Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KUIFUTA CCM SIO KUONDOA MATATIZO YA TAIFA HILI. HIYO NI PROPAGANDA YENYE UONGO MKUBWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Kuna watu wanadanganya Watanzania matatizo ya Nchi hii ni uwepo wa chama cha mapinduzi( CCM ). Huo ni uongo mkubwa.

2. Wengine wanausema uongo huo kwa makusudi wakijua ni uongo(Siasa) wengine wanasema uongo huo bila ya kujua.

3. Sisi Watibeli hatupendi upotoshaji, uongo. Mtu yeyote au kikundi chochote bila kujali nafasi, cheo, mahusiano yetu na wao.

4. Kusema CCM ikiondolewa kwenye hii nchi matatizo ya taifa hili yataondoka ni uongo. Na kauli za kisiasa.

5. Matatizo ya nchi yetu Yana mizizi mikuu miwili;
a) Malezi kuanzia ngazi ya Familia.
b) Ukoloni Mamboleo.

6. Asilimia 60% ya Matatizo ya nchi hii yanatokana na Malezi Mabovu kutoka kwenye ngazi ya Familia. Hapo ndipo kuna mambo ya uadilifu, uchapakazi, nidhamu, uzalendo n.k.

7. Asilimia 40% ni Ukoloni Mamboleo.
Binafsi ninaamini taifa letu bado halipo huru. Hicho ndicho ninajua. Ingawaje ukiniambia nikupe ushahidi naweza kukosa lakini ninachoamini ndivyo ilivyo.

8. Akili Yangu inanituma kuwa kuna mikataba ya siri ambayo iliingiwa ambayo inaifanya nchi yetu isiwe huru.

9. Unaweza ukawa mzalendo kikamilifu. Ukapewa urais na ukaona ni rahisi. Unaingia ikulu unakutana na vitu vizito unabaki unabung'aa.

10. Ukisema ukaze watu wako wa chini wanakuwa sio waadilifu. Wanaungana na mabeberu wanakunyoosha.

11. Mabeberu wananguvu kwenye jamii lililojaa watu wasiowaadilifu. Wasio wachapakazi, wenye tamaa, wapenda Rushwa., wavivu, wasaliti n.k.

12. Tabia zote hizo mbaya MTU hujifunza alipolelewa, makuzi, na jamii inayomzunguka.

13. Hauhitaji kuwa CCM ili uwe mla rushwa, haihitaji uwe CCM ili uwe Fisadi, haihitaji uwe CCM ili uwe msaliti wa taifa lako.

14. Mambo hayo ni matokeo ya malezi mabovu tangu mtu akiwa mtoto Mdogo.

15. Sheria za ndoa, familia zikilegezwa na kutosimamiwa ipasavyo huwezi kuwa na taifa la maana lenye uadilifu na maadili.

16. Uwe CHADEMA au CCM au huna chama kama hauna uadilifu ni hauna tuu.

17. Ukandamizaji wa kisiasa hautokani na CCM bali ukandamizaji ni mfumo mzima wa jamii ya taifa letu.

18. Ukandamizaji na unyanyasaji ni utamaduni wa jamii zetu nyingi katika nchi yetu. Sio suala la uccm.

19. Nitakupa Mfano, kwa jamii zetu nyingi Mwanaume ambaye ni Baba na mume akikosea hapaswi kukosolewa na watoto wake au Mkewe.

20. Mwanamke au mke atakapojaribu kuhoji na kukosoa maamuzi na matendo ya mumewe atashukiwa na kukabiliwa vilivyo.

21. Mzazi hakosei. Mke awe msikivu tuu na hapaswi kutoa maamuzi au kukosoa. Hup ni utamaduni..

22. Ukienda Kanisani nako au Msikitini nako utakuta vituko na ukandamizaji mwingine.

23. Unaambiwa Kiongozi hakosei. Au unaambiwa huwezi challenge Quran au biblia. Hizo ndio akili za kikoloni hizo. Utumwa!

24. Quran kwa nini isi chalenjiwe? Ina mini hasa cha ajabu. Kama ingekuwa ukikikosoa unapigwa shoti, au ukisoma andiko inakuwa jambo Fulani tungesema ni kitabu tofauti.

25. Halikadhalika na Biblia kwamba isikosolewe. Kwa vipi? Inakipi cha ziada? Huo ni ukandamizaji wa watu wenye mawazo tofauti na vitabu hivyo.

26. Najaribu kueleza mifumo mbalimbali ya jamii yetu ambayo inatujengea matatizo ya mbali kuliko vyama vya siasa

27. Malezi yaliyojikita kwenye ulaghai na Mila potofu ni sehemu ya kubwa inayoleta matatizo ndani ya taifa letu.

28. Fikiria Mgeni anakuja kwenu mnampa chombo cha udongo ambacho ninyi wenyewe hamkitumii. Ninyi mnatumia vyombo vya plastiki au vibaya. Mazoea hayohayo yanafika ngazi ya kitaifa fursa muhimu na miradi nyeti hata kama kuna raia wenye uwezo wa kuendesha miradi hiyo hatapewa watapewa Wageni.

29. Ukisema ni UCCM, wewe kwako unapoweka vyombo vizuri na maalumu kwaajili ya wageni huku watoto wako mwenyewe wakila kwenye makopo na sahani za plastic au mifupa badala sahari nzuri za udongo au za vioo. Huo kwako sio uccm ni ukarimu.

30. Kutumia mabavu kwenye familia yako, kumtesa mkeo na watoto huoni tatizo lakini serikali ikifanya unaona ni tatizo na linasababishwa na CCM. Unaona?

31. Mkeo hajui akaunti na mapato ya familia yako. Hajui unaingiza kiasi gani. Hajui matumizi yako. Unaficha pesa na miradi yako. Na mnahamasishana kutokuwaamini wanawake. Muda huohuo unailaumu serikali kutokuweka mikataba wazi, kuficha pesa nje ya nchi, kufanya anasa n.k.

32. Huo ni UCCM serikali kufanya anasa na kujinunulia magari ya kifahari, viongozi kujipendelea lakini wewe unapoenda kunywa bia na Kula nyama choma huku mkeo na watoto wakiwa nyumbani na bajeti ya elfu 15 wakati wewe unatumia zaidi ya elfu 50 bar pekeako huo sio UCCM. Na sio vibaya.

33. Tabia ya ubinafsi ni suala la kimalezi, kiutamaduni ambapo likifika level ya kitaifa linakuwa NI tatizo sugu ambalo kulidhibiti ni kipengele.

34. Kwa kumalizia. CCM sio tatizo la nchi hii. Tatizo ni malezi na ukoloni mamboleo.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
We jamaa Una akili Sana nafikiri wewe Una chembembe za Eastain.

Hii kitu umeelezea hapa ni 100%

Mimi jambo hill nililijua tangia mwaka 2015 nikabilidisha uelekeo wa siasa zangu.
 
Tatizo JF ya siku hizi watu wataanza kumjadili mleta mada badala ya kuijadili mada,
Na wengine watakuja na personal attack dhidi ya mleta mada!
 
Asilimia Tisini ya matatizo ya Tanzania yanatokana na CCM,CCM ukifa tutakuwa tumepunguza asilimia Tisini ya matatizo yetu.
Na tuache ujinga wa kusingizia wakoloni na ukoloni mamboleo,hakuna nchi ambayo haikutawaliwa Africa na nchi chache duniani,kwanini zenyewe zipige hatua kubwa sisi tubaki maskini? Unataka lawama ziende Kwa wazungu wakati chama chako kimetawala miaka 60 na upuuzi baada ya wakoloni kuondoka.
CCM ndiyo tatizo kuu la Tanzania
 
Tatizo unaleta hadithi za alpha na ulela kwenye maombolezo

ukisema ccm sio tatizo tayari we ni punguani

mwenye jukumu la kusimamia maadili ni ccm kwasabab ndio imeunda serkali

Maadili yalianza kuporomoka miakaya 2000s chini ya kikwete

na kikwete aliacha hili makusud kwasabab alikuwa na malengo mabaya nyuma ya pazia

anyway sikutukan lkn umeonyeaha ujinga
 
Kuna mtu alisema hata sisi tunaolalamika ni kwakuwa hatujapata fursa, tukiipata tutakuwa the same🤔
Huyo mtu alisema huo ujinga Kwa kutumia mfano gani,huwezi ukatoa hoja ya kijinga wakati unalosema halijawahi tokea.
Mfano baada ya uchaguzi wa 2015 halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na CHADEMA zilikuwa zinapata hati safi ya CAG na za CCM zilibaki na wizi na ufisadi.
Tuache argument za kijinga
 
Haya yote wanapaswa kujifunza Gen Z wote, Millennials na vizazi vingine vyote vilivyopo nchini na vinavyokuja.

Umeelezea Kila kitu kuhusu uzalendo Ina a simpler, clearer and a smarter way possible.

Hakuna kumlaumu mtu, ila tupo kwenye changamoto kubwa sana, na tukizembea zaidi kushabikia ujinga tunaangamiza taifa zima.

NB: hii haihusiani na Siasa au itikadi, kwani ni suala la jamii yetu nzima hasa ngazi ya familia.

Ni ujinga kusubiria jamii/serikali ikutatulie tatizo la ubinafsi ambalo tiyari unalipenda kwenye ngazi ya chini kabisa na hautaki kuliacha...na mbaya zaidi hauoni kama ni tatizo.
 
Huyo mtu alisema huo ujinga Kwa kutumia mfano gani,huwezi ukatoa hoja ya kijinga wakati unalosema halijawahi tokea.
Mfano baada ya uchaguzi wa 2015 halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na CHADEMA zilikuwa zinapata hati safi ya CAG na za CCM zilibaki na wizi na ufisadi.
Tuache argument za kijinga
Je ndani ya chama chao yanayolalamikiwa hayafanyiki?

Yawezekana hati safi zilipatikana kwasababu watendaji walikuwa ni wa ccm na upinzani walihitaji 'kuprove" kitu.
 
Tatizo JF ya siku hizi watu wataanza kumjadili mleta mada badala ya kuijadili mada,
Na wengine watakuja na personal attack dhidi ya mleta mada!

Mtoa mada atajadiliwa na kupewa matusi

Ila Kama ameamua kufanya biashara ya utumbo hawezi kuogopa nzi

Mtibeli hata kule Facebook akiweka mada zinazovuta hisia pinzani anapewaga personal attacks nadhani kashazoea

Ila alichoweka hapa ni kitu cha kweli ambacho sio CCM wala CHADEMA amabao wangetaka kijulilikane .

Tunatumia nguvu kubwa kupambana na umbo la nje na sio ndani.

N.B Luck is not some mystical energy dance around the universe randomly and bestowing people with Joy and satisfaction.
 
KUIFUTA CCM SIO KUONDOA MATATIZO YA TAIFA HILI. HIYO NI PROPAGANDA YENYE UONGO MKUBWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Kuna watu wanadanganya Watanzania matatizo ya Nchi hii ni uwepo wa chama cha mapinduzi( CCM ). Huo ni uongo mkubwa.

2. Wengine wanausema uongo huo kwa makusudi wakijua ni uongo(Siasa) wengine wanasema uongo huo bila ya kujua.

3. Sisi Watibeli hatupendi upotoshaji, uongo. Mtu yeyote au kikundi chochote bila kujali nafasi, cheo, mahusiano yetu na wao.

4. Kusema CCM ikiondolewa kwenye hii nchi matatizo ya taifa hili yataondoka ni uongo. Na kauli za kisiasa.

5. Matatizo ya nchi yetu Yana mizizi mikuu miwili;
a) Malezi kuanzia ngazi ya Familia.
b) Ukoloni Mamboleo.

6. Asilimia 60% ya Matatizo ya nchi hii yanatokana na Malezi Mabovu kutoka kwenye ngazi ya Familia. Hapo ndipo kuna mambo ya uadilifu, uchapakazi, nidhamu, uzalendo n.k.

7. Asilimia 40% ni Ukoloni Mamboleo.
Binafsi ninaamini taifa letu bado halipo huru. Hicho ndicho ninajua. Ingawaje ukiniambia nikupe ushahidi naweza kukosa lakini ninachoamini ndivyo ilivyo.

8. Akili Yangu inanituma kuwa kuna mikataba ya siri ambayo iliingiwa ambayo inaifanya nchi yetu isiwe huru.

9. Unaweza ukawa mzalendo kikamilifu. Ukapewa urais na ukaona ni rahisi. Unaingia ikulu unakutana na vitu vizito unabaki unabung'aa.

10. Ukisema ukaze watu wako wa chini wanakuwa sio waadilifu. Wanaungana na mabeberu wanakunyoosha.

11. Mabeberu wananguvu kwenye jamii lililojaa watu wasiowaadilifu. Wasio wachapakazi, wenye tamaa, wapenda Rushwa., wavivu, wasaliti n.k.

12. Tabia zote hizo mbaya MTU hujifunza alipolelewa, makuzi, na jamii inayomzunguka.

13. Hauhitaji kuwa CCM ili uwe mla rushwa, haihitaji uwe CCM ili uwe Fisadi, haihitaji uwe CCM ili uwe msaliti wa taifa lako.

14. Mambo hayo ni matokeo ya malezi mabovu tangu mtu akiwa mtoto Mdogo.

15. Sheria za ndoa, familia zikilegezwa na kutosimamiwa ipasavyo huwezi kuwa na taifa la maana lenye uadilifu na maadili.

16. Uwe CHADEMA au CCM au huna chama kama hauna uadilifu ni hauna tuu.

17. Ukandamizaji wa kisiasa hautokani na CCM bali ukandamizaji ni mfumo mzima wa jamii ya taifa letu.

18. Ukandamizaji na unyanyasaji ni utamaduni wa jamii zetu nyingi katika nchi yetu. Sio suala la uccm.

19. Nitakupa Mfano, kwa jamii zetu nyingi Mwanaume ambaye ni Baba na mume akikosea hapaswi kukosolewa na watoto wake au Mkewe.

20. Mwanamke au mke atakapojaribu kuhoji na kukosoa maamuzi na matendo ya mumewe atashukiwa na kukabiliwa vilivyo.

21. Mzazi hakosei. Mke awe msikivu tuu na hapaswi kutoa maamuzi au kukosoa. Hup ni utamaduni..

22. Ukienda Kanisani nako au Msikitini nako utakuta vituko na ukandamizaji mwingine.

23. Unaambiwa Kiongozi hakosei. Au unaambiwa huwezi challenge Quran au biblia. Hizo ndio akili za kikoloni hizo. Utumwa!

24. Quran kwa nini isi chalenjiwe? Ina mini hasa cha ajabu. Kama ingekuwa ukikikosoa unapigwa shoti, au ukisoma andiko inakuwa jambo Fulani tungesema ni kitabu tofauti.

25. Halikadhalika na Biblia kwamba isikosolewe. Kwa vipi? Inakipi cha ziada? Huo ni ukandamizaji wa watu wenye mawazo tofauti na vitabu hivyo.

26. Najaribu kueleza mifumo mbalimbali ya jamii yetu ambayo inatujengea matatizo ya mbali kuliko vyama vya siasa

27. Malezi yaliyojikita kwenye ulaghai na Mila potofu ni sehemu ya kubwa inayoleta matatizo ndani ya taifa letu.

28. Fikiria Mgeni anakuja kwenu mnampa chombo cha udongo ambacho ninyi wenyewe hamkitumii. Ninyi mnatumia vyombo vya plastiki au vibaya. Mazoea hayohayo yanafika ngazi ya kitaifa fursa muhimu na miradi nyeti hata kama kuna raia wenye uwezo wa kuendesha miradi hiyo hatapewa watapewa Wageni.

29. Ukisema ni UCCM, wewe kwako unapoweka vyombo vizuri na maalumu kwaajili ya wageni huku watoto wako mwenyewe wakila kwenye makopo na sahani za plastic au mifupa badala sahari nzuri za udongo au za vioo. Huo kwako sio uccm ni ukarimu.

30. Kutumia mabavu kwenye familia yako, kumtesa mkeo na watoto huoni tatizo lakini serikali ikifanya unaona ni tatizo na linasababishwa na CCM. Unaona?

31. Mkeo hajui akaunti na mapato ya familia yako. Hajui unaingiza kiasi gani. Hajui matumizi yako. Unaficha pesa na miradi yako. Na mnahamasishana kutokuwaamini wanawake. Muda huohuo unailaumu serikali kutokuweka mikataba wazi, kuficha pesa nje ya nchi, kufanya anasa n.k.

32. Huo ni UCCM serikali kufanya anasa na kujinunulia magari ya kifahari, viongozi kujipendelea lakini wewe unapoenda kunywa bia na Kula nyama choma huku mkeo na watoto wakiwa nyumbani na bajeti ya elfu 15 wakati wewe unatumia zaidi ya elfu 50 bar pekeako huo sio UCCM. Na sio vibaya.

33. Tabia ya ubinafsi ni suala la kimalezi, kiutamaduni ambapo likifika level ya kitaifa linakuwa NI tatizo sugu ambalo kulidhibiti ni kipengele.

34. Kwa kumalizia. CCM sio tatizo la nchi hii. Tatizo ni malezi na ukoloni mamboleo.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
uzi bora sana na wa mtu mwenye akili nzito! Sasa unaweza kwenda kwenye ballot tukupigie kura ata ukiwa nje ya ccm
 
We jamaa Una akili Sana nafikiri wewe Una chembembe za Eastain.

Hii kitu umeelezea hapa ni 100%

Mimi jambo hill nililijua tangia mwaka 2015 nikabilidisha uelekeo wa siasa zangu.

Mkuu nilichoeleza wala hakihitaji akili nyingi Sana.
Wengi wanakijua na ni Jambo la kawaida.

Ubinafsi pia unahusisha Tabia ya kulaumu wengi
 
Tanzania kukosa maendeleo ya kuridhisha kunatokana zaidi na changamoto za ndani kama historia ya umaskini wa familia, elimu isiyoandaa watu kujitegemea na mifumo dhaifu ya uwajibikaji (hii mifumo inaongozwa na chama cha CCM)

Mambo ya nje yana mchango mdogo lakini maamuzi, mtazamo wa kazi na uongozi wa ndani vina athari kubwa zaidi katika kasi ya maendeleo
 
Asilimia Tisini ya matatizo ya Tanzania yanatokana na CCM,CCM ukifa tutakuwa tumepunguza asilimia Tisini ya matatizo yetu.
Inawezekana na inaweza isiwezekane pia.
Inawezekana kwasababu upinzani watakuwa na nafasi ya kutibitisha yale waliyokuwa wanayakosoa hivyo watahitaji kufanya vizuri ili kujenga imani.

Inaweza isiwezekane kutokana na misingi iliyokwisha wekwa ambapo msingi wake ni aliyoyaeleza mtoa mada. Hivyo watakutana na upinzani mkubwa utakaokwamisha jitihada zote hizo.
 
Na hata wanaolaumu dini na Imani nawashangaa kwa sababu tunahubiriwa Kila siku tusitende dhambi tunazopenda kufanya lakini hatusikii..sanasana zinatunogea balaa..

Tumeshafkia kipindi kuwa tunachagua madhebebu na nyumba za ibada ambazo tunataka kusikia mahubiri fulanifulani pekee na sio ukweli mchungu.

Wapo wanaokimbia misikiti Yao ya karibu au makanisa yao na kwenda kusali mbali ili kufuata mahubiri mazurimazuri...kisa viongozi wa madhehebu hayo hawatuonyi dhambi zetu....Sasa zile dhambi Sasa tangu utotoni, ndio zinakomaa na kuzidi kukomaa...na madhara yake huenda yakawa makubwa zaidi tusipochukua hatua za kubadilika kuanzia ndani mwetu wenyewe nafsini mwetu.

Tusome, tuache dhambi na zaidi ya yote, kupendana. Upendo unatibu na kuponya Kila kitu. Asante
 
Back
Top Bottom