Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
Wewe unaamini kila report inayotolewa baada ya JPM kuondoka? Au hujui paka akiondoka panya hujitawala?

Tunahitaji paka mwingine fasta.
 
Wewe unaamini kila report inayotolewa baada ya JPM kuondoka? Au hujui paka akiondoka panya hujitawala?

Tunahitaji paka mwingine fasta.
Embu acha kutulisha huo ujinga wako wa chato! Kama huyo mshenzi wenu alikuwa msafi Kama mnavyosema kwa nini alikuondoa CAG Assad baada ya Assad kuibua ufisadi wake?
 
Best interest of our country at heart inapimwa je?

Egocentricity? Mwendazake hakuwa nayo?
Ndio,hakuwa egocentric,kwa maana kwamba alikuwa hajijali yeye tu,alikuwa anajali Watanzania wote,without exception.
 
Miaka mitano hizo nd
Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?

Miaka mitano hizo ndege zilikuwapo au wewe ndo bogus?
 
Bandari ya bagamoyo hata JPM alishaanza kuukubali mradi ule hasa hotuba yake ya chato inadhihirisha hilo nadhani aliitoa kipindi waziri wa mambo ya nje wa China alipo mtembelea chato

Kwa mujibu wa Deusdedit Kakonko aliye kuwa boss pale Tpa mazungumzo yalikuwa yanaendelea kuhusu marekebisho ya mashariti ya mkataba ule nimuda muafaka Sasa kwa viongozi wetu kutueleza wamerekebisha Nini kwenye mkataba mpya Kama wamekubaliana
 
Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua uhatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake
Jihadhari, hiyo chuki itakuua! Afya ya mwili inataka uwe na furaha na Amani! Hivi huwezi kuongea bila kutukana! Halafu huyo unayemtukana ni marehemu!
Huwezi kutushawishi hata kidogo kuwa shujaa Wa Taifa letu alikuwa MTU mbaya! We we mwenyewe labda mbaya!
 
Embu acha kutulisha huo ujinga wako wa chato! Kama huyo mshenzi wenu alikuwa msafi Kama mnavyosema kwa nini alikuondoa CAG Assad baada ya Assad kuibua ufisadi wake?
Assad alimbwela, na JPM kama ulivyomjua hakuwa mvumilivu sana kwa watu waliokuwa na ajenda zao walizozificha nyuma ya eti taaluma. Wewe unachokijua ni kwamba Assad katimuliwa basi, lakini Rais ana info za ndani zaidi kuliko wewe.
 
Hata kama ni Marehemu. Lazima ukweli usemwe. Alikuwa mshenzi asiyefaa na ndo mana Mungu kamchukua akiwa madarakani. Hutaki tafuta ndimu tengeneza juice unywe.
Jihadhari, hiyo chuki itakuua! Afya ya mwili inataka uwe na furaha na Amani! Hivi huwezi kuongea bila kutukana! Halafu huyo unayemtukana ni marehemu!
Huwezi kutushawishi hata kidogo kuwa shujaa Wa Taifa letu alikuwa MTU mbaya! We we mwenyewe labda mbaya!
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.

Daaa Afadhali Ufanywe Msumbiji...
Sijawahi Kuwaamini Wachina Hata Kidogo...
Pesa Zilizotumika Kukarabati Bandari ya Dar...
Then mamba ya Bagamoyo tena duuu
Miradi iliopo Ikamilike Kwanza Mkuu!
Kwani Huo Upo Kwenye Ilani?
Kwaninj Usisubiri Ilani ya 2025?
Mbona Unataka Kupachika Vitu vipya?
 
Assad alimbwela, na JPM kama ulivyomjua hakuwa mvumilivu sana kwa watu waliokuwa na ajenda zao walizozificha nyuma ya eti taaluma. Wewe unachokijua ni kwamba Assad katimuliwa basi, lakini Rais ana info za ndani zaidi kuliko wewe.
Hakuwa mvumilivu au alikuwa mshenzi aliyependa kuishi kwenye uzandiki na uongo???
 
Ndio,hakuwa egocentric,kwa maana kwamba alikuwa hajijali yeye tu,alikuwa anajali Watanzania wote,without exception.

Haya ya miradi ya chattle, Chatto Inc, sukuma gang na ya namna hiyo hayana elements za egocentricity?

Haya ya wapwa kama paymaster general na wapwa wenyeviti kwenye jumuiya za chama nayo ndiyo mwendelezo wa kujali watanzania wote?
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Kama unafanywa msumbiji sisi inatuhusu nini? Kwani aliyoyafanya JPM kwa kupanua bandari za Tanga, Mtwara na DSM wewe huoni? Mnakosoa relI ya SGR aliyoijenga JPM Kuunganisha na bandari ya Dsm lakini reli aliyotaka kujenga mchina kuunganisha bandari ya bagamoyi hamkosoi.

Hao mabwana zenu huko china wapelekeeni miili yenu sio nchi yetu Tanzania.
 
Hakuwa mvumilivu au alikuwa mshenzi aliyependa kuishi kwenye uzandiki na uongo???
Hakuwa mvumilivu, kama hilo hukulipenda kwake, pole. Ufanisi wake ulitokana na kutovumilia uzembe na uchokoraa.

Hakuja kuuza sura so its ok kama hukumpenda. Na watu effective kama yeye mara zote huwezi kuwa neutral juu yao: either utawachukia kama wewe unavyomchukia, au utamkubali kama anavyokubalika na mamilioni ya watanzania. Amelitendea haki kusudi lililomleta duniani, na ameondoka akiwa Shujaa wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Kwa vipengele vipi vya mikataba usiifaninishe Msumbiji na ujinga uliopo Tanzania.
 
Back
Top Bottom