Kuingia ndoani na MTU usiyempenda kutakuzidishia Upweke

Kuingia ndoani na MTU usiyempenda kutakuzidishia Upweke

Kitu kibaya pia kupendwa na mtu usiyempenda sometimes unakuta unapendwa sana tu lakini unaona kabisa huyu akinioa nitampa shida sijui ndio mapepo au ni nn au tutapendana huko mbele
Kundi kubwa wengi tunaangukia hapa ! Manzi anakuelewa kinoma ila wewe humuelewi !
Hivi haiwezekani kujifunza kumpenda mtu kweli ?
 
Unamaanisha mkuu usipopata anayekupenda ni heri usioe kabisa uwe mtume paulo..maana imekaa kama bahati fulani
 
Ngoja nikufundishe kitu mdogo wangu naona kuna vitu vingi kuhusu mahusiano huvijui, mwanamke kuna sifa Fulani Fulani ukiwa nazo atakupenda ,mfano urefu , weusi, ucheshi n.k. , pesa ni sifa ya ziada tu kama ilivyo kumridhisha kitandani. Kwa iyo kama mwanamke amekupendea urefu wako, siku akipata mwanaume mrefu kama wewe halafu ana sifa za ziada kama pesa, atampenda zaidi ya alivyokupenda wewe

Mkuu urefu au weusi, huchochea mvuto wa nje(tamaa)

Mapenzi au upendo ni ishu inayokuja natural na hakuna sababu ya moja Kwa moja ukimpenda mtu unaweza kusema umempendea nini.

Sifa za nje ni ziada tuu na zinahusu mvuto wa nje kufurahisha Mwili.

Kuna mademu wakali nimewashuhudia wameanguka kwenye mapenzi na washkaji wasio na Sifa maarufu kama hizo za Uhandsome boy, sijui urefu, yaani ni vishkaji Fulani hivi, na Pesa havina.
Na hao mademu wanatongozwa na wanaume wenye muonekano mzuri, wenye hadhi na Pesa lakini wanawatolea nje hao wanaume.

Pia kuna Wanawake ni handsome boy na wanavipato lakini utakuta anampenda mdada ambaye ukimtazama hata wewe unashangaa, na Haki kadada kakiamua kumpelekesha kanampelekesha kweli.
Mapenzi!
 
Nimeisubscribe niisome baadae vizuri mana na hii 33 niliyonayo....
 
Kitu kibaya pia kupendwa na mtu usiyempenda sometimes unakuta unapendwa sana tu lakini unaona kabisa huyu akinioa nitampa shida sijui ndio mapepo au ni nn au tutapendana huko mbele

Alafu unaweza ukaamua kusema Acha niwe naye nitajaribu(kuudanganya moyo) lakini ili ujue Uongo ni Mbaya Subiri Baada ya mikaa 10 au ishirini utashangaa mambo yakirudi yanarudi Kwa nguvu kubw, moyo wako unalipia kisasi Kwa kuupuuza, kuulaghai, kuiletea ubabe. Hapo ndio unakuta limama limegeuka, likorofi, haliambiliki, yaani hatari Sana hapo
 
Stress za ndoa kuna watu wanavua nguo huku wakijiongeresha kuwa hawa "mafundi machizi nini? wanadhani Mungu alikosea kutuumba bila nguo"

Baada ya miaka 20 unaambiwa Watoto hawa sio wako. Hapo usipopata presha au stroke wewe jembe
 
Baada ya miaka 20 unaambiwa Watoto hawa sio wako. Hapo usipopata presha au stroke wewe jembe
Unabaki unanung'unika tu kwamba "ina maana mimi ni mkaidi kiasi hiki? Nimegoma kurudisha faida ya Talanta, hata talanta, nimegoma ku multiply matokeo yake walimwengo wakanibeba ufala wakanibebesha mizigo ya kama Mnyamwezi ili nihangaike nayo. Yaani walinibebesha dhambi zao halafu wenyewe wakawa wanakula maisha?"
 
Unabaki unanung'unika tu kwamba "ina maana mimi ni mkaidi kiasi hiki? Nimegoma kurudisha faida ya Talanta, hata talanta, nimegoma ku multiply matokeo yake walimwengo wakanibeba ufala wakanibebesha mizigo ya kama Mnyamwezi ili nihangaike nayo. Yaani walinibebesha dhambi zao halafu wenyewe wakawa wanakula maisha?"

Ndio Ile kumbukumbu la torati 28 inatimia kwako
 
KUINGIA NDOANI NA MTU USIYEMPENDA KUTAKUZIDISHIA UPWEKE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuishi mwenyewe ni kazi, kunachosha, kunakufanya uwe mpweke. Hapo Maisha yanapoteza mvuto. Lakini kuishi na Mwenza usiyempenda na asiyekupenda ndio kubaya zaidi na kunaleta upweke zaidi.

Ninaposema utafute Mwanamke anayekupenda na unayempenda ninamaanisha kuyapa Maisha yako maana na furaha. Kuondoa upweke ambao hakuna Dawa ya upweke zaidi ya upendo.

Tafuta Mwenza ambaye Mtakuwa washkaji, marafiki, mnao-share interests nyingi(sio zote) na hobbies.
Ili hilo litokee lazima mpendane Sana.

Nakuhakikishia kama hampendani lazima Moto uwawakie, Utapeli utawaua, maumivu Makali yatawashusha kuzimu polepole Kwa uchungu mkali,

Watoto mtakaowazaa sio chanzo cha kuondoa upweke wenu. Mapenzi yenu ndio chanzo kikuu cha kuondoa upweke wenu.

Kijana wa miaka 30 iwe ni Binti au kijana wakiume anaweza asielewe nini ninasema hapa. Lakini Watu wazima wanajua nazungumzia nini hapa.

Bar haiwezi kukupa Kampani, vijiwe haviwezi kukupa Kampani, saluni au vilinge vya umbea havijawahi kuondoa upweke. Mumeo au Mkeo mnayependana ndiye MTU pekee anayeweza kuondoa Upweke wako.

Sio Baba yako, sio Mama yako atakayeweza kuondoa upweke wako.
Elewa kuwa kadiri unavyokua mkubwa ndivyo unavyozidisha umbali na Wazazi wako, kama ukiwa mdogo ulizoea kuwasiliana na mzazi wako masaa yote, basi ukifika umri wa balehe masaa hupungua, na itafikia Wakati Kwa Siku unaweza kuongea na mzazi dakika zisizozidi thelasini.
Na kuna Wakati inaweza kupita siku nzima hujaongea naye. Unajua hiyo inamaanisha nini? Jibu lako ni Stori ya siku nyingine.

Utamu wa ndoa upo katika umri wa utu uzima hasahasa Watoto wakishakuwa wamekuwa wakubwa, hapo Watoto wanaanza kutawanyika na kutafuta Maisha Yao. Hapo ndipo mambo huweza kuwa mazuri au mabaya ikiwa hamkuwa mnapendana kama Mume na Mke kweli.

Elewa kuwa kama hakuna mapenzi, unaweza kuwa umeolewa lakini bado ukawa mpweke, yaani unaishi na MTU lakini kama hayupo. Hakuna Stori, hakuna Michezo, hakuna matani, hakuna burudani, hakuna kucheza pamoja.

Yaani mnakuwa kama mpo kwenye Kampuni mnafanyakazi, yaani mmeajiriwa. Muda wote mpo serious kama vile vibarua walioajiriwa na Mjerumani.

Mkipendana, ninyi ndio Ma-boss WA nyumba yenu. Msipopendana ninyi wote ni watumwa, au mmoja WA hiyo Ndoa anaweza kuwa mtumwa WA mwenzake. Muda wote hofu, muda wote mashtaka, muda wote kushutumiana, muda wote kulaumiana na kurushiana maneno, muda wote kutafutiana Makosa.

Nafsi ikiwa uchi hata mwili uvalishwe nguo hautastirika. Upweke utakufanya uyachukie Maisha.

Pesa kamwe sio Dawa ya Upweke na haijawahi kuondoa upweke. Upweke SULUHU yake ni MTU unayempenda na anayekupenda. Hiyo ndio SULUHU.
Unaweza ukawa ndani ya jumba la ghorofa lakini ukawa mpweke na ukayaona Maisha mabaya Sana. Lakini mwingine anaweza akawa yupo Mkuranga kwenye nyumba ya nyasi lakini akawa na Kampani na furaha na kuyaona Maisha yanamaana kubwa.

Sio rahisi Watoto wadogo kunielewa, lakini zaidi sio rahisi Watu wenye upeo Mdogo au wavivu wa kufikirisha Akili zao kuelewa Taikon anazungumzia Jambo Gani.

Binti zangu, Mimi kama Baba yenu, kama nilivyowausieni, tafuteni wanaume wanaowapenda na mnaowapenda. Mimi kama Baba yenu siwezi kuwaingilia katika Jambo Hilo.
Hakuna mwanaume atakayeweza kununua moyo wako, wala hakuna thamani yoyote inayotosha kununua moyo wako zaidi ya moyo WA mwanaume unayempenda na anayekupenda.

Vivyohivyo Kwa Vijana wangu wa kiume, msilazimishe Mapenzi. Kama Mwanamke Hakupendi msimlazimishe, oeni Wanawake mnaowapenda na wanaokupendeni.
Msije mkajidanganya kuwa atakupenda hivyohivyo au atajifunza kukupenda. Huko ni kujidanganya. Wengi wameteseka.

Wengi wamewaona Wanawake ni wachawi, wabaya na wenye Roho Mbaya lakini kumbe kosa lilikuwa Lao kuwalazimisha wawapende, nao Wanawake wakajaribu kujifunza kuwapenda lakini siku zote kitu kisicho cha asili hushindikana.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wengi wamewaona Wanawake ni wachawi, wabaya na wenye Roho Mbaya lakini kumbe kosa lilikuwa Lao kuwalazimisha wawapende, nao Wanawake wakajaribu kujifunza kuwapenda lakini siku zote kitu kisicho cha asili hushindikana.[emoji419][emoji375]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu unaweza ukaamua kusema Acha niwe naye nitajaribu(kuudanganya moyo) lakini ili ujue Uongo ni Mbaya Subiri Baada ya mikaa 10 au ishirini utashangaa mambo yakirudi yanarudi Kwa nguvu kubw, moyo wako unalipia kisasi Kwa kuupuuza, kuulaghai, kuiletea ubabe. Hapo ndio unakuta limama limegeuka, likorofi, haliambiliki, yaani hatari Sana hapo
Hata wanawake wapo wanamng'ang'ania mtu Hadi mwingine anajibebesha na mimba mwisho wake Huwa mbaya pia
 
Back
Top Bottom