Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Dar ni Jiji la kwanza kwa maendeleo Tanzania na yamkini Afrika Mashariki.

Dar imejaa Fursa mbalimbali za kujikwamua Kiuchumi kwa kijana mtafutaji na mpambanaji hasa ambae ana lengo la kutoboa maishani. Lakini kijana huyu awe tayari kufanya kazi ya namna yoyote Mradi mkono uende kinywani.

Dar imejaa starehe na anasa za Kila namna ambazo asilimia kubwa sana zinawatoa kwenye reli vijana waliokuja kwa ajili ya kupambana, sababu damu inachemka hivyo starehe kwake inakua muhimu Sana kwa muda huo, changamoto vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kwa kushindwa kubalance kati ya mapato na matumizi.

Dar ni sehemu hatari Sana kwa kijana ambae amekuja kiupambanaji lakini akawa mvivu wa mwili na akili akataka Kutumia short cut ili atoboe. Huyu ataangukia kwenye mikono ya ushoga, kubebeshwa madawa au kua jambazi/kibaka au utapeli. Maana ukubwa wa starehe uliopo utampeleka resi Apate pesa nyingi kwa haraka ili kumudu matumizi.

Dar ni sehemu sahihi sana kielimu kwa mtu aliyekuja kusoma, lakini kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu hatarishi pia hasa Kwa wale ambao hawakua na malezi sahihi toka kwao. Mtoto anakuja kusoma anarudi na ukimwi. Utashangaa mtoto wa first year ana iPhone 15 pro max ambayo hata mzazi wake Hana uwezo wa kumiliki. So kaipataje, KATOA MZIGO kwa wadau.

Dar ni njiapanda ya ndoto za vijana wengi wanaotaka kwenda kuishi ughaibuni. Hapa nipo michongo yote na connection huanzia. Ukiwa hapa utajua Nini maana ya green card na unaipataje, utajua balozi zote zilipo na Fursa zao.

Dar ndio sehemu ambayo mtu anakaa anatunga kamradi tu kwa hovyo hovyo na kanaitika anapiga hela. Yamkini aliyeanzisha marathon hakujua kama Utakua mchongo Mkubwa wa watu kupiga hela either binafsi au kupitia mashirika...

HIYO NDIO DAR, ONGEZEA YA KWAKO..

KARIBUNI SANA DAR ES SALAAM ILA MUWE NA PASSPORT (kidding)
Umenikumbusha wimbo, zile old bongo flava, Balozi AKA Dola Soul and Mr Sugu AKA 2 Proud. Ngoma inaitwa DSM chorus "dar, dsm, sema? dar es salaam x2. Kama wewe ni mtoto wa juzi juzi nenda youtube,
 
Dar ndio Jo'burg, Boston town, London,Paris, Dubai, New York City, kwa TANZANIA kuishi dar es salaam TU tayar ni FORM 6.

Kuna mikoa ukitembelea unabaki kushangaa mfano huko Lindi na mtwara ndani ndani Kuna umaskini ulio topea.

Aje mtu kunipinga.
 
Dar es salaam ni nzuri kwa mtu mwenye kazi nzuri yenye mshahara mnono au mtu mwenye biashara kubwa zinazojiendesha zenyewe ,mtu mwenye nyumba nzuri ya kukaa na usafiri binafsi. Njee ya hapo ni mji wenye mateso makubwa.
Si wanasemaga ni heri kulia kwenye Range rover kuliko kucheka kwenye baiskeli
 
Umenikumbusha wimbo, zile old bongo flava, Balozi AKA Dola Soul and Mr Sugu AKA 2 Proud. Ngoma inaitwa DSM chorus "dar, dsm, sema? dar es salaam x2. Kama wewe ni mtoto wa juzi juzi nenda youtube,
DSM!! sema aah Dar es Salaam ,Dar!!.

Balozi Yuko daressalamu. Daressalamu mambo yanatokea.

Kila tu Bomba !!! Mademu Bomba!!!

Watu wanajichanya michuma Bomba!!!

Oiiii daressalamuuuuuuuuuu!!
 
Dar ni Jiji la kwanza kwa maendeleo Tanzania na yamkini Afrika Mashariki.

Dar imejaa Fursa mbalimbali za kujikwamua Kiuchumi kwa kijana mtafutaji na mpambanaji hasa ambae ana lengo la kutoboa maishani. Lakini kijana huyu awe tayari kufanya kazi ya namna yoyote Mradi mkono uende kinywani.

Dar imejaa starehe na anasa za Kila namna ambazo asilimia kubwa sana zinawatoa kwenye reli vijana waliokuja kwa ajili ya kupambana, sababu damu inachemka hivyo starehe kwake inakua muhimu Sana kwa muda huo, changamoto vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kwa kushindwa kubalance kati ya mapato na matumizi.

Dar ni sehemu hatari Sana kwa kijana ambae amekuja kiupambanaji lakini akawa mvivu wa mwili na akili akataka Kutumia short cut ili atoboe. Huyu ataangukia kwenye mikono ya ushoga, kubebeshwa madawa au kua jambazi/kibaka au utapeli. Maana ukubwa wa starehe uliopo utampeleka resi Apate pesa nyingi kwa haraka ili kumudu matumizi.

Dar ni sehemu sahihi sana kielimu kwa mtu aliyekuja kusoma, lakini kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu hatarishi pia hasa Kwa wale ambao hawakua na malezi sahihi toka kwao. Mtoto anakuja kusoma anarudi na ukimwi. Utashangaa mtoto wa first year ana iPhone 15 pro max ambayo hata mzazi wake Hana uwezo wa kumiliki. So kaipataje, KATOA MZIGO kwa wadau.

Dar ni njiapanda ya ndoto za vijana wengi wanaotaka kwenda kuishi ughaibuni. Hapa nipo michongo yote na connection huanzia. Ukiwa hapa utajua Nini maana ya green card na unaipataje, utajua balozi zote zilipo na Fursa zao.

Dar ndio sehemu ambayo mtu anakaa anatunga kamradi tu kwa hovyo hovyo na kanaitika anapiga hela. Yamkini aliyeanzisha marathon hakujua kama Utakua mchongo Mkubwa wa watu kupiga hela either binafsi au kupitia mashirika...

HIYO NDIO DAR, ONGEZEA YA KWAKO..

KARIBUNI SANA DAR ES SALAAM ILA MUWE NA PASSPORT (kidding)
Sio ndoto ya kila kijana samahani sana usitusemee
 
Back
Top Bottom