Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Tangu nilipomuona Fernandez kwenye kutapeli Madini dhahabu feki nimeyazarau sana haya makanisa
 
sitakaa nisahau mama mmoja alikuwa mja mzito alipelekwa kuombewa kisa ana mapepo kumbe ni kila kichaa kinaitwa kichaa cha mimba mama wa watu walipigwa mangumu pepo atoke in short alikuja kupoteza maisha.........Nina rafiki yangu mmoja mchaga tulikuwa tunaongea naye nikamuuliza aise wakristo kwa ujumla wao ni watu waliosoma sana elimu dunia kuliko waislam lakini ajabu ni kwamba pamoja na kusoma kwao ni rahisi sana kumuingiza mkenge au mjini mkiristo kuliko muislam.
Nikamukumbusha kikombe cha babu nikamkumbusha wale waumini waliokufa Moshi kwa ajili ya moto.
Wanawake ndio rahisi zaidi kuingizwa mjini.Nikamuambia umeshawahi kuona muislam anajiita nabii.Akaniambia muislamu akijitokeza akajiita nabii wanaondoka na shingo yake
 
Ahahaha..haya mambo bwana Yapo ndugu zangu .Ya kweli na Ya kitapeli pia.

Always kumbuka udanganyifu huwa hauji plainly kama ulivyo maana ni rahis kugundulila ndio maana lazima udanganyitu uji associate na ukwel ili upate tabu kung'amua.
So ukiona utapeli unafanyika kwenye hiz mambo za nguvu za kiroho then just understand dat the "real buznes" is real.Hawa wajasiriamali wachumia tumbo hawajanza leo na hawatatoweka mpaka mwisho wa dunia.Na kingine ambacho ni bahat mbaya sana ni kwamba wahitaji wa hiz huduma (kama ndugu wa mtoa mada hapo) mara nyingi huwa wanakutana na wrong people. But real God serving people are though out there.

MY TESTIMONY ON THIS.
Kabla sijachanganyikiwa na maisha nilikua (na bado) napenda sana kujifunza mambo ya Mungu.Sana na Maombi ya kumuombea mtu akashukiwa na Nguvu anayoshindwa kuistahimili mpaka kuanguka NISHAFANYA HIZO huduma.
Ilikuaje??

Family home ni wa Moravian.Ujana kama kawaida UKWATA imetulea wengi tukiwa wanafunzi mpaka kipindi naoa ndio nikayajuaga haya makanisa ya Kilokole na kuanza kushiriki huko TAG.
Bas hapo nikakutana na mchungaji aliyenikuza vizur sana na kunijenga kwa habar ya mambo ya Mungu.Ofcz nilikua na content ya kidin ila huyu akani shape namna ya kuitumia na kunifundisha zaid.Ilinichukua Muda mpka kuanza kupewa fursa ya kufanya service za kuhubir na maombezi.

I REMEMBER FIRST TIME kumuwekea mkono mtu kichwani na yeye kupigwa mweleka ILINISTAAJABISHA SANA ingawa nilizoea kwa kuona na niliogopa sana.But NI VITU REAL NA VIPO KABISA.
Kutana tu na watumishi wa Mungu kweli.
Sio hawa wababaishaji.

Nawasilisha
 
Umeongea kwel.Watu ni wabinafsi sana hawa wanaoji potray kama watumishi wa Mungu.
Lakin haiondoi ukwel kwamba watumishi wa kweli wapo.Wapo!!!
 
Aaaah mkuu yani nijiulize maswali yote hayo alaf bado tena nije nijiulize maswali ya maisha yangu aaah mkuu niache kidogo maswali ya maisha yangu yenyewe changamoto tosha
 
Mkuu wewe bado mchanga sana.
Inabidi utulie uanze kupewa mafundisho ya ulimwengu wa roho.
Ni elimu rahisi ila ni ngumu pia inategemea wewe unaishi maisha gani
 
Ha haaaaa uminikumbusha vibao vya kustukiza vya kisogoni E.A.G.T city center kwa pastor Katunzi....vinavurugaaa ila sikudondoka
Kwenye daraja mtoni mtongani kwa Florence[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hili kanisa halipotena na mchungaji wake pia yuko mahabusu
 
Mimi niliwahi kujifanya natetemeka kama nina wazimu ili tu nisimwaibishe mchungaji. Lkn nilikuwa naekti tuu basi na yeye akawa anazidi kunikandamiza kichwa. Nilicheka sana siku iyo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sio kila anayedondoka ana mapepo. Wale waombeaji bana wanasukuma balaa na ukikataa basi wanasema ni pepo bishi
 
😁😁😁😁
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Hakika ni muhimu sana mtu kutafuta kuijua kweli ya Mungu na kweli ya Mungu pekee ndiyo iwezayo kukuweka Huru ni wazi kuwa jamii tunayoishi nayo wengi wanauhitaji ya kimaisha kiuchumi na hata shida za kimahusiano pia,hili ndio upelekea watu wengi kumtafuta Mungu ili wapate mahitaji yao lakin ni wachache sana ambao huwa wanatafakari namna gani wanaweza kufanya jambo ambalo litampendeza moyo wa Mungu,kifupi ni hv watu wengi wanataka Mungu awafanyie kitu na hawatafuti kumfanyia Mungu kitu
 
Na pia kuna vitu haviwezi kumtoka mtu hata akiombewa kiasi gani lkn vinaweza kumtoka pale anapoanza kutafuta Mungu anasema nini katika vitabu vitakatifu
 
 
Hakuna muislam hapo ni makafiri tu hao
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ila mwamposa kateka watu Jamani..huku mtaani kwetu waislamu kwa wakristo kila jumapili wanakusanyana kuelekea kawe.
 
Nakumbuka mwaka 2018 Kuna kanisa lipo pale ilboru jina tunahifadhi kidogo ...buana weee nikaenda kuombewa nilikuwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara kwa ushawishi wa rafiki zangu nikaenda, sasa yule jamaa aliekuwa ananiombea akawa ananiombea taratibu baadae akapandisha mzuka akaanza kunisukuma nidondoke nika kaza nilipoona hamalizi na mim nimechoka kusimama, nikakaa bila kudondoka, akanifuata hukohuko chin akaendelea kunisukuma nidondoke basi kiroho safi nikaenda chini nikalala chali ndo maombi yakaisha, ...najiuliza ivi kama ningekaza maombi yasingeisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…