Wewe jiulize tu maswali rahisi tu kwanini hakuna siti namba 13 kwenye Ndege
Sababu watu wanaamini number 13 ni unlucky hivyo ili kutofukuza wateja baadhi ya company wanaiondoa kwa makusudi ya kibiashara ili wasikoje wateja.
Pia sio ndege zote hazina seat number 13.
Wewe ulipanda ndege gani ambayo haina seat number 13?
Labda ulipanda ndege za watu 12.
Wewe jiuliza tu unaambiwa mtu kafa hivi nini kinaondoka mwilini maana kila kitu ukikagua vipo mwilini lakini hapumui
Ni kwasababu ubongo umeacha kufanya kazi.
Pia viungo vya mwili vinaweza kuacha kufanya kazi bila ya kuonesha tatizo lolote la kuonekana na viungo vya fahamu vya binadamu wa kawaida.
ndio maana kuna vifaa maalum vya kupima sababu za viungo vya mwili kuacha kufanya kazi.
Viungo na kila kitu kwenye mwili wa binadamu vinategemeana na kimoja kikiathirika lazima mwili uache kufanya kazi ipasavyo au uache kufanya kazi kabisa.
Ila ubongo ndio unanafasi kubwa na kucontrol kila kitu na kukufanya wewe ujihisi hai kwa conscious kuwa active.
Kwani mtu aliye kwenye coma kitu gani kimeondoka mwilini na mbona bado hajafa?
Pia inategemea huyo mtu amekufa kutokana na nini.
Huyo mtu amekufa kutokana na nini?
Jiulize vijiswali vyepesi tu inakuaje Mtu anatoa kafara familia yake kisha anakuwa Tajiri
Unaweza ukaorodhesha watu waliotoa kafara familia zao na kuwa matajiri?
Hivi nini kinamkuta mtu tunayeambiwa anayo Mapepo unakuta Mtu anapiga kelele anapiga ukuta vichwa,
Hiyo ni disorder na sio mapepo.
Ni multiple personality disorder.
Mtu anakuwa na multiple personality zilizozalishwa na ubongo kutokana na sababu mbalimbali maybe stress au msongo wa mawazo au kuonewa alipokuwa mdogo au kushuhudia mambo mabaya maishani mwake.
Hiyo personality inazalishwa ili kudefend hiyo original personality ambayo ni mtu mwenyewe.
Na unaweza kutibiwa hospital.
Wewe unadhani kinamkuta nini mtu unayeambiwa ana mapepo?
anazama kwenye maji masaa mpaka mawili akiwa Hana mtungi wa gesi
Hiyo ni impossible na haitokaa iwezekane mtu akae bila ya oxygen kwa masaa mawili tena kwenye maji lazima afe tu.
Sababu mwili wa binadamu hauko designed kusurvive kwenye maji.
Hizo zitabaki kuwa story za vijiweni tu.
Wewe unaweza ukathibitisha hilo kwa facts?
pamoja na yote akiombewa na Sheikh au Mchungaji anapona na anaendelea na Shughuli zake
Hiyo haina tofauti na placebo.
Jiulize nini dhumuni la wewe kuwepo duniani
Jiulize kwanini sayari nyingine hazina maisha bali dunia tu?
Sababu hazisupport uwepo wa viumbe hai.
Sisi kuwepo duniani ni kama coincidence sababu hakuna anayejua chanzo cha dunia wala universe zaidi ya theory na scientist bado wanaendelea kutafuta chanzo.
Na kuna theory za kwenye vitabu vya dini ambavyo vimeandikwa na watu wa kale theory ambazo hazibadiliki wala hazimake sense ni full of contradictions.
Vitabu vya dini ni kama science ya miaka mingi iliyopita.
Wewe unajua dhumuni la kuwepo duniani?
Natakua kujua kwanini haujiulizi Dunia imetengenezwa na nani na ni Fundi wa aina gani
Mimi nakujibu ni "coincidence"
At least big bang theory inajaribu kumake sense.
Wewe unajua nani ametengeneza dunia?
Jichunguze mwenyewe kisha jiulize tu kwanini Daktari wa Macho kwanini hawezi kutibu moyo
Sababu hajasomea kutibu moyo.
Huwezi ukatibu ugonjwa ambao huujui ulivyo kiundani wala sababu zake na ndio maana daktari wa macho hawezi kutibu moyo.
Ila ataweza kutibu moyo kama akisomea kutibu moyo.
Udaktari ni kada yenye vitengo mbalimbali.
Na unasomea vitengo kadhaa na sio vyote.
Sio vyote sababu hata uchukue uhai wako wote hutoweza kumaliza kusomea hayo magonjwa yote.
Unajua duniani kuna magonjwa mangapi?
jiulize ni nani anaweza kutibu magonjwa yote
Hakuna
Umewahi kufikiri kwanini Madaktari nguli lakini bado wanakwenda Ibadan
Kwani kuwa daktari kunakuzuia vipo kutokwenda ibadani?
Hao madaktari nguli kabla ya kuwa madaktari nguli walikuwa na lifestyle gani?
Leo fikiria kwa upana zaidi Hivi walioandika vitabu vitKatifu walikuwa na upeo gani wa kufikiri?.
Kwani aliyesema kuna gravity ambayo huioni alikuwa na upeo gani wa kufikiri?
Aliyetengeneza artificial light alikuwa na upeo gani wa kufikiri?
Walioandika science walikuwa na upeo gani wa kufikiri?
Waliotengeneza smartphone ambayo unatumia walikuwa na upeo gani wa kufikiri?
Waliofanya uweze kuandika jamiiforums na watu mbalimbali waweze kuona in real time ulichoandika japo tupo mbalimbali walikuwa na uwezo gani wa kufikiri?
Hayo yote yaliyofanyika yalianza taratibu na kuzidi kukua kila siku.
Mfano ni science ambayo hajaandika mtu mmoja bali watu mbalimbali walikuja na mawazo yao ndani ya muda tofauti ndipo ukapata kitu kimoja ambacho ni science.
Na haijaandikwa kwa mkupuo.
Sasa vitabu vya dini havijaandikwa kwa mkupuo bali watu mbalimbali kuja na mawazo yao tofauti ndani ya muda tofauti na kupata vitabu kadhaa vya dini.
Sasa dini ni kama science ya kale.
Ukilinganisha science na dini basi watu waliondika science wana uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko walioandika vitabu vya dini.
Umewahi kuona watu wanapasua Nazi njia panda? Au kuchinja Mbuzi njia panda,
Hiyo sababu wameanishwa hivyo na sababu ya imani zao.
Na ujinga ndani yake.
Umejiuliza Kwanini wafanye hivyo?