Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Daaah yani hakuna hata moja ulilomsingizia natamani kuidanlowd maana kunawajinga huku mwanza wanamsifia chaajabu mpaka waha pia wanaendelea kuunga juhudi kamaunavyojua tena huwezi kumuelimisha muha
Just copy and paste
 
Wewe unaamini kila report inayotolewa baada ya JPM kuondoka? Au hujui paka akiondoka panya hujitawala?

Tunahitaji paka mwingine fasta.
Hatuitaji paka tunahitaji katiba mpya na taasisi imara, Rais ni binadamu atakuja ataondoka lakini tukiwa na taasisi imara zitafanya kazi vizuri.

Tabia ya kufikiri kwamba mtu mmoja ni bora kuliko wote ndio inatufanya tusiendelee

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
Hawafai kuaminiwa hawa Watu
Hata kama wanavaa suti na kupendeza
Ni Wasaliti katika uso huu wa Dunia na waongo mpaka wa nafsi zao
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Kama Msumbiji wako tayari kwa masharti ya muwekezaji sisi haituhusu, ni nchi yao.

Vv
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!

Mimi natamani zaidi tujikite zaidi kujadili kwenye plan ya huu mradi, huu ni bonge la project , sio lazima tufanye sasa na sio lazima na mchina hata tukikosa wawekezaji wengine wenye masharti nafuu tupambane sisi wenyewe mdogo mdogo hata kama ni plan ya miaka 25 au 30, tena nafikiri wakati huo hata bandari zetu zitakuwa zimezidiwa na mizigo.

Tuaangalie faida ya mradi kwanza tuone jinsi ya kuutekeleza, hapa tunabishana masharti ya wawekezaji atuelekezi akili nje ya hapo tufanye nini.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Hata kama haya yalosemwa juu ya mwendazake ni ya kweli, hili la bandari ya bagamoyo lazima tumuunge mkono tu. Kwa nini mtu usistuke unapoambiwa miaka 33 TRA wasisogee hapo, au bandari nyingine yoyote haitakiwi kuendelezwa kwa miaka 99. Au eti wachina wako tayari kutoa asilimia 90 ya gharama ya mradi wote!! Kwa wema gani huo? Kwa upendo gani walionao kwetu? Hii haihitaji elimu ya chuo kikuu kustuka. Lazima kuna deal somewhere behind kati ya hao wachina na wachache kati yetu.
Leta vifungu vinavyosema tra wasisogelee Bandari kwa Muda wa miaka 33 ?
Au ulisikia wakisema!
 
Sukuma gang,miradi yoote ya chato haikuwa na msingi,kama bandar ya bagamoyo itakuwa na tija itajengwa tuh,jiwe kukataa siyo kigezo tusiendelee,jiwe mwenyew alikuwa mwizi tuh
 
Hatuitaji paka tunahitaji katiba mpya na taasisi imara, Rais ni binadamu atakuja ataondoka lakini tukiwa na taasisi imara zitafanya kazi vizuri.

Tabia ya kufikiri kwamba mtu mmoja ni bora kuliko wote ndio inatufanya tusiendelee

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kama katiba tuliyonayo ni mbaya mbona mlikuwa mnamsimanga JPM kwamba hafuati katiba iliyopo? Kama katiba iliyopo haifai na akaja rais aliyewasikiliza, akawa anafanya mambo yake aliyoyaona yanafaa, na watanzania wakaona yanafaa, bifu naye la nini?

Katiba ni maandishi yale, watu wakiwa wabovu hata uwe na katiba nzuri namna gani hakuna la maana litakalopatikana.
 
Kila nafsi itaonja mauti, suala ni when and how, si why. Inshu yetu iwe je wakati ukifika tutaacha legacy, tutalitimiza kusudi? Kwa JPM kazi aliifanya, heshima ya nchi yetu aliijenga, na vizazi vitamuenzi.

Kama unahoji ufanisi wake rejea speech ya Mwinyi, "mwenzetu alitekeleza ndani ya miaka mi5 yale yaliyotushinda miaka 40".

Chato gang, na Burundi gang? Man, hata sijui unazungumza lugha gani hapa.

Kutofautiana na katoliki wenzake kuhusu corona? Bado sikuelewi. Kama alitofautiana nao mbona walimzika? Walitofautiana naye vipi kuhusu corona wakati hawakuwahi kuweka lockdown makanisa yao?

Mungu amemuua? Kama Mungu alitoa halafu akatwaa, sisi tusemeje zaidi ya kulibariki Jina Lake?

Afande selemani kazini.

Hiiiiii bagosha!
 
Ndugai ni kiongozi wa mhimili wa hovyo kuwahi kutokea, ni mtu anayecheza mdundo wa kila rais anayeingia madarakani na haelewi ni nini maana ya kuwa kiongozi wa mhimili kama bunge, kuna skendo zake za ufujaji wa pesa za walipa kodi kwenye matibabu yake huko India zimeongelewa sana humu...
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
Ni vyema mkataba huo uwekwe wazi kwa ajili uchambuzi na majadiliano.
Hii itasaidia faida na hasara zinazoweza kusababishwa na mkataba huo kujulikana ili kufikia a win-win situation na kuepika kubebesha Watanzania mzigo wa madeni yasiyo na tija kwa nchi.
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
Mkataba ya kujenga chato airport nao uwekwe wazi!
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.

Mkuu, Hayati Dr. Magufuli alivyokuwa na addiction na miundombinu asingeuacha huu mradi kirahisi namna hiyo.

Kama wewe unayo hiyo report kwa nini usiilete hapa?
 
Yaani mimi hata nikisikia JK ndiye prezidaa fresh tu, achilia mbali kucontrol remotely.

Mwendazake alitutesa sana.
 
Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua hatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake.
Unaonekana una roho mbaya, mbaguzi, mbinafsi, una kisasi na wewe ni mkabila. Haitakufikisha kokote, achana nayo.
 
Back
Top Bottom