Bradha
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 8,787
- 45,257
Tatizo upako sina na nguvu za kusukuma sina.Njoo uniombee wewe [emoji847]
Mzima lakini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo upako sina na nguvu za kusukuma sina.Njoo uniombee wewe [emoji847]
Tangu nilipomuona Fernandez kwenye kutapeli Madini dhahabu feki nimeyazarau sana haya makanisaMwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.
Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.
Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.
Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.
Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.
Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.
Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.
Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.
Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.
Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.
Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.
Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.
Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
Umeongea kwel.Watu ni wabinafsi sana hawa wanaoji potray kama watumishi wa Mungu.sitakaa nisahau mama mmoja alikuwa mja mzito alipelekwa kuombewa kisa ana mapepo kumbe ni kila kichaa kinaitwa kichaa cha mimba mama wa watu walipigwa mangumu pepo atoke in short alikuja kupoteza maisha.........Nina rafiki yangu mmoja mchaga tulikuwa tunaongea naye nikamuuliza aise wakristo kwa ujumla wao ni watu waliosoma sana elimu dunia kuliko waislam lakini ajabu ni kwamba pamoja na kusoma kwao ni rahisi sana kumuingiza mkenge au mjini mkiristo kuliko muislam.
Nikamukumbusha kikombe cha babu nikamkumbusha wale waumini waliokufa Moshi kwa ajili ya moto.
Wanawake ndio rahisi zaidi kuingizwa mjini.Nikamuambia umeshawahi kuona muislam anajiita nabii.Akaniambia muislamu akijitokeza akajiita nabii wanaondoka na shingo yake
Aaaah mkuu yani nijiulize maswali yote hayo alaf bado tena nije nijiulize maswali ya maisha yangu aaah mkuu niache kidogo maswali ya maisha yangu yenyewe changamoto toshaHuu ulimwengu hatujauumba sisi tumezaliwa tumeukuta. Kama unatambua uwepo wa uchawi naamini utaamini kuna Mungu. Wewe jiulize tu maswali rahisi tu kwanini hakuna siti namba 13 kwenye Ndege, Wewe jiuliza tu unaambiwa mtu kafa hivi nini kinaondoka mwilini maana kila kitu ukikagua vipo mwilini lakini hapumui. Jiulize vijiswali vyepesi tu inakuaje Mtu anatoa kafara familia yake kisha anakuwa Tajiri,Hivi nini kinamkuta mtu tunayeambiwa anayo Mapepo unakuta Mtu anapiga kelele anapiga ukuta vichwa, anazama kwenye maji masaa mpaka mawili akiwa Hana mtungi wa gesi pamoja na yote akiombewa na Sheikh au Mchungaji anapona na anaendelea na Shughuli zake, Jiulize nini dhumuni la wewe kuwepo duniani, Natakua kujua kwanini haujiulizi Dunia imetengenezwa na nani na ni Fundi wa aina gani.Jichunguze mwenyewe kisha jiulize tu kwanini Daktari wa Macho kwanini hawezi kutibu moyo halafu jiulize ni nani anaweza kutibu vyote. Umewahi kufikiri kwanini Madaktari nguli lakini bado wanakwenda Ibadan. Umewahi kuona watu wanapasua Nazi njia panda? Au kuchinja Mbuzi njia panda, Leo fikiria kwa upana zaidi Hivi walioandika vitabu vitKatifu walikuwa na upeo gani wa kufikiri?. Jiulize vijiswali vidogo hivyo kisha njoo utujibu..
Mkuu wewe bado mchanga sana.Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.
Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamsha kwenye mishe zangu za hapa jijini.
Kesho yake Jumapili waakambiwa warudi tena kweli Jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawaida nikasema ibada ikiisha mtanistua nije kuwachukua.
Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.
Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.
Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.
Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.
Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.
Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?
Kwenye daraja mtoni mtongani kwa Florence[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ha haaaaa uminikumbusha vibao vya kustukiza vya kisogoni E.A.G.T city center kwa pastor Katunzi....vinavurugaaa ila sikudondoka
Hili kanisa halipotena na mchungaji wake pia yuko mahabusuHili limenikumbusha miaka kadhaa iliyopita niliudhuria maombi katika kanisa moja liko boko maarufu kwa mzee*** basi bwana ilikua zamu yangu kuombewa nikawekwa mtu kati maombi yakaanza baada ya mda nikawa nimewekewa mikono sehemu mbalimbali ya mwili wangu,kutokana na kuomba kwao kwa kutumia nguvu wakawa wanasababisha maumivi mwilini mwangu especially mikono waliyokua wananivuta na kuniminya kwa nguvu,sasa nilishindwa kuvumilia nikawa nawatoa waniache wenyewe ndowanasema pepo linawajibu nikawa nawaambia mnaniumiza hawaniskii wanasema pepo linawajibu aisee nilipata tabu ambayo siwezi isahau mpaka nilipopata akili ya kwamba nitulie wajue pepo limeondoka nilikua na maumivu mwili mzima yaliyosababisha niumwe wiki nzima nyumbani ukijumlisha na yale mafuta tuliyokua tunapakwa machoni yanawasha kama pilipili...dah
Kingsmann
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mimi niliwahi kujifanya natetemeka kama nina wazimu ili tu nisimwaibishe mchungaji. Lkn nilikuwa naekti tuu basi na yeye akawa anazidi kunikandamiza kichwa. Nilicheka sana siku iyo.
Nimejikuta nacheka kama chiziMaombi bila kuanguka huko ni kukosa uzalendo wa kiroho.
Haya maigizo ya imani sijui wapi mwisho wake
Nimejikuta nacheka kama chiziMaombi bila kuanguka huko ni kukosa uzalendo wa kiroho.
Haya maigizo ya imani sijui wapi mwisho wake
😁😁😁😁Mwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.
Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.
Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.
Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.
Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.
Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.
Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.
Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.
Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.
Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.
Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.
Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.
Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
😀😀😀Pia mimi nilikuwa naombewa hivyox2 niache bangi miaka ya nyuma nikawa nakomaa kudondoka wakati wengine wanaoombewa wanadondoka. Mchungaji akanisogelea na kuninong'onezea Dogo Aisee chalii yangu jidondoshe basi mbona unazingua mbele ya kadamnas? Bado nikawa nimekomaa tu na kumuambia Mchungaji aniwekee laki mfukoni kwanza kisiri. Bas nikamuona kaenda kunong'onezana na wale wanawashikilia wanaodondoka wasijibamize halafu nakuendelea kumpigia Mungu kelele na sauti za ajabux2 baadaye wale wanaosaidia wanaojidondosha wawili wakanisogelea kwa nyuma. Mchungaji akanifuata na kuanza kubwabwaja kwa sauti za ajabu nikashtukizia nachomwa vipini kama sindano makalioni nilipiga ukunga wa hatarii nikasikia mchungaji akipaza sauti toka kwa jina yesu nikawa bado nakomaa kudondoka nikachomwa tena kipini cha hatarii na mtama kima cha nyoka na wale wanaowashikilia wanaodondoka wasijibamize ikabidi tu niende chini
angejifanya mbishi zaidi angechotwa mtama huyo, kuanguka ilikuwa lazima!
Umenikumbusha mchizi wangu mmoja aliwahi nambia alienda kuombewa wote wana dondoka yeye kakaza tu. yule bwana anamsukuma kwa nguvu yeye kakausha tu
alipozidi sukumwa akaona yaishe tu akaanguka na yeye.
wanamaombi watakuja na ufafanuzi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ila mwamposa kateka watu Jamani..huku mtaani kwetu waislamu kwa wakristo kila jumapili wanakusanyana kuelekea kawe.