
Pili, kuna issue ya family planning. Je ni jambo zuri au baya? Je, Tanzania, tuna uhitaji wa kupanga uzazi au family planning ni porojo? Je, Kwa vile tuna mapori ya kutosha, tunapaswa kujiachia Ili tuyajaze?
Tatu ni side effects za family planning. Ndani ya mwamvuli wa family planning kuna njia lukuki, kuanzia za asili mpaka za kisasa. Zipo zisizo na madhara kabisa, though efficiency yake ni ndogo, zipo zenye madhara kidogo na zipo zenye madhara makubwa. je ni njia ipi nzuri kwako? KUMBUKA TU KUWA NJIA ALIYOTUMIA JIRANI/NDUGU YAKO NA IKAFANYA VIZURI KWAKE, HAIMAANISHI NI LAZIMA IFANYE VIZURI NA KWAKO.
Sasa je, dhima ya mwandishi kumuunganisha hayati rais na issue hizo hapo juu ililenga nini?