Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.

Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamsha kwenye mishe zangu za hapa jijini.

Kesho yake Jumapili waakambiwa warudi tena kweli Jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawaida nikasema ibada ikiisha mtanistua nije kuwachukua.

Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.

Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.

Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.

Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.

Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.

Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?​
Mkuu wanatupiwa mapepo na hao Pastors, manabii, wachungaji, mashetani, hizi dini ni usanii tu.
 
Mimi sikuiona hiyo video kwa kwakweli....ila.mbunge Askofu Ustadhi Rashid Gwajima....sidhani Kama anafimbo sahihi ya kuongoza kondoo.
Gwaji boy ,Mbunge,Ustadhi Rashid ni miongoni wanao tumia Uaskofu kutengeneza pesa ,Mimi nashindwa mpaka leo, wahumini wake wanamwamini na kumkubali Kama Askofu wao au Kuna kitu nje ya pazia.
 
Gwaji boy ,Mbunge,Ustadhi Rashid ni miongoni wanao tumia Uaskofu kutengeneza pesa ,Mimi nashindwa mpaka leo, wahumini wake wanamwamini na kumkubali Kama Askofu wao au Kuna kitu nje ya pazia.
Imani yawengi...Inaanza kwa watu..kabla ya Huyu mawanae muabudu
 
Mwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.

Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.

Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.

Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.

Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.

Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.

Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.

Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.

Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.

Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.

Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.

Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.

Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Lile kanisa la Agape pale Mbezi Africana sasa hivi hakuna hata Kondoo mmoja kazi kubwa nikuweka cd siku za Jumapili ya ibada za zamani
 
Watu wanatafuta pesa tu hapa hamna kingine.
Katika aina za EXCUSES, hii yako inaitwa Selfish Motive. Naona wewe hata ikitokea ukasaidiwa utasema, "Siyo bure; lazima jamaa atakuwa tu kapenda hii black beauty."
 
Hahahahahaha..eti Rashid gwajima...mpaka Sasa hv porn video ya Gwaji boy limenitenga na rafiki yg kipenzi,akibisha lile sio Gwaji boy....tulibishana tukashindwa kuelewana ..akanichukua kuwa mm ni balozi wa shetani..
Mlipoteza muda kujadili utopolo; kwa staili my friend pepo utakayoiona ni ile tu inayovuma kwenye tufani. Mmh hatareee
 
NI kweli miujiza ipo ila shaka yangu kubwa inatokana na mambo makuu mawili, kama umenisoma vizuri hapo juu. Ni kwamba huyu mtumishi baada ya kuwa amekaribishwa na kusimama kwenye madhabahu:

MOJA: Hakutoa hata ile sala fupi tu ya maombi, kuombea program iliypokuwa mbele yake

PILI: Kipindi chote alichokuwa amesimama madhabahuni, hakuwahi kusoma hata fungu moja fupi tu kutoka kwenye maandiko matakatifu.

Hoja yake kubwa ilikuwa ni kwamba apewe hela kwa ajili ya kwenda kufanya uinjilisti, ndiyo topic aliyoongelea mwanzo mpaka mwisho

Sasa haya yote ndiyo yanayonifanya niwe na mashaka makubwa sana kwamba mtumishi wa aina hii anaweza kweli akaambatana na muujiza wa kiwango cha juu kwa kiasi hicho tajwa, wakati hata kule kutoa sala fupi anapokuwa kwenye ibada kwaker ni shida, achilia mbali kusoma fungu fupi kutoka kwenye maandiko matakatifu. Tukio hili lilkitokea mwaka 2014 mwezi Septemba au Oktoba

Halafu kama wewe ni muumini kanisani, naktahadharisha uwe mwangalifu sana na mtumishi yeyote wa Mungu anayesimama madhabahuni halafu akawa anafanya mojawapo ya mambo haya matatu au yote kwa kwa pamoja

MOJA: Mtumishi kukaribishwa madhabahuni halafu akaanza kufundisha somo la maandiko matakatifu bila kuwa limetanguliwa na sala. Hata hivyo hii ina-apply tu kwa haya makanisa yetu ambayo huwa yanaendesha Ibada ambazo usomaji wake wa maandiko hauko guided sana.

MBILI: Mtumishi wa Mungu kusimama madhabahuni akifundisha maandiko matakatifu, bila yeye kuwa anasoma maandiko hayo, badala yake anakuwa amechagua mtu aqu watu miongoni mwa waumini kuwa wanasoma mafungu ya maandiko hayo badala yake yeye ila yeye anakuwa hasomi kabisa. Kwenye ulimwengu wa roho, kuna tofauti kati ya maandiko matakatifu kusomwa kutokea madhabahuni na kutokea sehemu nyingine yoyote ile ndani ya nyumba ya Ibada. Ndiyo maana watumishi huwa wanapanda juu madhabahuni wakiwa na Bibila. Neno linalosomwa na mtumishi kutokea mbele ya waumini au madhabahuni lina nguvu kuliko lile linalosomwa na muumini mwingine yoyote aliyekaa sehemu yoyote ile katikati ya waumini wengine, ndani ya nyuma ya Ibada. Kwa hiyo ukimuona mtumishi ambaye hasomi neno kutokea mbele ya waumini au madhabahuni, uwezekano mkubwa ni kuwa kuna kitu hakiko sawa na kwamba anaweza kuwa anafanya uchakachuaji wa hali ya juu sana.

TATU: Mtumishi wa Mungu kusimama mbele ya madhabahu na kuanza kufundisha maandiko matakaitu kutokea mdomoni kwake. Yaani anakuwa hasomi maandiko na sana sana ikibidi llabda anafaribu kutaja taja mafungu tu. Huyu anayeangukia kwenye kundi hili la mwisho ndiyo hatari zaidi na ni wa kuogopa kama ukoma!
Tatizo lako ni mashaka mengi na kupima mambo ya rohoni kwa macho ya kimwili. Halafu umeandika: "Neno linalosomwa na mtumishi kutokea mbele ya waumini au madhabahuni lina nguvu kuliko lile linalosomwa na muumini mwingine yoyote aliyekaa sehemu yoyote ile katikati ya waumini wengine, ndani ya nyuma ya Ibada."

Sidhani kama ni kweli.
 
Back
Top Bottom