Inashangaza Sana kuona Tanzania Kuna wapuuz wengi wait tangu Corona ianze wanaombea vifo viongezeke, wanaombea wagonjwa waongezeke. Taarifa zikitolewa kwamba Tanzania Kuna wagonjwa 20 wenyewe wanakomaa wapo wengi ukimuuliza kwenu kuna wagonjwa wangapi hana jibu means wore wapo safe. Tatizo wanasiasa wa Tanzania hutumua majanga kujichukulia umaarufu. Nyie mnaoombaTanzania iwe na Corona siku ukipoteza hata mtu mmoja kwenye familia yako kwa ajili ya Corona ndo hapo mtaungana na wengine kuliombea Taifa. Kama upo safe tulia unawashwa Nini, unataka kuiga mataifa mengine, umekomaa na WHO wanatoa taarifa za Kisayansi kumbuka WHO inaongozwa na hao waliokuwa Colonialist waliowanyonya na kuwakandamiza babu zetu, acheni kushikiwa akili. Tanzania ipo safe tuendelee kuchukua Tahadhari.
Mtoa Mada upo Out Of context kama ulivopenda kulitumia hilo neno kwenye thread yako.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu:
1. Watu wanaohadharisha kuzuia maambukizi kusambaa au kuongezeka hawawezi kuwa wanaliombea taifa vifo. Isipokuwa wale walio kinyume na hadhari hizo.
2. watu waliohadharisha kuuzuia ugonjwa kuingia nchini ili vifo vya ugonjwa huu visitufike, hawawezi kuwa walikuwa waliliombea taifa vifo, isipokuwa wale waliopuuzia yote hadi ugonjwa ukatufika.
3. Kwamba hujui kuwa pana ndugu zetu wamekufa kwa Corona hata unajinasibu bila ya aibu kusema sote tuko safe? Mkuu utakuwa hukijui unachokisema.
Si, Ummy, Majaliwa au hata jiwe mwenyewe atakubaliana nawe kwenye hilo. Kuwa na ubinadamu angalau kidogo basi kwa kutowacheza shere waathirika wote wa moja kwa moja wa ugonjwa huu uliosababishwa na uzembe wa watu wachache na ambao kwa hakika wanajulikana.
Indian woman whose husband died of Covid-19 in Tanzania reunites
4. Mnaowawashwa siyo nyinyi kweli? Kama mnadhani tuko salama, makelele yako ni ya nini? Si wewe hujafiwa, hufiwi wala hujafiwa?
Kwa nini mnawazuia watu kutangaza matukio yao binafsi hata ya ugonjwa huu?
Mwananchi: Kwenye daftari la mazishi ya vifo vya COVID19 Jina la babangu lilikuwa namba 256 (Amana Hospital-Ilala) - JamiiForums
Mkuu acheni kutucheza shere tukipoteza jamaa zetu wakati nyie mkiingiza per diem zenu Chatto na sasa Dodoma.
5. Wa kuidunisha WHO ni wewe? Hujui unachokisema. Haiyumkiniki ndiyo sababu waswahili walisema, "asiyejua maana haambiwi maana." Kaa hivyo hivyo hadi utakaposikia Corona ikikogongea mlangoni kwako.
6. Eti mtoa mada upo "out of context." Statement hiyo haiendi hivyo bila ya ushahidi.
Hukuweka ushahidi wowote wala huna ushahidi wowote kufikia usemi huo. Kwa maana nyingine ni kama "uko unaota ota tu."
7. Ugonjwa huu kama ilivyo mada, hakuna cha siasa hapo. Kama unataka siasa fuata wenyewe waliko. Hatutakujibu Corona, hatutaki kufa na Corona inayosokomezwa kwetu na mtu yeyote anayeweka maslahi yake binafsi mbele.
Soma mada kuelewa mkuu, ikibidi wakati huna maluweluwe ya kujifukiza nyungu:
: