Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Nikienda kutafuta bodaboda huwa napenda kuwasapot hawa wazee maana wana majukumu kuliko kiasi
 
Mhubiri 3:1-8 BHN

Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake:

1 Timotheo 5:8 BHN

Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.


2 Wathesalonike 3:10 BHND

Tulipokuwa pamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, “Mtu yeyote asiyependa kufanya kazi, asile chakula.”

Methali 14:23 BHN

Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini.

Methali 28:20 BHN

Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu.
 
Akili mgando hiyo.unapaswa uwaze nje ya box jombaa
 
Akili za mleta mada bwana.
Kuna bodaboda wajinga kama walivyo waajiriwa wengine wajinga wanaostaafu bila maandalizi yoyote.

Fikiria mtu anachukua boda ya mkataba, anafanya 12months mkataba unaisha, anachukua nyingine, ile yake anampa mtu analeta hesabu, baada ya miaka mitatu anakuwa na boda zake tatu anachukua hesabu za wiki/siku.

Kuna boda wapo very smart kichwani, wanaingiza vipato vikubwa kuliko hata waajiriwa.
Tusikariri.
 
Ninapopanda bodaboda anayoiendesha mtu mzima huwa na amani kweli nenda moi kaangalie jinsi vitoto vilivyovunjika miguu.
Bodaboda wengi ni rika la vijana wa sekondari au vyuoni.
 
Acheni mawazo haya ya kizamani ya kuamini kuajiriwa tu au kulima.
Kuna dogo amepiga kazi ya boda kwa mkataba akapata zake 2 na bajaji 1. Pia akamiliki mgahawa na kuajiri watu huku mwenyewe akipiga bajaji ya mkataba kwa mtu mwingine.

Huyo utamlinganisha na mwajiriwa wa chini wa serikali? A mkulima wa kilimo kidogo duni cha jembe la mkono?

Sandali Ali mwenyewe huenda hamfikii kipato chake kwa siku/mwezi.
Huyo anakopesheka na anaweza kujilipia bima ya afya.

Barua ya dhamana ya mwenyekiti wa serikali za mtaa ina shida gani? Si mbadala tu wa barua ya mwajiri? Au inapunguza kiwango cha kukopeshwa?
Kuna watu wamekopa milioni zaidi ya hizo 10M kwa hiyo barua ya utambulisho.
 
Kama ni rahisi hayo uliyoyaeleza hapa acha kufanya mambo yako kwani bajaji na pikipiki za mkataba ziko nyingi na ili upewe huulizwi hata elimu yako.
 
Kama ni rahisi hayo uliyoyaeleza hapa acha kufanya mambo yako kwani bajaji na pikipiki za mkataba ziko nyingi na ili upewe huulizwi hata elimu yako.
Hakuna kitu rahisi au kazi rahisi kwenye utafutaji.
Ajira pia ni mateso na manyanyaso kwa sehemu zingine.
Unaweza kuhamishwa sehemu uliyowekeza na kupelekwa sehemu ya ovyo.
Kuna wanaotoa ngono kwa boss wao.
Kuna wanao pigwa uhamisho mbali na filia zao au kupangiwa safari ili boss wao apate muda wa kuwachukulia wake zao n.k.
Kuna wanasingiziwa makosa na kujikuta jela n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…