ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Jirani wa kwanza yeye ana shamba lake la mahindi sasa mbwa wake amezaa akawa anasubiri nikienda kazini anakuja kumuazima wife kambwa changu kisa kanabweka anakachukua anaenda nacho shamba kwenda kulinda dhidi ya tumbili. Sijui kama huko anampa chakula au hampi ila jioni anamrudisha imagine mbwa nilimchukua ili alinde mifugo yangu yeye anakuja kumchukua na hapo ni MPAka aje avune wife wakamwambia watampa mahindi.. inachekesha sana sasa shida nikaanza kuona noma kumkataza maana me mgeni mtaani kwao nikaona itaonekana Nina roho mbaya.
Mwingine yeye kaamka asubuhi bila kunipa taarifa kaanza kuukata mti upo ndani ya eneo langu kisa tu Kuna siku nilisema huu mti nitatafuta mtu aupunguze.Alipaswa aje aniambie jirani mti nakusaidia kuukata huu basi yeye kaamka bila hata Salamu Mzee..nikashindwa ku react chochote maana nimekuta kaukata kaenda kutengenezea mkaa..
Majiran wa bongo nyoso sana ila pia hii nimegundua inasababishwa na wake zetu kupeana peana vitu kugawana gawana mboga na kwenda kukaa kaa ndani mwa watu kupiga stori inapelekea jirani anajiona na ye ni member wa familia yako..