"Kuishi na Corona" kunavyopotoshwa Tanzania

Wewe ambae haumtukuzi mzungu kitu gani umekifanya kuliko hao wazungu? Kwanini mnaendekeza mihemko kuliko logic? Mbona ukiumwa unaenda hospitali kupigwa ma exray? Dawa zote unazozitumia zinatengenezwa nani? ,Magufuli hapo alipo kila kitu anatumia cha mzungu kuanzia suti zake, magari, simu, Tv na vitu vingne.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzungu ndio kagundua football lakini mfalme wa mpira ni mweusi Pele.
Mzungu kagundua basketball lakini mfalme wa basketball ni mweusi Jordan
Mwaka 2018 france kachukua worldcup akiwa na wachezaji 7 weusi kwenye first eleven.
Ufaransa 1998 kachukua worldcup akiwa na wachezaji 6 weusi .
Kuanzisha jambo haimaanishi unajua kila kitu.

Kwa hiyo mnyama tumweke kwenye(Corona) cage? Hiyo Cage wapi kama sio total lockdown.

Narudia tena wewe kama unataka kukaa ndani kaaa hujakatazwa,ila wengine wacha wasio uhakina na kipato wacha wakawatafutie watoto wao chakula alafu kuna nchi nyingi hazijafanya lockdown huko ulaya Beralus huko shughuli zinaendelea kama kawa na ligi yao inaendelea na mashabiki wana ruhusiwa kuingia.Sweden haina total lockdown maisha yanaendelea kama kawa.
 
Nimeandika kila kitu, labda kama unataka bwana k aje akupe rizi, mimi sina..!
Mkuu kwani wewe umechungulia nini unachokijua kuhusu WHO ambacho wewe hujakiweka hapa kuhusiana na hii mada?
Mada iko wazi "kuishi na Corona kwa mujibu wa WHO" ambako mada inatambua dhana hiyo kuwa ina mashiko.
Kama Corona ilivyo, mada inatambua Corona ni kama mnyama mkali ambaye inawezekana kuishi naye salama, lakini akiwa kwenye udhibiti.
1. Mada imetambua nchi zilizo fanikiwa kumweka mnyama mkali huyu mahali salama anapopaswa kuwa.
2. Mada inatambua nchi zinazopambana kumweka mnyama mkali huyu anapopaswa kuwa.
3. Mada inatambua nchi ambazo mnyama mkali huyu yungali yuko mitaani na wanajaribu kuishi naye hivyo hivyo.
Mada iko humo tu si zaidi?
Mkuu hizo ramli zingine unazoongelea zinahusika vipi hapa?
 
Kwa hiyo mnyama tumweke kwenye(Corona) cage? Hiyo Cage wapi kama sio total lockdown.

Narudia tena wewe kama unataka kukaa ndani kaaa hujakatazwa,ila wengine wacha wasio uhakina na kipato wacha wakawatafutie watoto wao chakula alafu kuna nchi nyingi hazijafanya lockdown huko ulaya Beralus huko shughuli zinaendelea kama kawa na ligi yao inaendelea na mashabiki wana ruhusiwa kuingia.Sweden haina total lockdown maisha yanaendelea kama kawa.

Mkuu 'Dawa ya mbu.'

Niko busy sasa hivi napiga nyungu, tayari kwa chereko chereko za jumapili.

Nipe muda tafadhali.

Bye bye amigo don't even remember to write back.
 
Wee endele kujifungia na kupiga nyungu.Sisi wengine acha tukawatafutie ugali watoto wetu.
 
Mzungu ndio kagundua football lakini mfalme wa mpira ni mweusi Pele.
Mzungu kagundua basketball lakini mfalme wa basketball ni mweusi Jordan
Mwaka 2018 france kachukua worldcup akiwa na wachezaji 7 weusi kwenye first eleven.
Ufaransa 1998 kachukua worldcup akiwa na wachezaji 6 weusi .
Kuanzisha jambo haimaanishi unajua kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pamoja na kuwa nakubaliana nawe kuwa kuanzisha jambo si fursa ya kuwa ndiyo wewe ulijue zaidi kuliko wote tena at all times, sioni relevance ya suala hili kwenye hii mada.

Kwenye mada hii, hayapo mashindano wala ubishi wa nani zaidi wala nani anajua nini zaidi ya nani.

Hapa pana mada, a plain mada kama ilivyo:

IMG_20200520_173123_274.jpg

Sijaona kinachoainishwa kama tatizo kwenye mada, zaidi ya kuwa hata bandiko lako pia lina sequence of true statements ambazo hata hivyo hazihusiani na somo liliopo at hand.
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada. Itifaki yote imezingatiwa.

Shirika la afya Ulimwenguni (WHO), limekuwa likitoa tathmini, mapendekezo na kauli mbalimbali likionya na kushauri kwenye jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu hatari.

Kwa bahati mbaya sana hapa nchini kwetu kumekuwa na upotoshwaji wa wazi kwenye baadhi ya jitihada hizo za WHO.

Ushauri wao usipokubaliana na misimamo ya viongozi wetu, utasikia, "wanatumiwa na mabeberu hao". Ushauri ukiangukia tulipo, tunaukumbatia kwa chereko chereko, hata kama ni nje kabisa ya uhalisia (out of context).

Mifano ni mingi ila kwenye uzi huu, itoshe kuangazia kauli yao hii muhimu ya 'kwenye kuishi na Corona.'

Kwa tathmini za wazi na kwa jinsi maambukizi ya ugonjwa huu yalivyo, WHO walisema:

"ugonjwa huu si wa kuondoka leo au kesho." Kwamba, "itabidi tu kujifunza namna ya kuendelea kuishi nao hadi pale tiba au chanjo kamili itakapopatikana".

Kauli hii imekuwa ikinukuliwa hapa nchini nje ya uhalisia (out of context), kuwa WHO wamepata funzo toka kwa rais wetu mpendwa na kuwa eti sasa sisi tuko kwenye mstari wa mbele tayari kuishi na Corona.

Haiyumkiniki hata hizi chereko chereko na mayowe ya ushindi dhidi ya Corona chini ya bwana yule hapo jumapili ni kwa minajili hiyo.

Kauli ya WHO ni kauli sahihi ya kisayansi na iliyokamilika. Kauli ile haitokei hewani bali ina vigezo kamili vilivyo zingatiwa. Kiuhalisia nchi (yenye Corona) haianzi kuishi tu na Corona from nowhere. Kuna pa kuanzia (starting point) kabla ya kufikia kwenye hatua ya kuishi na ugonjwa huu hatari Ila katika hali ya usalama. Hii ikiwa, wakati hatua zingine zikisubiriwa.

Nchi zote tunazozisikia kuwa zinalegeza masharti yao ya udhibiti zilizo kuwa zimejiwekea, huko kulegeza hayo masharti, ndiyo katika kujipanga kuingia sasa salama kwenye awamu hii ya pili ya kuendelea na maisha kwa tahadhari wakati ugonjwa huu ukingalipo. Angalizo la msingi, "lakini ugonjwa ukiwa umedhibitiwa vilivyo kwanza."

Rwanda, Uganda, USA, UK, Australia, New Zealand, Namibia, Italy, Spain nk, ni mfano wa nchi zilizoko kwenye hatua hizo. Kenya wanapambana vilivyo ili nao angalau waweze kufika kwenye hatua hiyo.

Unaweza ishi na mnyama hatari aliyeko kwenye cage au mhalifu hatari aliyeko jela si anayezurura huru mitaani.

Brazil, Tanzania, Sudan kusini, Burundi, Congo nk, tungali na makundi ya simba, chui, fisi, mbwa mwitu, nk yakizurura mitaani mwetu.

Eti kuwa tunataka sasa kujiaminisha na kuwaachia watoto wetu wadogo kabisa wa chekechea wajiendee tu shule peke yao kwamba wanyama hao watawazoea tu muda unavyopita! Mbona itakuwa ni kujidanganya kwa wazi kuliko pitiliza mno?

Brazil na sisi kwa hali ya sasa kimsingi tofauti haiwezi kuwapo. Kiuhalisia maambukizi yangali bado yanaongezeka sana. Tunatofautiana kwa viwango tu na hilo kwa mwendo wetu huu ni suala la muda tu.

Angalia hapa hawa (Brazil). Wanaanza vipi kuishi na Corona katika hali hii waliyomo sasa?

Kilicho wafikisha hapo ni kama hiki hiki cha kwetu - kibri kilicho pitiliza cha kiongozi wao mkuu.

Asante kwa uchambuzi yakinifu. Ni kweli tupu, hali ya corona USA, Spain, UK, nchi nyingine zilizoendelea ni tofauti kabisa na Tanzania. Nchi hizo zimefikia kilele (peak) ya maambukizi na wanaanza kufungua BAADHI ya secta walizofunga sio kila kitu. Sisi hatujafikia kilele cha maambukizi, hakuna takwimu sahihi na tunataka maisha yaendelee kama kawaida wakati kirusi kipo kwa wingi na kwanza ndio kinasambaa. Tutegemee hali mbaya sana baadaye. Nashangaa watu wanasifia serikali jinsi ilivyo kabili corona! Hakuna taifa lililofanya hovyo kama sisi. Ndio maana nasema tuombe Mungu tu manake vinginevyo hali itakuwa siyo.
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada. Itifaki yote imezingatiwa.

Shirika la afya Ulimwenguni (WHO), limekuwa likitoa tathmini, mapendekezo na kauli mbalimbali likionya na kushauri kwenye jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu hatari.

Kwa bahati mbaya sana hapa nchini kwetu kumekuwa na upotoshwaji wa wazi kwenye baadhi ya jitihada hizo za WHO.

Ushauri wao usipokubaliana na misimamo ya viongozi wetu, utasikia, "wanatumiwa na mabeberu hao". Ushauri ukiangukia tulipo, tunaukumbatia kwa chereko chereko, hata kama ni nje kabisa ya uhalisia (out of context).

Mifano ni mingi ila kwenye uzi huu, itoshe kuangazia kauli yao hii muhimu ya 'kwenye kuishi na Corona.'

Kwa tathmini za wazi na kwa jinsi maambukizi ya ugonjwa huu yalivyo, WHO walisema:

"ugonjwa huu si wa kuondoka leo au kesho." Kwamba, "itabidi tu kujifunza namna ya kuendelea kuishi nao hadi pale tiba au chanjo kamili itakapopatikana".

Kauli hii imekuwa ikinukuliwa hapa nchini nje ya uhalisia (out of context), kuwa WHO wamepata funzo toka kwa rais wetu mpendwa na kuwa eti sasa sisi tuko kwenye mstari wa mbele tayari kuishi na Corona.

Haiyumkiniki hata hizi chereko chereko na mayowe ya ushindi dhidi ya Corona chini ya bwana yule hapo jumapili ni kwa minajili hiyo.

Kauli ya WHO ni kauli sahihi ya kisayansi na iliyokamilika. Kauli ile haitokei hewani bali ina vigezo kamili vilivyo zingatiwa. Kiuhalisia nchi (yenye Corona) haianzi kuishi tu na Corona from nowhere. Kuna pa kuanzia (starting point) kabla ya kufikia kwenye hatua ya kuishi na ugonjwa huu hatari Ila katika hali ya usalama. Hii ikiwa, wakati hatua zingine zikisubiriwa.

Nchi zote tunazozisikia kuwa zinalegeza masharti yao ya udhibiti zilizo kuwa zimejiwekea, huko kulegeza hayo masharti, ndiyo katika kujipanga kuingia sasa salama kwenye awamu hii ya pili ya kuendelea na maisha kwa tahadhari wakati ugonjwa huu ukingalipo. Angalizo la msingi, "lakini ugonjwa ukiwa umedhibitiwa vilivyo kwanza."

Rwanda, Uganda, USA, UK, Australia, New Zealand, Namibia, Italy, Spain nk, ni mfano wa nchi zilizoko kwenye hatua hizo. Kenya wanapambana vilivyo ili nao angalau waweze kufika kwenye hatua hiyo.

Unaweza ishi na mnyama hatari aliyeko kwenye cage au mhalifu hatari aliyeko jela si anayezurura huru mitaani.

Brazil, Tanzania, Sudan kusini, Burundi, Congo nk, tungali na makundi ya simba, chui, fisi, mbwa mwitu, nk yakizurura mitaani mwetu.

Eti kuwa tunataka sasa kujiaminisha na kuwaachia watoto wetu wadogo kabisa wa chekechea wajiendee tu shule peke yao kwamba wanyama hao watawazoea tu muda unavyopita! Mbona itakuwa ni kujidanganya kwa wazi kuliko pitiliza mno?

Brazil na sisi kwa hali ya sasa kimsingi tofauti haiwezi kuwapo. Kiuhalisia maambukizi yangali bado yanaongezeka sana. Tunatofautiana kwa viwango tu na hilo kwa mwendo wetu huu ni suala la muda tu.

Angalia hapa hawa (Brazil). Wanaanza vipi kuishi na Corona katika hali hii waliyomo sasa?

Kilicho wafikisha hapo ni kama hiki hiki cha kwetu - kibri kilicho pitiliza cha kiongozi wao mkuu.
Unatumiwa na mabeberu wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwendeni huko mmeanza kusema tusubiri, sijui Corona itatunyoosha karibia miezi mitatu na bado tunadunda.

Mtasubiri sana.

WHO ndio wamekuwa wapuuzi kabisa siku hizi. Walisema Corona haienezwi kati ya mtu na mtu. Wakasema Barakoa wavae wagonjwa tu.

Baadae wanakuja tena kukanusha. Kila habari mbaya wanaitabiria Africa wakati wazungu ndio wanakufa kama kuku wa mdondo.

WHO wapite hivi ndio maana Trump anawazingua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu haujui kuwa watu wanapukutika Tanzania? Au Kwa kuwa wanaficha kwa kisingizio kuwa vipimo vimeharibika na mapapai? Idadi ya maaambukizi Tanzania hata kenya haitufikiii hata nusu, na waliokufa hata kenya haitufikii hata nusu, angalia tu waziri wa mambo ya ndani kapoteza Ndugu Saba hiyo ni ukooo mmoja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nimemwelewa mleta mada ni kwamba hatupaswi kuacha kuzingatia makatazo ambayo yanapaswa kufuatwa kuepukana na maambukizo haya so kusema watu watoke wakaafanye sherehe au kuparty hapo si ndo kuruhusu misongamano? Kila siku tuko kitaa ila kwa tahadahri sasa ukiwaruhusu wabongo na kuwaambia korona imeisha ni kama unataka watu waambukizane wenye kufa wafe.
Kwani unafikiri hata sasa ni kipi kikubwa kilichobadilika au kufanyika ambacho husaidia kuepusha maambukizi? Maana ukiangalia shughuli nyingi bado zinaendelea na zenye kufanya mikusanyiko na huku mitaani maisha yapo kama kawaida. Kwahiyo kwa hali ilivyo hata hiyo party haitokuwa jambo la ajabu.
 
Mkuu haujui kuwa watu wanapukutika Tanzania? Au Kwa kuwa wanaficha kwa kisingizio kuwa vipimo vimeharibika na mapapai? Idadi ya maaambukizi Tanzania hata kenya haitufikiii hata nusu, na waliokufa hata kenya haitufikii hata nusu, angalia tu waziri wa mambo ya ndani kapoteza Ndugu Saba hiyo ni ukooo mmoja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kututajia watu saba wa waziri wa mambo ya ndani waliokufa na Corona?
 
Mimi ni majirani zangu so far waliokufa naowajua ni baba ake George na mdogo wake wengine sijasikia na sijui kama ni covid
 
Manake msiba wake niliona ITV waki uripoti na ulifanyikia nyumbani kwa mzee wake na watu walikuwa wanaenda kutoa pole au ndio tuna unganisha misiba yote iliyotokea kipindi hiki cha partial lockdown wamekufa na Corona.
 
Mkuu haujui kuwa watu wanapukutika Tanzania? Au Kwa kuwa wanaficha kwa kisingizio kuwa vipimo vimeharibika na mapapai? Idadi ya maaambukizi Tanzania hata kenya haitufikiii hata nusu, na waliokufa hata kenya haitufikii hata nusu, angalia tu waziri wa mambo ya ndani kapoteza Ndugu Saba hiyo ni ukooo mmoja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanakufa wapi huko?

Mbona huku niliko sijaona, na hakuna mtu ninayemfahamu kafa kwa corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom