Kuja kwa Sevilla: Simba watapigwa hadi wachakae!

Kuja kwa Sevilla: Simba watapigwa hadi wachakae!

Kwa mfano,Samahani lkn;Sevilla ya kutoka HISPANIA ikifungwa na Simba Sc ya kutoka TANZANIA,Wewe Utaumiaje?
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
Hawezi mfunga,
Yaan itakuwa aibu mkuu, na itathibitisha kuwa sisi kwenye soka bado sana! Hizi tambo za hapa na pale hazina maana. Nadhani baada ya kipigo pamoja na kuchukua ubingwa timu itafumuliwa kama sivyo next year ligi ya mabingwa watatolewa mapema mno.
 
Wakuu,
Natabiri hawa mabingwa watetezi na watarajiwa ligi kuu kulambwa bao kadhaa pale kwa mchina na kutuabisha sana. Kama unaamini kama mimi sema "mnyama atakatwa mkia"
Teh teh teh!
Tuanzie hapa kwanza,wewe ni mshabiki wa timu gani hapa Tanzania...?
 
Mujiandae kwa kichapo tu Mtani. Japo wanaeza waonea huruma pia sababu nyie ndio wenyeji wao angalau mkasuluhu nao.
Duuh mshaanza sasa, kwa hiyo wakitufunga hatuna uwezo 😐,tukisuluhu nao wametuonea huruma 😱,na tukiwafunga tumebahatisha /kikosi b /tumehonga marefa /hawakujituma uwanjani. 😃Mnakwama wapi aisee Shadeeya
 
Hata tukifungwa goli 100, Simba hatakuja kuwa Chura!!

Nyie vyura size yenu ni Mabwepande FC timu ya daraja la 6, mnakaribishwa kuja kuangalia mechi ya kiume Simba wakikipiga na Timu kubws ya Ulaya. Walau 2050 mtapata nafasi ya kucheza walau na timu kubwa pale Burundi Ntambamulugamba FC!

Gracias muchus!
 
Mkuu stephot
Tuanzie hapa kwanza,wewe ni mshabiki wa timu gani hapa Tanzania...?
Hata nikikwambia mimi ni shabiki wa timu xyz itakusaidia nini? Subiri utaona kipigo cha mbwa kwa mnyama ile ni timu ya ulimwengu wa kwanza, soka ni sayansi na sayansi ya timu ya mnyama ni ndogo mno hasa akikutana na timu kubwa kubwa.
 
Ninasema hivyo kwa sababu haya maneno yalishasemwa sana na wenzetu wa upande wa pili matokeo yake tukishinda mtaanza kusema tuliwawekea wachezaji wao sumu ili tuwafunge...
 
Ninasema hivyo kwa sababu haya maneno yalishasemwa sana na wenzetu wa upande wa pili matokeo yake tukishinda mtaanza kusema tuliwawekea wachezaji wao sumu ili tuwafunge...
Teh teh teh, nimecheeka! Acha kujihami mkuu! Hao jamaa wamekuja kumla mnyama na baadae wakale bata (kutalii)
 
Back
Top Bottom