Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.

Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamsha kwenye mishe zangu za hapa jijini.

Kesho yake Jumapili waakambiwa warudi tena kweli Jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawaida nikasema ibada ikiisha mtanistua nije kuwachukua.

Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.

Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.

Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.

Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.

Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.

Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?​
nyingi ni drama
 
Mwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.

Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.

Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.

Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.

Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.

Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.

Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.

Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.

Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.

Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.

Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.

Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.

Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
dadek
 
Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
ww ni chenga aise
 
...wachungaji na hao manabii wapo kimasrahi na ni waongo sana....wengne vitombi hatar yaani anakula kondoo bila huruma tena anachagua zile kondoo mbichimbichi zenye Imani kali....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Khaaaa wallahi nimecheka kwa nguvu aise kuwa na wazazi macomedian raha sana
Kwahiyo huyu ndio role model wako sio?
 
Kwahiyo huyu ndio role model wako sio?
Daah kwa kweli hapo namuunga tu mkono baba jamani! Wachungaji wenyewe wa siku hizi ndiyo design ya kina Mwamposa na Gwajima!

Wewe na Heaven Sent nendeni mkatuwakilishe tu mama! Ninyi ndiyo mtakuwa mnakuja kutuambia nyumbani mliyohubiriwa huko!
 
Tulikuwa tunamuombea Dada anajini mahaba. Mwombezi anayependa mambo ya kuanguka alipoona Dada hafurukuti nikamuona kambinya tumbo na kumfinya mfinyo Mkali Dada akapiga kelele Kali kisha akatulia mwombezi akasema jini limemtoka.

Nilimfuta pale pale kushiriki naye katika huduma za kuwahudumia watoto wa Mungu. Sipendagi ujinga movie yote niliiona
 
Tatizo lako ni mashaka mengi na kupima mambo ya rohoni kwa macho ya kimwili. Halafu umeandika: "Neno linalosomwa na mtumishi kutokea mbele ya waumini au madhabahuni lina nguvu kuliko lile linalosomwa na muumini mwingine yoyote aliyekaa sehemu yoyote ile katikati ya waumini wengine, ndani ya nyuma ya Ibada."

Sidhani kama ni kweli.
Utafiti wa kiroho haugawanwi kama vile tafiti zetu zingine hizi za kwenye makaratasi. Katika hili, wewe uko sahihi, ila mimi niko sahihi zaidi. Nina ushahidi ambao siwezi kuuthibitisha kwa mtu mwingine yeyote yule kwa sababu mwenye jukumu hilo ni Mungu. Binadamu utapewa ufunuo wa kiroho tu, halafu mwenye kuuthibitisha ufunuo huo huo kwa mtu mwingine anabaki kuwa ni Mungu peke yake, si binadamu. Mshirikishe Mungu katikia hili halafu uone atakuambia nini
 
Mwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.

Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.

Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.

Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.

Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.

Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.

Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.

Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.

Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.

Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.

Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.

Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.

Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Utafiti wa kiroho haugawanwi kama vile tafiti zetu zingine hizi za kwenye makaratasi. Katika hili, wewe uko sahihi, ila mimi niko sahihi zaidi. Nina ushahidi ambao siwezi kuuthibitisha kwa mtu mwingine yeyote yule kwa sababu mwenye jukumu hilo ni Mungu. Binadamu utapewa ufunuo wa kiroho tu, halafu mwenye kuuthibitisha ufunuo huo huo kwa mtu mwingine anabaki kuwa ni Mungu peke yake, si binadamu. Mshirikishe Mungu katikia hili halafu uone atakuambia nini
Hukujibu swali, umelikwepa wewe jamaa
 
Back
Top Bottom