Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Usichanganye kuondoa matatizo ya nchi hii, na matatizo yaliyoletwa na ccm. Ukiifuta ccm matatizo makubwa yaliyoletwa na ccm ndani ya nchi hii yataondoka. Huenda unaelewa kuwa matatizo ya nchi hii yameletwa na ccm. Ni hivi, ndani ya nchi hii matatizo mengi yameletwa na uwepo wa ccm, na hayo yataondoka kwa kuiondoa ccm. Na hayo matatizo mengine ya taifa hili yataondolewa kwa njia nyingine. Jitahidi kwenye maandiko yako usiwe mpotoshaji.


Ertugrul Bey
Safi sana kaka #Tindo huyu mleta maada anajifanya hamnazo na kujitoa ufahamu. Matatizo ya nchi yabaki kama yalivyo na Yale yalioletwa na CCM yataondolewa Kwa kuitoa CCM madarakani.

Mfano mdogo tu . Mchakato wa kupata katiba mpya inayotokana na wananchi ulikwama Kwa sababu ya CCM hii Ina maana kama CCM isingekuwa madarakani Leo hii tungekuwa na katiba mpya yenye kujali sauti za wananchi wake .
 
Mimi napingana na hoja zako baadhi kwa mtazamo huu hapa;

a) Malezi kuanzia ngazi ya Familia.
-Mfuno ukiharibika hata ulelewe na malaika, ukija huko ndani (umeeleza mwenyewe) utakuna na maelekezo ya huo mfumo na utaufuata.

Hapo kinacholalamikiwa ni nani anayesimamia huo mfumo ulioharibika? Jibu unalo.

b) Ukoloni Mamboleo.
-Huu ukoloni unabebwa na hao uliowataja kutokana na nguvu zao, ila pamoja na kwamba wana nguvu wananchi kwa kushirikiana na viongozi mkakataa kutawaliwa na huo ukoloni mnaweza kutoka.

Kikubwa na wananchi wote kuungana, kwani watakendo wapo siyo kwamba wameisha na wengine wapo humo ndani wanatambaa kulingana na uelekeo wa maji.

Sisi wengine tulikuja duniani tukakuta wazazi wetu wamo chamani na wanatumia nafasi hiyo ili waishi.

Hivyo Chama kama CCM kinaposhindwa kusimamia maslahi mapana ya nchi lazima kibebe lawama za kushindwa kufanya jukumu hilo. Kuna kushindwa kutokana umri au funza wanaotafuna ndani kwa ndani, kinachotakiwa ni dawa kuwaua au kung'oa mbao zinazoliwa na kuweka mpya!.
 
Back
Top Bottom